Uchaguzi 2020 Watanzania, uongozi haujaribiwi. Chagua kwa ajili ya Uhuru na Amani ya Watanzania

Kwa kweli tumejaribu kwa miaka 5 tumeona hasara yake,
Jifunze kuwa mkweli na uache tabia ya kughushi vyeti. Nenda darasani kasome, upimwe kwa mitihani kisha ufaulu ndio Sasa upate cheti na ukaajriwe. Tabia ya kitonga hakibaliki mpaka mbinguni. Wajibika kwanza na kisha hiyo iwajibike kwako. Kinyume chake ni uhuni kwa jina la Haki na Uhuru.
 
Amani ili waendelee kugawana na kujijengea mahekalu kwa damu na jasho la Mwananchi?!
Ulafi wizi na uporaji tu huo..
Zile nyumba zimejengwa kwa kutambua thamani ya mchango wao wakati wa uongozi wao. Ni kama vile ilivyojengwa nyumba ya Baba wa Taifa ya msasani na Butiama, kwa fedha za serikali. Na hiyo haitaathiri mwenendo wa wewe kuacha kulipa Kodi na kutokufanya kazi. Fanya kazi lips Kodi ili kesho kesho kutwa serikali itambue mchango wako nawe ujengewe nyumba. Kumbuka habari za Mzee Jumanne Ngoma na Milioni 100!
 
Jiwe alikuwa hajawahi kuwa hata kiranja wa darasa, hata wa chekechea, leo eti ni Rais......
Tunawataka Ben, Azory, Mawazo, Akwilina and many others...... hatusikii lolote katu
Lakini alikuwa waziri tangu 1995 mpaka 2015 mwaka ambao watanzania walimchagua kuwa Rais wa nchi.
 
Kwa hiyo kwa mawazo yako walioko madarakani wabakie milele? Hao wenyewe waliingia je? Labda angebakia mkoloni tu aliyekuwapo kabla yao?
Suala si hao ndio wabakie madarakani pekee. Suala ni kuwepo kwa amani na utulivu nchini. Kama katika jopo la wagombea uongozi yupo mmoja ambaye atatuhakikishia amani na utulivu nchini haijilishi aliwahi kuwa kiongozi ama la, huyo ndiye atatufaa hasa. Wengine hao wakajaribu kugombea uongozi kwenye mabaa huko.
 
Jiwe alikuwa hajawahi kuwa hata kiranja wa darasa, hata wa chekechea, leo eti ni Rais......
Tunawataka Ben, Azory, Mawazo, Akwilina and many others...... hatusikii lolote katu
Justice for Azory , Ben Saanane!!!! Hawa wana Mkono wa MTU FULANI.

Akwilina ni Mkono wa DED na Hi NOW.

Mawazo kuna Mkono wa Mbunge Fulani.
 
Kagame amewadanganya Sana eti ukiuwa, ukiteka, ukibambika, ukifungia media, ukiwasomesha watu namba utaweza kuwacontrol, hata Nyerere asingekiweza kizazi cha sasa. Aliweza zama za Giza kucontrol watu na sio hiki cha global vision
Usije ukatuambia hata manabii walifanikiwa kwa sababu walikuwa kwenye kipindi cha Giza, hahahahahaha.

Kijana ukishajua kutumia kompyuta na smart phones pamoja na ku-download na ku-upload unajiona upo kwenye zama za Nuru hahahahahaha.

Ni lazima ujue mamlaka huwa yanalindwa kwa mbinu zote na nguvu zote. Na ndio maana serikali zote Dunia Zina Majeshi na vitengo vya usalama wa Siri. Nenda kamuulize Yericko Nyerere, atakupa darasa zuri juu ya jambo hilo. Mtu yeyote anayetaka kuharibu amani ya nchi ni muharifu wa sheria, naye atawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
Mlisema magu amewafanyia watanzania mambo makubwa sana kuliko raisi yoyote, hivyo atapata kura nyingi hamna haja ya kutumia nguvu kubwa, na upinzani Tanzania ulikwisha kufa.
Kulikoni tena mnakosa usingizi?
 
Attachments

  • EkngmJ1XYAEahup.jpeg
    EkngmJ1XYAEahup.jpeg
    43.2 KB · Views: 1
Watz kwa pamoja tumeshaamua kuwajaribu chadema na lissu, msimamo wetu ni huo wala hatuyumbishwi kura zetu zote ni kwa lissu tu!
 
Mlisema magu amewafanyia watanzania mambo makubwa sana kuliko raisi yoyote, hivyo atapata kura nyingi hamna haja ya kutumia nguvu kubwa, na upinzani Tanzania ulikwisha kufa.
Kulikoni tena mnakosa usingizi?
Hata sasa tunaendelea kusema kuwa nguvu ya shetani haizidi nguvu za Mungu, lakini hatujaacha kukesha kuhubiri juu ya sifa na ukuu wa Mungu. Vivyo hivyo hatutaacha kukesha kuyasema mazuri ya Rais Magufuli, John Pombe dhidi ya Vibaraka wa watu fulani fulani.
 
Mda huu mchache vyama vya upinzani vifanye kazi ya kuwaelimisha wapiga kura wao mgombea wao yupo namba ngapi, wakifika kwenye sanduku wavute pumzi watulie kwanza waisome vizuri karatasi ya kura wajiridhishe kwanza ndipo waweke tik
 
Watz kwa pamoja tumeshaamua kuwajaribu chadema na lissu, msimamo wetu ni huo wala hatuyumbishwi kura zetu zote ni kwa lissu tu!
Kubadili chama sio dhambi nchi zote zilishabadili vyama vyao thus zimeendelea.Nchi sio chama nchi Ni katiba chama chochote chaweza kuongoza nchi kinapoaminiwa na wengi.ccm haina hati miliki ya kuongoza nchi
 
Watz kwa pamoja tumeshaamua kuwajaribu chadema na lissu, msimamo wetu ni huo wala hatuyumbishwi kura zetu zote ni kwa lissu tu!
Ni kweli kuwa wewe na wenzako ninshemu ya watanzania ambao mmeamua kuwajaribu wakina Lissu na CHADEMA. Lakini huna budi kufahamu kuwa amani na utulivu katika nchi huletwa na walio wengi. Watanzania walio wengi kwa idadi wataenda kumpa Rais John Pombe Magufuli miaka mitano Tena ya uongozi.
 
Hakuna raia wa kawaida ambaye anachagua raisi hapa Tanzania, toka wakati wa chama kimoja Hadi wakati huu wa vyama vingi, kuna baadhi ya watu ambao niyo huwachagua wanaowaona kuwa wanafaa kuwa maraisi ikiwa kwa maslahi yao binafsi au maslahi ya genge lao, hivyo huu uchaguzi ni mbinu za kuonyesha ulimwengu kuwa kuna mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, lakini kiukweli ni maigizo.

Hivyo basi tusipotezeane wakati na mali kwa kufanya kitu ambacho tuna uhakika ni maigizo. Tujifunze tuwe wakweli na wenye kuipenda nchi yetu na watu wetu bila kujali tofauti zetu na ikiwezekana basi tuwe na mfumo mwingine kabisa wa kiutawala ambao hautauletea hizi chuki za kijinga na kukoseshana maendeleo kwa kuwa mtu ameamua kutofautiana na wewe kifikra.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mmoja
Tanzania moja
Watanzania wamoja.
 
Zile nyumba zimejengwa kwa kutambua thamani ya mchango wao wakati wa uongozi wao. Ni kama vile ilivyojengwa nyumba ya Baba wa Taifa ya msasani na Butiama, kwa fedha za serikali. Na hiyo haitaathiri mwenendo wa wewe kuacha kulipa Kodi na kutokufanya kazi. Fanya kazi lips Kodi ili kesho kesho kutwa serikali itambue mchango wako nawe ujengewe nyumba. Kumbuka habari za Mzee Jumanne Ngoma na Milioni 100!
Haya tunasubiri wakujengee wewe hayo mahekalu kama yao!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom