CHADEMA bado sana kufikia daraja iliyopo CCM mioyoni mwa watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu Watanzania,

Daraja na hatua iliyopo CCM Kisiasa kwa sasa hakuna chama kilichofikia wala kukaribia,Ni kama vile CCM inacheza uwanja wake na ligi yake ya pekee yake ambayo kwa vyama vilivyopo hapa nchini bado havijafikia hatua hiyo na kufuzu.ndio maana ni makosa makubwa sana kuifananisha CCM na vyama vilivyopo hapa nchini kwa vigezo na ufananisho wa aina yoyote ile.

Hii ndio sababu wakati vyama kama CHADEMA vikienda na kupita kwa wananchi kujitambulisha. Hali ni tofauti kwa upande wa CCM, Maana CCM iwapo au viongozi wa CCM wawapo unaona watu wakiwa na furaha, matumaini,faraja, Tabasamu na Shauku ya hali ya juu sana kusikia neno kutoka kwa viongozi wa CCM.kwa kuwa watanzania wanatambua ya kuwa palipo na CCM ndipo penye majibu ya kero zao,ndipo penye suluhu ya changamoto zao,ndipo penye matumaini ya maisha yao. Wanafahamu kuwa CCM inatoa majibu ya uhalisia na siyo malalamiko .

Ndio maana viongozi wa CCM wawapo majukwaani hujikita katika kutoa majibu,kueleza mikakati na mipango ya serikali yao juu ya miradi mbalimbali inayokwenda kufanyika katika maeneo yao,hueleza juu ya fedha zinazokwenda kupelekwa katika kutatua na kumaliza kero fulani. Huwezi ukasikia viongozi wa CCM wakitukana au kulalamika au kuongea vitu bila suluhisho.wakati upande wa CHADEMA wao hujikita katika kushambulia kwa matusi, ubaguzi, uchochezi,lawama pasipo majibu wala suluhisho wala kueleza njia mbadala wa nini wangefanya au nini kifanyike.

Lakini pia mfumo mzima na Taswira nzima ya kiuongozi ndani ya CCM ni yenye kuleta matumaini kwa watu.ukiitazama CCM unaona kuwa hakuna aliye mkubwa ndani ya chama na aliye juu ya chama,kila mtu ana sauti sawa ndani ya chama na mawazo yake yanaheshimika na kuheshimiwa.ndio maana imesheheni wanachama wazito wenye kuheshimika ndani na nje ya chama. Wenye ushawishi na ujenzi wa hoja wenye kukubalika na kuaminika sana katika Taasisi,jumuiya,vyama na makundi mbalimbali.

Sasa chama kama chadema ukikitizama ni kama kimejengwa kumzunguka mtu mmoja au wawili na familia zao na watu wao wa karibu tu. Mfano leo mh mbowe akiugua unaona na chama nacho kinaenda hospitalini. Embu niambieni nani leo hii unaweza kusema ni mbadala wa mbowe pale CHADEMA? Nitajieni huyo mtu ni nani? Mwenye uwezo wa kuzungumza akasikilizwa na wanachama wote,akawa na uwezo wa kukiunganisha chama na kikawa kimoja? Nani huyo? Yupo wapi? Mnakumbuka kipindi mbowe yupo mahabusu?

Mnakumbuka namna chama kilivyopalanganyika? Mnakumbuka kila mtu kuanzia Lema, Lissu, Mnyika, Msigwa, Heche, Sugu kila mtu alikuwa na msimamo wake? Nani kati yao aliyekuwa akizungumza kama kiongozi? Nani kati yao ambaye alizungumza na chama kikamfuata? Nani ambaye alizungumza kati yao na kauli yake ikawa ya chama chote? Mnakumbuka mambo ya chama yalikuwa yanazungumzwa Twitter na space za akina Maria Sarungi?

Mmesahau kuwa chama kilipata msimamo na muelekeo mpaka mh mbowe alipotoka ndani na kuzungumza na wanachama wake? Sasa nani ni mbadala wake huyu ? Nani wa kuvaa viatu vyake ndani ya siasa za upinzani hasa CHADEMA? Sasa nani na mtanzania gani anayeweza kukiamini chama hiki chenye safu finyu na nyembamba ya uongozi? Nani akiamini chama ambacho hakiwezi kuandaa hata mgombea urais tu? Nani mwenye kukiamini chama ambacho kinaweza kuhubiri leo hiki na kesho kikayakana matamshi yake?

Embu niambieni watanzania wenzangu hivi nani wazee wa CHADEMA? Wapo wapi hao wazee ambao wakizungumza wanaweza hata kusikilizwa na vijana watovu wa nidhamu kama akina Mdude CHADEMA? Wapi waliko? Hii ndio maana unaweza ukaona vijana ndani ya chama hiki hawana adabu wala hekima wala staha wala uvumilivu wala mchujo wa maneno na matamshi yao.hii ni kwasababu wamekosa walezi wanaoweza wakazungumza na kusikilizwa,hawana wazee wanaoweza wafunda adabu,hawana watu wazima huko wala wenye kuwalea,kuwakuza na kuwaongoza mpaka wakue,hivyo hukua tu kila mtu kivyake tu.

Lakini ukija CCM unaona wazee kama akina mzee Jakaya Mrisho Kikwete,akina mzee Sinde warioba au mzee Lowassa au mzee mizengo Kayanza pinda au Dr Asha Rose migiro na wengine wengi sana ambao wanaheshimika sana ndani na nje ya chama. Hii ndio maana ya kusema chama kinacholeta matumaini kwa watu na kuungwa mkono na kukubalika kwa wananchi wa makundi yote.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Naona umekuja baada ya kutajwa kwenye uzi wa Mzee Msuya
 
Mimi huyu kijana ananiachaga hoi kwa kudhihirishaga ufinyu wake wa fikra humu jukwaani na mwisho kabisa anaweka/anaambatanisha na jina lake kamili pamoja na nambari ya simu.

Hii yote kwa mwenye fikra pana anaona ni walewale tu... kelele nyiiingi kumbe una targets zako unajidanganya kwamba utatafutwa upewe angalau kanafasi ka kupatia ugali.

Kalagabaho 🤣

Unaendelea kuonesha wazi kwamba CCM ni wachumia tumbo sio wazalendo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Daraja na hatua iliyopo CCM Kisiasa kwa sasa hakuna chama kilichofikia wala kukaribia,Ni kama vile CCM inacheza uwanja wake na ligi yake ya pekee yake ambayo kwa vyama vilivyopo hapa nchini bado havijafikia hatua hiyo na kufuzu...
Chadema hawawezi kuifikia CCM hata kidogo.

Ushawahi kuzisikia sera za chadema?

Mie sijawahi.
 
Back
Top Bottom