Waziri Gwajima: Watanzania tuwe Makini na habari za Mtandaoni

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
216
478
Tuwe makini na watu wanaoandaa taarifa za video kama ya huyu anaye 'trend' kwa video ya madai kuwa eti anafanya mapenzi na nyoka Ili kupata hela pamoja na video zingine zenye mlengo aina hii.

Napenda KUIKUMBUSHA jamii kuwa:

Ni kosa la jinai chini ya Kanuni ya Adhabu , Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kuharamisha ngono kinyume na asili au maumbile.

Kifungu cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania S.154 (1) (b) 'Any person who has carnal knowledge of an animal commits an offense, and is liable to imprisonment for life and in any case to imprisonment for a term of not less than thirty years'

Habari tata kama kinyume na sheria zina madhara kwenye jamii ya makundi yote na hasa watoto hivyo, naikumbusha jamii kuwa makini na kuzalisha habari kwa mujibu wa sheria, taratibu. Mhusika wa madai haya vema ujitokeze uombe radhi au ushtakiwe kwa mujibu wa sheria.

Kutunza maadili ya jamii ni jukumu letu wote wanajamii. Kila mwanajamii ahusike na kuzijua sheria na kuzitekeleza.

1715424173381.jpg
 
Tena nashangaa hadi leo hii tarehe 11/5/2024 kwanini hajakamatwa huyo muhuni.
Nashauri mamlaka husika zimkamate haraka na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wahuni wengine.

Kamwe tusiwe na muhali kwa watu wa aina hii ambao wanalenga kuharibu jamii kwa maksudi.

Na huyo nyoka achukuliwe apelekwe maliasili akahifadhiwe.mpuuzi kabisa huyo!!!
 
Media zenyewe nyingi zimejaa waandishi wajinga na wpmbv

Ova
 
Na hiyo media uchwara ichukuliwe hatua, inaacha kwenda kusaka habari za namna wabunge wa CCM kama gwajiboy wanavyotembea kwa miguu nyumba hadi nyumba majimboni kuwalaghai tena wananchi, wao wanakuja na habari za kipuuzi kama hizi!
 
Hata kabla ya mitandao watu walikuwa na midomo hivyo kuweza kutoa kauli yoyote..., Ni jukumu lako wewe unayesikia kutumia akili zako na kichwa chako..., Dunia ya Sasa usiamini lolote hata Propaganda za Serikali nyingi ni uongo...

Hivyo badala ya kupoteza rasilimali fedha na muda kwa kuzunguka na kufunga / kuzima every fake news na click baits ni vema kuwafahamisha watu wasiamini kila wanachokiona au kukisikia....
 
Back
Top Bottom