Watanzania tutafute namna bora ya kumtunza Freeman Mbowe

Watanzania tutafute namna bora ya kumtunza Freeman Mbowe

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
17,992
Reaction score
24,901
Watanzania wenzangu Mh. Freeman Mbowe ni hazina kwa taifa letu. Kiongozi huyu wa upinzani Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA ameonesha ujasiri na umahiri mkubwa sana katika kujenga Tanzania yenye uhuru, demokrasia na amani. Freeman Mbowe amekuwa kiongozi mwenye weledi mkubwa na tunashukuru Mungu kwa kipaji chake, Tanzania bado tuna amani na utulivu pamoja na madhila yote aliyotendewa yeye binafsi, familia yake, chama chake na watanzania wenzake.

Mh. Mbowe amekuwa mlinda amani ya nchi yetu kwa busara na uvumilivu wake. Freeman amesimama kidete dhidi ya udhalimu na uonevu hata wakati ule hatari kabisa kwa wana harakati, yaani kipindi cha awamu ya 5. Mbowe amepoteza mengi sana yeye binafsi, amepoteza biashara zake, amepoteza marafiki zake, amepoteza mabilioni. Mbowe angeliweza kubaki nyumbani na kufurahia utajiri wake huku akiwa kada wa CCM. Mbowe amevumilia matusi na kejeli nyingi. Mnakumbuka jinsi kibaraka Sabaya alitumwa kwenda Hai kumtesa Mbowe na wafuasi wake?

Sasa ni kwa namba gani tumwenzi Mh. Freeman Mbowe?
  • Kuamka na kutetea haki za raia
  • Kuunga mkono juhudi za Mbowe na CDM kuleta demokrasia
  • Kujiunga CDM na kuhudhuria mikutano ya chama
  • Kuchagua viongozi na wakilishi kutoka CDM
  • Kukataa dhuluma na uonevu
  • Kuipinga CCM na utendaji wao mbovu wa miaka mingi
Tunampongeza Mh Mbowe kwa hekima na busara kubwa anazoendelea kuonesha katika wakati huu ambapo mikutano ya siasa imerudishwa majukwaani. Mbowe amekuwa mtetezi wa haki yetu ya kujumuika na kujadili mustakabali wa taifa letu. Haikuwa kazi rahisi! Tumuunge mkono Mbowe kwa ukombozi wa Taifa letu. Freeman Mbowe, wewe ndiye mkombozi wa demokrasia ya Tanzania, ni kaka wa taifa letu! Tupo pamoja nawe na viongozi wenzako wenye nia na maono kama yako. Mungu akubariki na kukulinda.
 
Nimekuja kugundua wengi wanaomlaumu Mbowe kwa ile speech yake kwenye ufunguzi wa mikutano ya siasa juzi, ni waoga, wanaoogopa kumpongeza mpinzani kwa kuhofia kwamba umaarufu wa Chadema utashuka.

Hawa bado wachanga wa siasa, wanaodhani hadhi iliyojengwa miaka nenda rudi Chadema, tena Mbowe wanayempinga akiwa miongoni mwa wenyeviti waliochangia, inaweza kushushwa kwa tukio moja la kumpongeza mwenyekiti wa CCM, kwa kuwezesha kufikia maelewano kwenye mazungumzo yao.

Hizi ndio siasa za kuviziana. Mbowe amekomaa sana kwenye siasa zetu, amepitia mazingira tofauti, ana experience, tofauti na wapenzi na wanachama wake wengi hasa mitandaoni, waliokariri harakati bila kujua kutofautisha wakati na mazingira kisiasa.
View attachment 2492530
 
Kuna kuku wa kienyeji wanaofikiri urefu wa pua yao watakupinga. Wanamtaka yule barbaig slaa na msaliti mkubwa. Alishiriki kuutafuta urais maramoja tu akataka watanzania waingie barabarani. Slaa ni hatari!
 
FB_IMG_1589397986327.jpg
Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
 
Kuna kuku wa kienyeji wanaofikiri urefu wa pua yao watakupinga. Wanamtaka yule barbaig slaa na msaliti mkubwa. Alishiriki kuutafuta urais maramoja tu akataka watanzania waingie barabarani. Slaa ni hatari!
Ukombozi ni process na Mbowe anaendesha process hiyo kwa weledi mkubwa!
 
Hongeraa zake kwa kazi yake aliyoitiwa na Mungu.

Kila mtu na ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Watanzania wenzangu Mh. Freeman Mbowe ni hazina kwa taifa letu. Kiongozi huyu wa upinzani Tanzania na mwenyekiti wa CHADEMA ameonesha ujasiri na umahiri mkubwa sana katika kujenga Tanzania yenye uhuru, demokrasia na amani.

Tunampongeza Mh Mbowe kwa hekima na busara kubwa anazoendelea kuonesha katika wakati huu ambapo mikutano ya siasa imerudishwa majukwaani. Mbowe amekuwa mtetezi wa haki yetu ya kujumuika na kujadili mustakabali wa taifa letu. Haikuwa kazi rahisi! Tumuunge mkono Mbowe kwa ukombozi wa Taifa letu. Freeman Mbowe, wewe ndiye mkombozi wa demokrasia ya Tanzania, ni kaka wa taifa letu! Tupo pamoja nawe na viongozi wenzako wenye nia na maono kama yako. Mungu akubariki na kukulinda.
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom