Kwani IMF imetoa trilioni 2.4 kwa Tanzania ?

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Jibu ni wazi kabisa wkamba, kutokana na kutambua rekodi ya Tanzania katika utekelezaji wa mageuzi na pia utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu ambapo fedha hizo zitatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo pamoja na kuleta nafuu kwenye mfumuko wa bei kwa kushusha bei ya mafuta na uchumi jumuishi.

Aidha, Naibu Mkurugenzi Mtendaji na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya IMF, Bo Li, alisema wameridhishwa na hatua za serikali ya Tanzania katika kupunguza matumizi na kuelekeza nguvu kuboresha huduma za kijamii kwa ufanisi kwa wananchi.

Pia, Hizi ni fedha za masharti nafuu, zitasaidia kushusha bei ya mafuta, ruzuku ya pembejeo, kuwezesha vijana na makundi maalum. Haya ni matokeao ya dhamira njema ya serikali ya awamu ya sita, iko tayari kuendana na dunia.
 
Lugha nzuri ni "IMF imeikopesha Tanzania .........."
Tuanzie hapo, TUMEKOPESHWA TENA 2.4 trilion
 
Back
Top Bottom