Uchaguzi 2020 Watanzania, uongozi haujaribiwi. Chagua kwa ajili ya Uhuru na Amani ya Watanzania

Bandiko refu hili kumbe unamuongelea huyu aliyesukumizwa ili ajiribiwe,anayehubiri utengano kwa watanzania wenzetu ambao hawakuchagua wawakilishi toka chama cha mbogamboga,huyu asiyewapenda watanzania wenzetu mama, dada, shangazi zetu weusi,huyu aliyekuwa na lengo la kuwapiga na kuwaua shangazi zetu wa Ruangwa na mikoa ya kusini kwa ujumla, huyu aliyekula rambirambi zilizotolewa na watanzania na wafariji wengine toka nje ya nchi kwa ajili ya ndugu zetu waliokumbwa na tetemeko la ardhi kagera,nk
 
Habari za muda huu ndugu wanabodi wenzangu? Leo nimerudi tena baada ya takribani siku kadha zilizopita kuwa na majukumu mengine na hasa ya kiuchumi pamoja na ya kisiasa...
Ngonjera hizi wapelekee mbumbumbu sio Watanzania wa leo waliokwisha fumbuka macho. Unasema uongozi haujaribiwi. Je mtu hajawhi kuwa kiongozi ina maana hatakua kiongozi milele? Chama hakijawahi kuongoza serikali, hakitaongoza milele? Munataka muwaaminishe watu ccm itatawala milele? 2015 mliparangana kwny ccm yenu mkatuletea hili jaribio (magufuli) matokeo yake ndo haya.

Rais gani ni mbaguzi mfano wa magufuli? Kauli zake: Ukichagua mpinzani sitawaletea maendeleo, mtalimia meno, mtaishi kama shetani, hao usiwavunjie (nyumba) walinipa kura, msichague wapinzani hata kama wana sifa, serikali yangu haitasomesha wazazi (mabinti wanafunzi waliopata mimba), serikali haitawasaidia chakula kwakua haina shamba, nk.

Mnakua kama mazezeta kumsifu binadamu mpaka mnamlinganisha na Mungu. Kwa neema ya Mungu ametuepusha janga la vovid19, leo mnakuja kumsifu magufuli. Alifanya nini cha maana kwenye hili janga? Nani asijua alikimbia mjini kujificha chato? Unasema tafiti zilizofanywa- nani mwenye uhuru wa kufanya utafiti huru Tanzania ya leo?

Nani asie jua yaliyowapata TWAWEZA baada ya utafiti wao kuonyesha umaarufu wa magufuli umeshuka? Nani asiejua yaliyowapata wakosoji wa magufuli- Ben Saanane, Askofu Niwemugizi, Kabendera, Tundu lissu, etc? Tunataka UHURU HAKI NA MAENDELEO YA WATU. Tuchague madiwani wa CHADEMA, wabunge CHADEMA na MH. TUNDU LISSU RAIS tupate UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU.
 
Amani gani yakuteka watu watukuwekwa kwenye viroba kutufilisi wavuvi hiyo unaita amani hii amani bandia hatutaki amani bandia tunataka mtu ayahemu mawazo na malizetu
Six moth:
Kwanza Pole kwa kuchomewa Moto nyavu zako. Kipindi kabla Rais hajawa John Magufuli. Kulikuwa na matukio makubwa ya kijambazi na uaji. Yapo matukio ya kikatili ya liyohusishwa na imani za kishirika, wivu wa mapenzi pamoja na ujambazi hata kabla ya mwaka 2015.

Baada ya Rais Magufuli kuapishwa, ni kwa miaka 5 Sasa, u shahidi taarifa ya matukio ya kijambazi ya kutumia silaha umepungua kabisa, mauaji kwa sababu za imani ya koshirikina hakuna kabisa n.k ni kwa sababu Rais John Magufuli alijiapiza kushughulika kufa kupona na majambazi hao. Na ndio maana njia zimetumika za kiiinteljensia kuhakikisha hilo limekamilika.

Lakini pia, kwenye uvuvi wa samaki, haimaanishi kwamba wavuvi hawatakuwa kwenye vizazi vyetu vijavyo na kwamba kizazi cha kula samaki ni hiki cha sasa. Kwa jinsi hiyo sio kila wavu ni maalum kwa kazi ya uvuvi, zingine hasifai maana zinaharibu Hadi mazalia ya samaki hivyo kupelekea kupungua kwa idadi ya samaki mwaka hata mwaka. Tukafanye kazi huku tukifikiria kesho yetu ya vizazi vyetu, Kama ambavyo wazee wetu walitufikiria sisi.
 
Hakika ndugu, Mimi ni masikini wa kuamini katika siasa mbovu zenye kuwagawa watu. Utajiri wangu umeegemea katika Imani yangu juu ya kufanya kazi katika amani na utulivu.
Siasa zenye kugawa watu? Za magufuli? Kua maskini wa vitu na maskini wa akili pia ni mzigo sana, nakupa pole sana. Jiwe limewabrainwash mnaamini kila mtu ambaye hampendi ni mleta vurugu, ngoja niongeze ignore list tu sina muda na vilaza
 
Mbona ye mwenyewe alisema amesukumiziwa tu?
Plato aliwahi kutoa ushauri wake katika kitabu chake cha Republic. Kwamba, kazi ya uongozi itakuwa nzuri kwa wanaoongozwa ikiwa kiongozi ni mwanafalsafa. Kwa kuwa wanafalsafa wanaweza kuongozea kwa uzuri sana. Lakini kwa bahati mbaya wanafalsafa wengi hawependi kuongoza.

Kwa hiyo wakati mwingine wanajikuta wanasukumiwa tu. Rais John Magufuli ni mwanafalsafa, mfano mdogo na wa haraka tazama alovyoweza kulivusha taifa kwenye janga kubwa la covid-19. Dunia na Afrika imeshangaa Hadi Bill Gate na mkewe Melinda Gate wameshangaa! Na mwaka huu tutamsukumia Tena Urais kwa kura nyingi za kishindo.
 
Thus tulijaribisha 2015 kuchagua mtu ambae ajawahi ongoza hata watu tumevuna hasara, thus tumeamua kuweka mtu makini atuvushe.Na sio kusomesha watu namba.
 
Jiwe alikuwa hajawahi kuwa hata kiranja wa darasa, hata wa chekechea, leo eti ni Rais......
Tunawataka Ben, Azory, Mawazo, Akwilina and many others...... hatusikii lolote katu
Kuwaletea watu maendeleo sio lazima uwaue sasa ukiwamaliza utaongoza kina nani.
Pili killing people haijawahi silence people thus pamoja na killing, kubambika,utekaji still imeshindwa kulazimisha kupendwa.
 
Masikini wa frika na muoga wa mabadiriko. Alafu kuna watoto wanakuita baba!
Nimejitahidi kukuelewa kiasi. Ni kweli waafrika ni waoga wa mabadiriko, ni kwa sababu hawajayajua hasa yanalengo gani kwao maana ni msamiati mpya.

Lakini waafrika hawahawa wapo tayari kundilika na hawayaogopi mabadiliko. Ambayo yatakuwa na msingi wa kuleta maendeleo ya watu wote na sio kwenye kundi la watu fulani wa nchi.

Waafrika wanataka wafikie uwezo wa kupata huduma za muhimu za jamii uwe no uwezo wa kila mtu. Ikiwa n huduma ya maji safi na salama, elimu Bor, afya bora, lishe bora n.k kama ambavyo yametekelezwa vema na Rais Magufuli kwa miaka mitano ya kwanza. Hakika #MagufuliNiMafanikio.

#magufuli5tena
 
Kagame amewadanganya Sana eti ukiuwa, ukiteka, ukibambika, ukifungia media, ukiwasomesha watu namba utaweza kuwacontrol, hata Nyerere asingekiweza kizazi cha sasa. Aliweza zama za Giza kucontrol watu na sio hiki cha global vision
 
Nilipoona heading imekosa neno "HAKI" nikajua tu hii ni rubbish kutoka viunga vya lumumba.
Watu wa Lumumba wanatambua msingi wa Haki ni usawa kwanza na kisha ndio amani ya nchi. Itakuchukua miaka mingi sana kukubaliana na hili.

Maana kama patakuwa na haki bila usawa usitegemee kama kutakuwa na amani ndugu. Maana haki itasema kila mfanya biashara alipe kodi kiasi fulani, lakini USAWA utasema kila mfanya biashara wa mtaji wa kiasi fulani atalipa Kodi kiasi fulani. Ukishelewa msingi wa usawa juu ya haki ndio utakombolewa kifikra na chaguo lako litakuwa ni CCM karibu sana Lumumba, nyumba ya vijana wasomi waelewa.
 
Chagua : Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu
Ndio uchaguzi mkuu wa kwanza wapinzani hawana tena sera zaidi ya kauli mbiu, ambazo zilitumiwa miaka ya 1960's hahahahaha.

Ngoja nikuambie ndugu, Dunia na Afrika Sasa inafahamu kwa uzuri kuhusu dhana ya Haki, Uhuru na Maendeleo ya watu. Sasa kinachohitajika ni kulipa gharama ili kuweza kutokana kwenye dhana na kwenda kwenye utekelezaji.

Ni wajibu wa watu kufanya kazi. Kazi ndio msingi wa maisha. Maendeleo yataletwa na kazi. Tusiukalie uchumi wetu kwa kujadili habari za "Maendeleo ya watu". Watu ndio sisi, na mendeleo ya watu yataletwa na watu wenyewe. Huku wakifahamu wao ni watu sawa na wenye kuheshimiana. Hivyo watafanya kazi katika hali ya amani na utulivu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom