Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Swali hili labda ni swali kubwa na la msingi ambalo watu wanahitaji kuona linajibiwa wanavyoona CDM inajipanga kushika madaraka. Haitoshi kuunga mkono CDM kwa sababu ya kuchukia CCM au kutokubaliana na sera za CCM. Watu wanapounga mkono CDM au kujiunga na CDM ni kwa sababu wana matarajio fulani au matumaini fulani. Matumaini hayo yanawafanya wawe tayari kuunga mkono CDM na hata kujitolea kwa mambo mbalimbali. Ni nini basi Watanzania wanataka?
Kisheria: NI sheria gani ambazo CDM itafanyia mabadiliko au inapaswa kufanyia mabadiliko? Yaani, Sheria ambazo CCM imeshindwa kuzifanyia mabadiliko au imefanyia mabadiliko ya juu kwa juu. Au sheria za hivi sasa ndizo zitaendelea kutumika chini ya CDM?
Kimfumo: Mfumo wote wa utawala uliopo sasa umetengenezwa na serikali ya CCM na matokeo yake tunayaona. Je chini ya CDM ni vitu gani vitabadilika? Jeshi la Polisi, Jeshi, usalama, wizara n.k vitakuwaje?
Kuwajibishana: Mojawapo ya matatizo ambayo tunayaona sana - na hasa siku za karibuni - ni jinsi gani CCM iko goigoi katika kuwajibisha serikali yake na hata huko serikalini utamaduni wa kubebana ulivyozoeleka. Je chini ya CDM watu watarajie nini?
Na mambo mengine mengi. Ndio hapa nauliza kwa wale wapenzi na wanachama wa CDM wanatarajia nini kutoka kwa utawala wa CDM tofauti na yale yanayofanywa au kufanyika chini ya utawala wa CCM? Au labda niulize kivingine ; ni mambo gani ambayo ukiyajua sasa kuwa CDM itayatekeleza ikishika madaraka yatakutia hamasa zaidi kuunga mkono, kujiunga au kuwa sehemu ya M4C?