Serikali irudishe pesa za IMF trilioni 2.4, ni nyingi sana - zote hizi za nini?

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,843
Wataalam mtanipa elimu kidogo kama nipo tofauti. Hivi hii mikataba ya kuingia mkopo na mabenki makubwa ni nani anaepitisha?

Je, ni kweli bunge tulilonalo linaridhia hivi vitu? Mimi naona hapana vinginevyo hili Bunge Letu litakuwa limelogwa. Hii mikopo mikubwa mikubwa mbona inakuja kwa mlipuko kiasi hiki.

Mbona hatuoni matokeo chanya yanaonekana kwa wananchi kutokana na hii mikopo jamani. Nina uhakika wa asilimia mia ipo siku utawala wa huyu mama utaota magamba kila uchafu wanaoficha utakuwa wazi.

Kama Bunge linapitisha hii mikopo kwa kumuogopa Rais kwa kuwa ni mwenyekiti wao wa chama kisheria hii ni undue influence which renders contract void and void ab initio. Nawalipaji wa haya mamikopo ya kihuni ni sisi Watanzania.

Pia soma - Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF

Ipo siku maneno yatakwisha ya kusema tutasema kwa vitendo sasa.
 
Unashauri serikali ifanyie nini hizo pesa za mikopo? Tatizo sio kukopa tazizo unakuta mtu amekoppa anaenda kufanyia sherehe:p Maana yake hela inatumika sio katika uzalishaji. .

Ningefurahi kama ungeshauri wafanyie nini hizo hela. Ili mkopo uwe na tija. Mie nashauri wanajeshi wangepewa wafugie nguruwe hizo hela, baada ya miezi mitatu mpaka sita tutakuwa tunawauza nje huko tutapiga hela sana. Nguruwe wanalipa pesa mingi kwa return. .
 
Warudishe tu, mamiradi mangapi yamewashinda. Hivyo viwanda walivyokuwa wanajimwambafai viko wapi? Royal tour ilvyoyeyuka kama barafu.
 
Hii nchi sisi ni Watanzania ni wazembe kiwango cha SGR, na kwa kulijua hilo wanafanya mambo ya hovyo wakijua wajinga sisi hatuna la kufanya zaidi ya wachache kulia lia mtandaoni.
Kila kiongozi anaeingia anapiga dili zake anapotea, hakuna mzalendo, hakuna anaejali tanzaniia ya kesho, sababu tanzania ya leo wanaila na kesho wameshawatengenezea watoto wao sio watanzania, ni watoto zao.
 
Mikopo ni tools ya kuifanya afrika izidi kuwa masikini, watoa mikopo wanajua kabisa hizo pesa haziwezi leta positive change, bali zitarudishwa kufichwa kwenye bank za Ulaya na walamba asali, kwa expenses ya walipa kodi.
Wangekuwa na nia ya dhati kuisaidia afrika wao wenyewe ndio wangeingia front kuzifanya hizo project na kuzikabidhi kwa wananchi na sio kuwakabidhi fisi pesa.
 
Hii nchi sisi ni Watanzania ni wazembe kiwango cha SGR, na kwa kulijua hilo wanafanya mambo ya hovyo wakijua wajinga sisi hatuna la kufanya zaidi ya wachache kulia lia mtandaoni.
Kila kiongozi anaeingia anapiga dili zake anapotea, hakuna mzalendo, hakuna anaejali tanzaniia ya kesho, sababu tanzania ya leo wanaila na kesho wameshawatengenezea watoto wao sio watanzania, ni watoto zao.
Uongozi ni ajira binafsi kwa ajili ya kutatua matatizo binafsi ya kiongozi na sio ya jamii.
Mwafrika bado yupo kwenye hatua ya awali ya ukuaji,hivyo hawezi mletea maendeleo mwafrika mwenzake.
 
Dogo mpaka mkopo utoke ni lazima mkataba umesainiwa wa kuomba hicho kiasi cha pesa ikiwa imeambatanishwa na mchanganuo wa kazi husika

La maana ni kuomba riba ipunguzwe na riba ya adhabu isiwepo.

Hii mikopo italipwa hadi kizazi cha nne wataendelea kulipa.
 
Huwa nawaza kama pangekuwepo na sheria ya kuwabana hawa wakopaji, ikiwezrkana kila anayekopa arudishe mikopo yake kabla muda wake haujakwisha wa kukaa madarakani.

Hii mikopo imekuja kudumaza akili za viongozi wetu, ndio maana siku hizi wanaona kukopa sifa, kauli kama "tunakopesheka" au "mikopo ya masharti nafuu" zinazidi kutawala.
 
Unashauri serikali ifanyie nini hizo pesa za mikopo? Tatizo sio kukopa tazizo unakuta mtu amekoppa anaenda kufanyia sherehe:p Maana yake hela inatumika sio katika uzalishaji. .

Ningefurahi kama ungeshauri wafanyie nini hizo hela. Ili mkopo uwe na tija. Mie nashauri wanajeshi wangepewa wafugie nguruwe hizo hela, baada ya miezi mitatu mpaka sita tutakuwa tunawauza nje huko tutapiga hela sana. Nguruwe wanalipa pesa mingi kwa return. .
Hizo zinaingia mifukoni mwao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom