Swali hili labda ni swali kubwa na la msingi ambalo watu wanahitaji kuona linajibiwa wanavyoona CDM inajipanga kushika madaraka. Haitoshi kuunga mkono CDM kwa sababu ya kuchukia CCM au kutokubaliana na sera za CCM. Watu wanapounga mkono CDM au kujiunga na CDM ni kwa sababu wana matarajio fulani au matumaini fulani. Matumaini hayo yanawafanya wawe tayari kuunga mkono CDM na hata kujitolea kwa mambo mbalimbali. Ni nini basi Watanzania wanataka?
Kisheria: NI sheria gani ambazo CDM itafanyia mabadiliko au inapaswa kufanyia mabadiliko? Yaani, Sheria ambazo CCM imeshindwa kuzifanyia mabadiliko au imefanyia mabadiliko ya juu kwa juu. Au sheria za hivi sasa ndizo zitaendelea kutumika chini ya CDM?
Kimfumo: Mfumo wote wa utawala uliopo sasa umetengenezwa na serikali ya CCM na matokeo yake tunayaona. Je chini ya CDM ni vitu gani vitabadilika? Jeshi la Polisi, Jeshi, usalama, wizara n.k vitakuwaje?
Kuwajibishana: Mojawapo ya matatizo ambayo tunayaona sana - na hasa siku za karibuni - ni jinsi gani CCM iko goigoi katika kuwajibisha serikali yake na hata huko serikalini utamaduni wa kubebana ulivyozoeleka. Je chini ya CDM watu watarajie nini?
Na mambo mengine mengi. Ndio hapa nauliza kwa wale wapenzi na wanachama wa CDM wanatarajia nini kutoka kwa utawala wa CDM tofauti na yale yanayofanywa au kufanyika chini ya utawala wa CCM? Au labda niulize kivingine ; ni mambo gani ambayo ukiyajua sasa kuwa CDM itayatekeleza ikishika madaraka yatakutia hamasa zaidi kuunga mkono, kujiunga au kuwa sehemu ya M4C?
mzee mwana kijiji I salute you!
Kimsingi wanacho takiwa CDM kufanya ni kutulia na kujiandaa ku manage people's expectations! and they are so many!
watu wanatarajia miujiza baada ya CDM kuchukua nchi, na CDM hawajawaanda watu kukubaliana na hali itakavyo kuwa baada ya ya CDM kuchukua nchi! wakati huo huo, haijajulikana CDM iko mrengo gani, kijamaa, kibepari au ukomunisti, dhana ya peoples power, haita-apply kwenye kungoza nchi, ni applicable kwenye pressure groups tu kwa political parties si rahisi ku-work, lazima wasomi wa CDM waanze kuleta maandiko yakionyesha vision na mission yao juu ya Tanzania baada ya CCM, yasiwe ya falsafa ya CDM bali watumie model mbali mbali ili kuunda serkali ya karne hii ya sayansi na Technolojia.
kwa maana hiyo, ni CDM wanapaswa kusoma alama za nyakati na kujianda ili rais wa CDM asije kuwa kama yule wa Madagascar (the former DJ), aliingia madarakani kwa mbwembe kilichofuata baadae ni aibu.
halafu kitu kingine ambacho cdm wanaanza nacho vibaya ni kufikiri watapendwa daima! wajifunze kutokana na makosa ya CCM, hali iliyopo CCM kwa muda huu ni very likely CDM ikafika huko and very soon! why? kwa sababu CDM wana tabia ya kutopenda kukosolewa au kupokea mawazo mbadala (rejea humu JF) na kuamini wako soo perfect! wakumbuke wana CCM ni wabongo, and wana CDM ni wabongo pia! and whatever goes around, very well, comes arround!
so ku, sum up maswali yako, unge ya address moja kwa moja kwa CDM rather than wananchi, and if you ask me, CDM should prepare and be ready to manage the "People's Expectations" after using the People's power to go to Ikulu! and as you and me know, they are a mountain!
I am out.