Hata kama Rais Samia haumkubali, si sahihi kumpuuza na kumwandikia jumbe zisizo na staha

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Umeibuka utamaduni wa wengi pale inapotokea mada imuhusuyo mheshimiwa Rais Samia walio wengi wamekuwa wakimbeza na kujibu yamhusuyo pasi na staha.

Hakika hiyo tabia si ya kiuungwana na sote kwa umoja wetu tuikemee.

Samia ni dada,mama,shangazi lakini pia ni mke.Shime tusiutweze utu wake.

Na hata kama hana uwezo wa kuongoza kama Viongozi wengine waliopata kuwa lakini bado ni kiongozi wetu.

Mungu ibariki Tanzania.

Nb: Gesi ya Mtwara wazungu walishafanyaga yao kitambo!
 
Kwa kweli binafsi siungi mkono tabia hii!!
HAIFAI!!
Ukiona anakosea wapi umetoa ushauri wa kurekebisha??? Tena ushauri wenye staha
 
Na wale waliokuwa wanamuabudu mungu mtu wajue sasa huyo mungu wao ameshakufa na hawezi kurudi tena na wakitaka kulia waende kaburini kwake.
Imesha expire hiyo haiko kwenye chati tena wale waliokuwa wana mdhiaki "mungu wetu" sasa tunaimba nao wimbo mmoja bado wewe ndo hutaki kujifunza na kuelewa ila soon nawe utaunga tera.
 
Kama humkubali ni wewe, Mimi namkubali kabisa, Mtu anayetutawala kufuata sheria na Katiba ndo kipimo cha kiongozi mzuri
Nanukuu maneno ya mwalimu Nyererer : Rais anayetawala bila kufuata katiba hatufai, haatufai kabisaaaa.

Sasa linganisha Mama SAMIA na hilo lipunguani lako nani ametia fora kwa kuvunja katiba?

Labda nikupe mifano michache:

1.Wabunge wa kuteuliwa katiba inasema ana uwezo wa kuteuwa wabunge kumi. Punguani lako halikuteuwa wabunge 11 mpaka lilivyoona limevunja katiba likatengua uteuzi wa Abdalla Possi

2. Hela za kodi zinazokusanywa na hazina matumizi yake yanaidhinishwa na Bunge kwa mjibu wa katiba, Punguani lako halikuwa linazigawa barabarani? Tena mleta mada ukome kabisa mwachae Rais wetu SSH atawale kufuata katiba.
 
Tz

2717833_Tanzia1.png
 
Umeibuka utamaduni wa wengi pale inapotokea mada imuhusuyo mheshimiwa Rais Samia walio wengi wamekuwa wakimbeza na kujibu yamhusuyo pasi na staha.

Hakika hiyo tabia si ya kiuungwana na sote kwa umoja wetu tuikemee.

Samia ni dada,mama,shangazi lakini pia ni mke.Shime tusiutweze utu wake.

Na hata kama hana uwezo wa kuongoza kama Viongozi wengine waliopata kuwa lakini bado ni kiongozi wetu.

Mungu ibariki Tanzania.

Nb: Gesi ya Mtwara wazungu walishafanyaga yao kitambo!
Hakuna aliyekamilika chini ya Jua. Kwa kweli mimi naona Mama anafanya vizuri na kazi zinaonekana kufanyika bila kelele nyingiiii.. swala la machinga limefanyika vizuri sana bila kelele, washirika wetu wa maendeleo wamerudi na tunaona miradi ikitekelezwa kama ilivyopangwa. Ukweli usemwe na unafiki ujitenge..
Kwa hali ya kawaida kila binadamu anatamani kitu flani na sio rahisi kuwaridhisha watu wote kwa wakati mmoja, kwa maana hiyo pia mtu asitegemee mama akaonekana mzuri machoni pa wote. Wapo watakaomuona tofauti tu na ni mitazamao yao.
 
Back
Top Bottom