Watanzania wanataka nini kwa CHADEMA?

Oh my God!! Yu are terribly wrong and coherent in exhibiting your IQ!

we are the employer we are asking employee what he will do for us and you are saying we are wrong??? if u belong to CDM please feel free to respond to this question convince him and other citizen! ulichojibu ni kukwepa swali na kushambulia

Kuna watu sehemu fulani, mahali fulani humu! niliwauliza kuwa tatizo la CCM ni kuwa kina wafanyabiahsara walio kwenye position kubwa kisiasa na hivyo wanajisukumia tenda na ku-influence decision kwenye kila kitu

Nikauliza, Mbowe ni mfanyabiashara, Ndesamburo au Komu...Je wakishika nchi, say Slaa ni rais Mbowe ni waziri mkuu

Mechanism gani au kitu gani kitafanyika kuzuia wafanyabiashara hawa wasifanye yale yale ya CCM given lawas and regulations will still be there before them to change!!

Hili swali nikiuliza.....nitakuwa 'shambolic and incoherent asker''??


Mkuu Wabe si tupo kwenye mchakato wa katiba mpya? Huenda ikawa imetoa mwelekeo kati ya biashara na siasa !
 
Mimi kama Mtanzanaia nataka ufafanuzi(Kama sio ufuatiliaji) wa hizi ahadi za CCM kutoka CHADEMA


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Pamoa na mambo mengi watz wanataka kurejeshewa utu na heshima yao yaani kuheshimiwa kama binadamu. Siyo kuwa kama vibarua wa viongozi wa Serikali. Wawe na sauti juu ya nchi yao. Siyo viongozi tu ndo wenye haki na nchi hii. Hilo nalo ni jambo kubwa sana.
 
Watu wanataka mabadiliko wamechoka na CCM,maisha ya mekuwa magumu na hakun chochote kinachofanywa kutatua haya matatizo,viongozi wapo lakin hawawezi kutokana na mfumo uliopo,Chadema wakiingia madarakani mabadiliko lazima yawepo kwa miaka kadhaa ya mwanzo na wanachi kupata imani hata kama itavulunda huko mbele baada ya kulewa sifa.
 
Mi nitaongelea kwa upande wa wanafunzi.
1. Tunataka mabadiliko ya sera ya elimu hasa ktk baraza la mitihani mabpo kuna ukiritimba na ufisadi mbaya ktk michango ya ada ya mitihani ya taifa especially kwa wadogo zetu wa 4M4, kwani serkali kupitia baraza la mitihani huwa wanakusanya fedha nyingi kwa wale wanaorudia mitihani(private candidates) lakini mwisho wa siku mitihani yao wanaiburuza ktk usahihishaji pasipo kuregard kama hao watu wametoa fedha na kusababisha kuharibia watu matokeo yao maana unakuta kituo cha mtihani chenye wanafunzi 400 unakuta wanafahuru watu 5, sasa hebu ona hapo inamana hao wengine walofeli hawana akili?

MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Maelezo yako MM Mwanakijiji yanareflect majibu yangu kwenye fb wall yako ulipouliza ' Ni mambo gani matano ungependa kuona cdm wanafanya ndani ya siku 100 zao madarakani'?
 
Watanzania wanachotaka kikubwa kwa CHADEMA, kwakuwa kimejipambanua kama chama kinachoweza kukemea na kupinga mfumo wa kifisadi na wenye kuvujisha uchumi wa nchi, haya ndio wanayoyatamani watz!
Lakini sana kabisa ni muhimu kwa watz kuyaendea mabadiliko hayo sababu watakuwa wameutangazia ulimwengu na watawala wengine (hata hao cdm) kuwa mamlaka yote ya nchi inatoka kwa WATU!
Hii itajenga nguvu zaidi kwa UMMA kuwa kumbe inawezekana kuweka utawala na kuuondoa, kutokea hapo tawala zote zitaheshimu watu na zitafanya kwa matakwa ya muafaka wa taifa.
Watu wanakitaka Chadema ili kuonyesha kweli kuwa kuna "peoples' power", kwamba mfumo tuliokuwa nao kwa zaidi miaka 50 umeshindwa hvyo watu wanataka kubadilisha, na keshokutwa wakiona mizinguo wanabadilisha tena.
Hivyo mwaka 2015 ni mwaka wa kuvunja laana ya kuendelea kuamini na kufikiri ndani ya box kwa watz wavuja jasho , damu na machozi.
 
What they want is not neccesary. What they need must come from CHADEMA's party Manifesto (ILANI). Hivyo wananchi wakasome ILANI na SERA za CHADEMA.
Kabisa mkuu katika hilo wanainchi,wanachama na mashabiki wa wa chadema wanatakiwa kuisoma kwa makini na kuielewa na kuitambua ILANI ya chadema.hapo ndipo tutakapo kuwa na wanachama wanaojuwa kuwa chadema kinataka kuwa fanyia nini WATANZNIA.
 
Hili wanalitekeleza vipi? Unaweza vipi kufanya watu waheshimu sheria na taratibu zilizopo.. ?

Hilo watalitekeleza kwa kuwajibika na kuwajibishwa kwa wale wote walio pewa dhamana katika serikali.kwani kwa mfumo wa kutokuwajibishana au kulindana ndio maana watu au viongozi wengi hawaheshimu sheria na taratibu zilizopo.
 
Kubwajinga nature ya kazi yangu unaijua? mimi nipo mapokezi nafanya kazi mpaka pawe na mgeni au simu ikiingia, mda uliobaki nacheza game na kukaa humu Jamvini na hata nikikutwa nacheza game siyo ishu. Ishu nikikutwa kwamba mimi ni mwanajamvi
Ezan,
Hongera sana kwa kuwa na muajiri asiyejali. Ungefanya kazi ofisini kwangu nisingekuruhusu ufanye kitu kingine chochote kisichohusiana na ajira yako wakati wa kazi. Kama kuna gaps nyingi kiasi cha kukupa muda wa kucheza, ni makosa ya hiyo ofisi yenu ya kutokukupatia majukumu ya ziada hata ya kujielimisha. Ningekushauri ujitahidi kusoma vitabu wakati wa ziada utakuwa unafanya kitu cha bora zaidi na ukichagua vitabu vitakavyokuendeleza kikazi ni vizuri zaidi badala ya ku-hang around kwenye mitandao. Jitahidi uwe unabangaiza kwenye mtandao kwenye nyakati mbovu-mbovu baada ya kazi. Good lucky.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom