MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
Na Mwandishi Wetu, Iringa
Nawahakikishia kuwa Wakenya wanazungumza Kiingereza cha kienyeji, lakini sisi Watanzania tunazungumza Kiingereza cha Oxford (Uingereza), alisema Dk. Kamala na kushangiliwa.
Alisisitiza kuwa, Watanzania wanapaswa kujifunza somo la Maendeleo ya Jamii (Development Studies), Mawasiliano ya Umma (Communication Skills), Maadili (Ethics) na Technolojia ya Mawasiliano ya Umma (ICT) kwa nia ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kiushindani.
nakubaliana na maoni yakoo..Nakaubaliana naye kuhusu Kiingereza kama Wakenya wanavyokubaliana kuwa ati Watanzania ni wavivu! Ukimkuta Mtanzania anaongea Kiingereza huwa kimenyooka kuliko jirani zetu ambao wengi wanaijua lugha hiyo laikin wameelemewa na lafudhi za lugha zao. 'Generalisation' hata hivyo sio kigezo kizuri kufanyia maamuzi.
Masomo yote aliyoyataja ni muhimu kuliko Watanzania wengi wanavyodanganyika kuwa ati Kiingereza kikiendelea kuwa lugha ya kufundishia mashuleni na vyuoni kitawasaidia sana Watanzania katika anga za kimataifa. Ujuzi ndio utakaotufikisha hapo na ikumbukwe kuwa ujuzi hauna lugha, angalia Wajapani, Wajerumani na Wachina walipofikia ingawa wengi wao hawazungumzi Kiingereza...

I agree with some of the things this guy has said. Tanzanians shouldn't be scared to compete and have more confidence with themselves. Some parts I don't agree with is e.g Tanzanians(I'm assuming he meant the majority) speak English from Oxford. Smatta my Kenyan bro, I am more curious to hear your opinions on this. I'm sure this is one piece both me and you will agree upon.
...waahhh!!!...No comment.Kwani Watz wanawaogopa Wakenya??
hakuna mtanzania mwenye akili timamu anaye waogopa wakenya au challenge kwa jumla, tatizo letu ni kuwa na viongozi wabovu ambao wana kutupa sehemu huna nyenzo wakati mwenzako anakianzio, hivyo huwezi kushindana nae, mfano elimu unaweza kuwa nayo lakini hakuna mikopo kama kianzio cha maisha au vitu vya msingi katika maisha, hata mishahara wanayo lipwa watanzania wengi ni midogo kulinganisha na mkenya , kwa nafasi hiyo hiyo, sasa mtu wanamna hiyo anaweza kuwa na confidence zaidi na utulivu wa kiakili katika kutekeleza majukumu yake, lakini mtanzania anayelipwa kiduchu anafikiria namna gani atapata mlo wake au atamsaidia namna gani wazazi wake au ndugu etc etc. tukiacha utekelezaji mbovu wa sera zetu , hakuna kipingamizi, mfano aina ya walimu wengi hapa kwetu ni chini ya kiwango , hivyo hata wanafunzi matokeo ni mabaya, mtu akitaka kujenga nyumba hakuna mikopo hivyo mpaka ukaibe, uchumi wetu ume duma hivyo hata hizo nafasi za kazi ni chache, ukipata hiyo kazi hakuna professionalism katika mashirika yetu, mtu moja anahodhi karibu kila kitu unabaki kama robot ya majamaa, matokeo yake kila kitu kinaduma, mfano mwingine hapa miaka ya karibuni ntulibinafsisha mashirika ya umma, badala ya kuwauzia watu wenye uwezo tukawauzia wasio na uwezo matokeo yake ni kuduma kwa uchumi. in short misingi yetu ya kiuchumi haiwasaidi wananchi kwa hiyo integration. labda ya kuwa manamba au wasindikizajiNa Mwandishi Wetu, Iringa
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, amewataka wasomi nchini kujiamini na kujiandaa kufanya kazi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Dk. Kamala alitoa kauli hiyo juzi katika Chuo Kikuu cha Tumaini mjini Iringa, wakati akizindua maonyesho ya Siku ya Waajiri Kukutana na Wahitimu Tarajiwa (Careers Day).
Alisema, mwakani milango ya soko la pamoja katika EAC itafunguliwa, hivyo Watanzania wanapaswa kujiandaa kwa ushindani.
Alisema, Watanzania wanayo maarifa ya kutosha, hivyo hawapaswi kuwa na wasiwasi juu ya kinachodaiwa kuwa Wakenya wanafahamu Kiingereza vyema kuliko Watanzania.
"Nawahakikishia kuwa Wakenya wanazungumza Kiingereza cha kienyeji, lakini sisi Watanzania tunazungumza Kiingereza cha Oxford (Uingereza)," alisema Dk. Kamala na kushangiliwa.
Alisisitiza kuwa, Watanzania wanapaswa kujifunza somo la Maendeleo ya Jamii (Development Studies), Mawasiliano ya Umma (Communication Skills), Maadili (Ethics) na Technolojia ya Mawasiliano ya Umma (ICT) kwa nia ya kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kiushindani.
Alionya kuwa, wakati umefika kwa Watanzania kuanza kujifunza Kifaransa, kwani soko likifunguliwa nchi za Rwanda na Burundi zinazungumza Kifaransa, lakini zinajifunza Kiingereza kwa kasi kubwa, hivyo kama Watanzania watakuwa hawajui Kifaransa, itawawia vigumu kufanya kazi katika nchi hizo.
Waziri huyo alisema, faida za kuingia katika soko la Afrika Mashariki ni nyingi, kwani ukubwa wa soko utapanuka na gharama za uzalisjaji zinazidi kupungua.
Alitoa mfano wa mauzo ya Tanzania kwenda Kenya kuwa, tangu ushuru wa pamoja uanze kutekelezwa 2007, Tanzania imeongeza mauzo nchini humo kutoka wastani wa Sh bilioni 94.5 kufikia Sh bilioni 275.5.
Dk. Kamala alizitaka nchi wanachama wa Afrika Mashariki kuruhusu wananchi wa nchi hizo kufanya kazi katika nchi zao, kwa maelezo kuwa Tanzania imeshaonyesha njia.
"Leo hii Tanzania inaajiri wana-Afrika Mashariki wengi kuliko nchi nyingine yoyote, wapo kwenye hoteli na kila mahala," alisema.
Aliongeza kuwa serikali ya Tanzania imejenga misingi mizuri ya uchumi, na hadi sasa imedhibti mfumko wa bei kuliko nchi zote wanachama wa EAC.
"Mfumko wa beki kwa Kenya ni asilimia 26, Rwanda ni asilimi 19, Burundi ni asilimia 19, Uganda ni asilimia 13.4 na Tanzania ni asilimia 13.
Hii inamaanisha kwamba kama kuna mtu anataka kuwekeza dola zake, atanona ni hasara kuwekeza katika hizi nchi nyingine, hivyo atakimbilia Tanzania na ndivyo inavyokuwa," alisema na kushangiliwa.
Chuo Kikuu cha Tumaini kimekuwa cha kwanza kukutanisha waajiri na wahitimu tarajiwa, suala ambalo ni kawaida kwa nchi za Ulaya.
I agree with some of the things this guy has said. Tanzanians shouldn't be scared to compete and have more confidence with themselves. Some parts I don't agree with is e.g Tanzanians(I'm assuming he meant the majority) speak English from Oxford. Smatta my Kenyan bro, I am more curious to hear your opinions on this. I'm sure this is one piece both me and you will agree upon.
Suala hapa si kuwaogopa kwamba wanatisha kielimu na kiujuzi la, jamaaa wamechoka tu.Tunawaogopa kiukabila maana unapofungua milango ya ushindani maanake nasi twende kwao kusaka kazi kitu ambacho kitakua ni njozi hawa jamaa kukupa ajira.
Kuna kipindi serikali ya Botswana ilitangaza ajira za ualimu na walihitaji walimu wa sayansi toka Tanzania na kosa likawa kuipa kampuni ya Kenya kufanya recruitment.Watanzania wengi tena wenye elimu nzuri tu hata hawakujibiwa nini kupata hata interview.
Hivyo kufungua milango na watu ambao hawako fair ni kujidanganya!
wewe ni mkenya au mganda,....Ni kwanini Wakenya na Waganda wanawaoutshine watanzania katika nafasi nzuri za kazi hasa katika mashirika ya kimataifa hata ndani ya Tanzania.
Nafahamu Kugha ya Kiingereza ni moja ya sababu, naomba tujadili sababu nyingine zaidi, na nini watanzania wafanye ili kuwa bora zaidi.
Karibuni
Ni kwanini Wakenya na Waganda wanawaoutshine watanzania katika nafasi nzuri za kazi hasa katika mashirika ya kimataifa hata ndani ya Tanzania.
Nafahamu Kugha ya Kiingereza ni moja ya sababu, naomba tujadili sababu nyingine zaidi, na nini watanzania wafanye ili kuwa bora zaidi.
Karibuni