Watanzania walioonesha uvumilivu wa kisiasa nchini

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Sisemi kwamba ni wakamilifu, lakini kwa matendo yao, wameonesha kuwa wanao uvumilivu mkubwa wa kisiasa, na hivyo ni sahihi au ilikuwa sahihi kwa wao kushika nafasi kubwa za kisiasa nchini.

Miongoni mwao ni hawa wafuatao:
1. Mzee Ally Hassan Mwinyi

2. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

3. Freeman Aikaeli Mbowe

4. Edward Ngoyai Lowassa

5. Mzee Joseph Warioba

Eleza kwa nini unaamini kuwa watajwa wameonesha uvumilivu wa kisiasa.
 
Na ndio maana kwenye muda wa uongozi wao mambo yalikuwa mteremko mana hawakutaka kuwabana wapigaji ambao ndicho kinakufanya useme hao walikuwa wavumilivu kisiasa
 
Sisemi kwamba ni wakamilifu, lakini kwa matendo yao, wameonesha kuwa wanao uvumilivu mkubwa wa kisiasa, na hivyo ni sahihi au ilikuwa sahihi kwa wao kushika nafasi kubwa za kisiasa nchini...
Hao ni watu, uvumilivu ni usipokuwa na chakula kwa watoto wako, kazi, kwamba wahuni wamekata umeme.
 
Kwa nini Ali Hassan Mwinyi?
1. Alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, askari waliokuwa chini ya Wizara yake wslipotuhumiwa kukiuka haki za binadamu, aliamua kujiuzulu bila kushinikizwa

2. Muda mfupi baada ya kujiuzulu, aliyeteuliwa kuchukua wadhifa aluouacha alimshinikiza kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi bila kuchukua baadhi ya Mali zake halali. Alikuja kurejeshewa baada ya kuwa Rais wa JMT

3. Alipokuwa Rais, hakulipiza kisasi kwa watu waliowahi kumtendea mabaya kabla ya jukwaa Urais

4. Kwa ufupi, ni Rais ambaye hana nongwa na mtu
 
Kwa nini Dr. Jakaya Mrisho Kikwete?

1. Utawala wake ulishuhudia kelele nyingi za ukosoaji bila ya wakosoaji kusulubishwa

2. Kutokana na kupenda kwake Demokrasia, wengine ilifikia hatua wakamwita Rais dhaifu, lakini staili ya aliyemfuatia baada yake iliwafanya watu waukumbuke utawala wake. Ndiye Rais pekee aliyewahi kukaa meza moja na wapinzani Ikulu na kunywa nao juisi

3. Misimamo yake iliendana na moja ya kauli mbinu zake kuwa "hoja haipigwi rungu bali hujibiwa kwa hoja"

4. Uongozi wake ulikubalika ndani na nje ya Tanzania. Kipindi cha utawala wake kilishuhudia viongozi wa mataifa makubwa wakiitembelea Tanzania, mfano George Bush na Barack Obama
 
Kwa nini Freeman Aikaeli Mbowe?

1. Wana CCM huwa hawachoki kumnanga, lakini yeye hana muda wa kuwajibu. Yuko zake busy kukijenga Chama chake

2. Japo amewasaidia wengi kisiasa kwa kuwaibua na kuwajenga hadi wakawa maarufu, walipomsaliti hakusumbuka nao. Kumbuka akina Zitto Kabwe, Profesa Kitila Mkumbo,
Mwita Waitara, Halima Mdee, Esther Bulaya, Mwambie, Dr. Godwin Mollel, Patrobas Katambi, n.k.

Kwa idadi ya watu ambao aliwajenga kisiasa na baadaye kuishia kumsaliti, kama angelikuwa mtu wa kinyongo, "angekonda" sana

3. Ukomavu wake kisiasa umemfanya aheshimike ndani na nje ya Tanzania. Uongozi wake umewavutia watu wa Kanda zote, wakiwemo "maarufu" na "wakubwa" kukubali kujiunga na CHADEMA. Miongoni mwao ni pamoja na Lazaro Nyalandu, Edward Lowassa, Frederick Sumaye, Tundu Lissu, Godless Lema, John Mnyika, Profesa Safari, Juma Duni, Dr. Slaa, n.k.

Hata baadhi yao walipoamua kuondoka CHADEMA hakuwalaumu.

4. Pamoja na kujua kuwa CCM haimpendi na inamtamania mabaya kisiasa, bado alikubali kukaa nao meza Moja kwa ajili ya kutafuta maridhiano ya kisiasa

5. Kwa mafanikio yake ya kisiasa na katika biashara, kama angelikuwa raia wa nchi nyingine kama Marekani, angeweza kutunukiwa Udokta. Watu wenye vipaji wanaheshimika sana huko.
 
Kwa nini Edward Ngoyai Lowassa?

1. Ni mtu asiyekuwa na kinyongo. Kw a jinsi CHADEMA ilivyokuwa ikimpond isingetarajuwa kuwa siku moja angekuna kuwa mmoja wa wanachama wake, lakini sote tulishugudia kilichotokea baada ya CCM kumnyima ridhaa ya kukiwakilisha kwenye mbio za Urais

2. Alimsaidia Kikwete kuupata Urais, lakini baadaye Kikwete akaja kumtosa, lakini bado hakuonesha chukua dhidi yake

3. Ndiye mwanasiasa aliyetukanwa sana Tanzania. Kuna wengine walimtabiria hata kifo ingawa baadhi yao wameishia kufa kabla yake. Hakuonesha chuki kwa waliomkejeli, waliomtukana na hata wdliomtabiria kifo.
• Joseph Msukuma alikuwa mmoja wa wanasiasa wdliokuwa wakimuunga mkono kwenye mbio za Urais, lakini baadaye alimgeuka na kuanza kumshushia matusi yasiyomithilika

• Nape alimwita oil chafu

• Wana CHADEMA walimwita majina mbalimbali: fisadi, mwizi, kibaka, n.k.

Pamoja na yote hayo, yeye hakuuweka "uadui" katika harakati zake za kisiasa.

Huyo ndiye Edward Ngoyai Lowassa, mwanasiasa mwenye uvumilivu wa kisiasa nchini Tanzania.
 
Kwa nini Mzee Joseph Sinde Warioba?

1. Si kwamba ni mvumilivu tu, bali ni mmoja wa watu ambao Tanzania inapaswa kujivunia kuwa nao!

2. Angalia alivyoiongoza tume ya Katiba Mpya. Hakuweka mbele maslahi ya Chama cho chote bali ya nchi

3. Ni mtu anayejiamini na kuisimamia kile anachokiamini hata kama atapingwa. Hata akipingwa yeye hawakasirikii wanaompinga

4. Inasemakana wakati mjadala wa Katiba Mpya ulipokuwa umepamba moto, kuna watu walimfanyia fujo lakini yeye hakuhangaika nao

5. Ni msomi mzalendo anayeipenda nchi yake na watu wake bila kujali kama wenyewe wanampenda au la

6. Ni mtu anayefikiria kabla ya kuongea hivyo si mtu wa kukejeli wengine!
 
Kwa nini Ali Hassan Mwinyi?
1. Alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, askari waliokuwa chini ya Wizara yake wslipotuhumiwa kukiuka haki za binadamu, aliamua kujiuzulu bila kushinikizwa

2. Muda mfupi baada ya kujiuzulu, aliyeteuliwa kuchukua wadhifa aluouacha alimshinikiza kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi bila kuchukua baadhi ya Mali zake halali. Alikuja kurejeshewa baada ya kuwa Rais wa JMT

3. Alipokuwa Rais, hakulipiza kisasi kwa watu waliowahi kumtendea mabaya kabla ya jukwaa Urais

4. Kwa ufupi, ni Rais ambaye hana nongwa na mtu
Mara nyingi( viongozi wa kiislam) are relatively Good as compared to Others.

Mimi sio Mdini
Cc Faiza Fix
 
Sisemi kwamba ni wakamilifu, lakini kwa matendo yao, wameonesha kuwa wanao uvumilivu mkubwa wa kisiasa, na hivyo ni sahihi au ilikuwa sahihi kwa wao kushika nafasi kubwa za kisiasa nchini.

Miongoni mwao ni hawa wafuatao:
1. Mzee Ally Hassan Mwinyi

2. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

3. Freeman Aikaeli Mbowe

4. Edward Ngoyai Lowassa

5. Mzee Joseph Warioba

Eleza kwa nini unaamini kuwa watajwa wameonesha uvumilivu wa kisiasa.
Hao ndio mababa wa Taifa hili!
 
Kwa nini Dr. Jakaya Mrisho Kikwete?

1. Utawala wake ulishuhudia kelele nyingi za ukosoaji bila ya wakosoaji kusulubishwa

2. Kutokana na kupenda kwake Demokrasia, wengine ilifikia hatua wakamwita Rais dhaifu, lakini staili ya aliyemfuatia baada yake iliwafanya watu waukumbuke utawala wake. Ndiye Rais pekee aliyewahi kukaa meza moja na wapinzani Ikulu na kunywa nao juisi

3. Misimamo yake iliendana na moja ya kauli mbinu zake kuwa "hoja haipigwi rungu bali hujibiwa kwa hoja"

4. Uongozi wake ulikubalika ndani na nje ya Tanzania. Kipindi cha utawala wake kilishuhudia viongozi wa mataifa makubwa wakiitembelea Tanzania, mfano George Bush na Barack Obama
Ya Dr Ulimboka kung'olewa meno umeyasahau?

Vipi kuhusu ya Mwangosi Daudi
 
Ya Dr Ulimboka kung'olewa meno umeyasahau?

Vipi kuhusu ya Mwangosi Daudi
Ya Dr Ulimboka sifahamu saaana japo iliongelewa sana, labda niseme sijafuatilia kiviile!

Ya Daudi Mwangosi inawezekana ni ajali iliyotokana na viongozi wa Mkoa.

Isitoshe, sijasema ni mkamilifu, lakini ukiwalinganisha na wenzake wengi, utaona yeye kaonesha ukomavu kwa kiasi kikubwa.

Unajua Urais ni mamlaka makubwa sana, kujizuia kutokutumia vibaya si kazi rahisi pia. Mzee Kikwete anastahili pongezi kwenye eneo la uvumilivu wa kisiasa.
 
Lissu ayupo listed

Pamoja na kupgw lisasi zote akapamban uhai wake bado yupo kwenye uliko wa siasa , Huwez muacha Huyu mtu
Sijawataja wote mkuu!

Ndiyo maana hujawaona akina Amani Abeid Karume na Salim Ahmed Salim, watu ambao naamini nao ni viongozi "wastaarabu"
 
Back
Top Bottom