Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Wakuu kwema?
Nimekutana na video hii mtandaoni, ambako huyu 'kuruta' (kama sijakosea) anapewa amri ya kugeuka kulia na kushoto, kijana huyo anafata maagizo aliyopewa huku anayetoa maagizo na wengine wakisikika wakicheka.
Nini dhumuni la kurekodi video hizi mpaka kufikia hatua ya kuzirusha mtandaoni? Anayerekodiwa ameridhia? Na hii sio mara ya kwanza kukutana na video kama hizi mtandaoni, za hawa wanafunzi wanaokwenda jeshi kwa mujibu wa sheria kurekodiwa katika matukio mbalimbali.
Huu ni udhalilishaji wa utu wake, tayari watu washaanza kutoa maoni mbalimbali juu ya muonekano wake, maumbile na kadhalika, kwa hali tu ya kawaida hakuna mtu angependa kurekodiwa katika hali hiyo na video hiyo irushwe kwa kila mtu kuona.
Hii sio sawa, kwanza ukipewa amri hapo lazima ufate, usipofata ni kukaidi na udhabu unapewa. Kwanini tunahalalisha udhalilishaji huu uendelee kutokea na kuonekana na kawaida? Wanajeshi wapo juu ya Sheria? Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wao haiwahusu?
Aliyechukua video hii awajibishwe, Jeshi kama chombo cha ulinzi wanatakiwa kuwa mfano kwenye kufata sheria na sio kuwa wa kwanza kwenda kinyume na kudhalilisha utu wa watu.
Kutoka kwenye comments za video hiyo anayesikika akitoa amri ni Afande Sese, JKT Oljoro.
Sheria iwe msumeno, sio ikate kwetu tu halafu kwao kuwe butu.