Watanzania tusidanganyike, Mbowe na wenzake hawana cha kupoteza

1472576558426.jpg
 
Ninyi ni watu wa namna gani? Kwa hakika ni watu wa ajabu kabisa. Ufisadi uliokuwa umekithiri miaka ya huko nyuma hamkuona haja ya kuandamana wa kuleta fujo za aina yoyote ile. Leo hii ufisadi umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa ninyi ndiyo mnatoka mafichoni kuwaaminisha watanzania kuwa ninyi ndiyo wazuri. Mliwaaminisha watanzania kuwa EL ni fisadi, alipokuja tu kwenu ghafla mkabadilisha mashairi kuwa huyo si fisadi. Ndiyo maana tunajiuliza kuwa ninyi ni watu wa namna gani?
Ni nani aliyetoa taarifa za Huo ufisadi,ni Magufuli?? Ni change?? Tibaijuka au huyo LOWASA??ni sisi unaotuita wajinga tulipaza sauti,tulifanya mikutano na maandamano,operesheni sangara alifanya nani?? Ni Magu,Ni wewe na babaako?? NI MARA NGAPI CHADEMA WANASEMA LOWASA APELEKWE MAHAKAMANI,NI MARA NGAPI WAMETAKA CHENGE NA MAFISADI WENZIO WOTE WAFUNGWE??? FIKIRI KWA KUTUMIA KICHWA
 
Siku ya September mosi nitaamka Saa NNE asubuhi, napiga mswaki kisha nakunywa chai na mandazi! Alafu naungana na makamanda kufanya usafi! Nchi hii inawenyewe!
Dunia nzima itakuwa Tanzania kushuhudia jinsi jeshi linavyoingia barabarani KUTISHIA RAIS kwa kisingizio cha usafi,ahahahahha hamuwezi kwepa mtego wa CHADEMA hata mmoja,jeshi limeingia chaka
 
Watakaoandama watakua wadanganyika. Mtanzania (awe Mtanganyika au Mazanzibar) hawezi kuandamana kibubusa.
 
Kauli za kutukatisha tamaa hatutazipa nafasi tunafuta uhuru wa pili hauna tofauti na ule aliutafuta nyerere!!
 
Leo nimeona niwaambie ukweli na niwape uhalisia ndugu zangu Watanganyika na wazanzibar,Kuhusu oparesheni UKUTA ya sept mosi.
Mbowe,Lowasa,Lissu,Dtk Mashinji,Pro Safari,Maalim Seif,Sumaye na viongozi wa juu wa CHADEMA na UKAWA hapana cha kupoteza hata wasipoandamana.
Sumaye amekuwa waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa miaka kumi,kama Mali nyingi alizipata kipindi hicho,Sumaye asipoandamana hana cha kupoteza,analipwa asilimia 80 ya mshahara aliokuwa akiupata alipokuwa waziri Mkuu,analindwa na mlinzi wa serikali,ana gari,ana nyumba kama ana watoto basi wapo ulaya

Freeman Mbowe,mbali ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, ni mfanyabiashara mwenye mafanikio yake,anamiliki hoteli,ana biashara zake nyingi halali,ana pesa ya kumtosha yeye na familia yake, ruzuku ya CHADEMA ikikatwa Mbowe hafi njaa,CHADEMA ikifa Mbowe hafi njaa,Kabla baba zetu hawajapata hata mia babake Mbowe alikuwa mtu mkubwa mwenye mafanikio nchi hii.

Edward Lowasa amekuwa serikali karibu miaka 30,anamiliki Ng'ombe wa kutosha,ana shule kubwa za kimataifa,ana his a kampuni kubwa,ameshakuwa waziri Mkuu,kama ana watoto basi watakuwa wanashinda ulaya,ana mlinzi wa serikali,analipwa asilimia 80 ya mshahara,ruzuku ya CHADEMA ikikatwa hafi njaa,CHADEMA ikifa hana shida.

Tundu Lisu,prof safari,Dkt Mashinji,Peter Msigwa,Lema,Sugu wote ni watu wenye mafanikio,wana pesa washajijenga,Ruzuku ya CHADEMA ikikatwa hawafi,CHADEMA ikifa hawafi njaa,Magufuli asipoleta elimu bora watoto wao hawaathiriki,huduma za afya zikiwa mbovu hawateseki wataenda Agha Khan watakuta dawa,wakikamatwa wataweka mawakili watashinda kesi.

Pamoja na yote hayo,mtu anatoka huko anasema maandamano ya UKUTA viongozi, wa CHADEMA watangulie mbele,seriously?? Wasipoandamana wana nini cha kupoteza??

Watu ambao wana maisha yao,siasa ni kwaajili ya kuweka historia tu za maisha yao,ruzuku ya chama ni kwaajili ya kukuza harakati tu,Lowasa anataka urais ili awepo kwenye kitabu cha historia ya nchi,kuwa ashawahi ifanyia kitu nchi yake,Mbowe anapambana kujenga legacy tu CHADEMA siyo kitu kinachofanya aishi,ila yeye anasaidia kufanya CHADEMA iishi.

From no where anatoka mwanaccm mmoja anasema tuache mbowe na lowasa waandamane sababu ndo wafaidi ruzuku ya CHADEMA, mtu huyo alivyo mjinga anadhani CHADEMA ikifa mbowe atakufa njaa.

Watanzania tusiwe wajinga Mbowe hata asipotangulia mbele sept mosi haimuathiri yeye,sisi tunaoathirika na hali ngumu ya maisha,afya mbovu,elimu mbovu,barabara mbovu,mishahara mibovu,kilimo duni,magari hatuna ndo tuna sababu kubwa ya kuandamana,tuna kila sababu ya kumtaka rais afuate katiba, tuna kila sababu ya kutangulia mbele,Tuna kila sababu ya kudai ajira zetu na ndugu zetu,tuna kila sababu ya kumwambia rais hapa unakosea hapa siyo sahihi,hapa rekebisha hapa acha hapa ndiyo.

Mbowe,Lowasa na wenzao hata wakifa leo wametimiza wajibu wakuwaamsha watanzania kudai haki zao na kujitambua,wamefanya kilichowaleta duniani,wameacha legacy.

Mwalimu Nyerere, akiwa mwalimu Pugu Alikuwa akilipwa mshahara,alikuwa na uwezo wa kujimudu maisha yake,lakini wazee wa TANU walipomuomba asimame aungane kutetea watanganyika dhidi ya manyanyaso na Maovu ya mwingereza Nyerere aliwafikiria watanganyika wenzie,unadhani Nyerere angekuwa mbinafsi angekubali kupoteza kazi,kuhatarisha maisha yake wakati anaweza kuepuka..

Wanaharakati kina Durbois,Martin Luther, Mandela hawakua na cha kupoteza,wakoloni walikuwa tayari kuongea nao na kuwapa Mali na vyeo,lakini walisema no na kuendelea na harakati.

Unayejiona unahitaji UKUTA, kwaajili yako,elimu yako,afya yako,mshahara wako,biashara yako na uongozi unaotii na kuheshimu katiba,HAUNA HAJA YA KUMSUBIRI MBOWE,LOWASA,LISU,SUMAYE WATANGULIE KWENYE UKUTA.IT BEGINS WITH YOU
KAMA UNAHISI MBOWE ANAANDAMANA ILI APATE KITU UNAJIDANDANYA MBOWE HANA CHA KUPOTEZA,HATA ASIPOKUWA CHADEMA,ASIPOKUWA MWENYEKITI WA CHAMA,ASIPOGOMBEA UBUNGE,WALA ASIPOTANGUALIA MBELE HANA CHA KUPOTEZA.

MBOWE NA CHADEMA WAMETIMIZA WAJIBU WAO,WAKIFA LEO WAMETIMIZA KILICHOWALETA DUNIANI.WAMETUAMSHA WATANZANIA.

TUACHANE NA PROPAGANDA ZA KUAMBIWA WATANGULIE MBELE,HATA NCHI IKICHAFUKA LEO, WANAOWAAMBIA KINA MBOWE WATANGULIE MBELE,WATAKUWA WA KWANZA KUFICHA FAMILIA ZAO ULAYA

SISI NDIYO TUNAJUKUMU LA KUWALINDA VIONGOZI WETU,TUNAJUKUMU LA KUHAKIKISHA WAPO SALAMA,TUNATAKIWA KUWAJENGEA UKUTA DHIDI YA WATU WANAOWAWINDA,TUNAJUKUMU LA KUWATETEA SIO KUWATUKANA .
THEY STAND FOR US.TUSIMAME NAO


......UKUTA NI UKOMBOZI....
.......UKUTA NI MUHIMU ZAIDI KWA KIPINDI HIKI.....
TUNAHITAJI UKUTA,HATA KAMA SIO WA KINA MBOWE.TUNAHITAJI UKUTA WA KUDAI MASLAHI YETU NA KIZAZI CHETU
.............NIMEMALIZA
Wewe ni mchochezi hatari
 
Wewe ni mchochezi hatari
Sasa maneno kama haya nshawaambia vijana wengi hapa mtaani kwetu,anyway naandika yote haya nikijua nawaudhi watu kibao wakiwamo system,lakini I have nothing to lose,nipo tayari
 
Na hata Mbowe na Lowasa wasipoumia maisha yao hayaharibiki kitu,wewe gamba ndo utaumia kwa ugumu wa maisha, elimu mbovu, afya mbovu,wenzako wana account Dubai, wanasomesha shule bora,wanatibiwa ulaya,kupigwa kwao,kukamatwa,kutukanwa,na wewe kuwadhihaki yote haya ni kutamani na babu yako kijijini aishi kama malaika,sio shetani kama rais wenu anavyosema

Wewe mwenye uheri nitakuja kwako kukuomba msaada! Pole yako sana kama unadhani Lowassa & co. wanatetea maslahi ya babu na bibi yako aliye kijijini kwenu Liwale mpigamiti, Njinjo au Kipatimu! Kama Lowassa alishindwa kukusaidieni when he was in govt system for over 30 yrs, may be he is able to do it now, teh teh teh!
 
Watanzania tutajuta milele tukikubali chadema ipotezwe na polisi kipitia ccm
CHADEMA ilijipoteza yenyewe ilipotupilia mbali hoja ya ufisadi ambayo wananchi wengi tulikuwa tumeshaielewa na kuiunga mkono. Sasa wamegeukia hoja ya udikteta ambayo sijui ni wananchi wangapi wataielewa!
 
Back
Top Bottom