Watanzania tusidanganyike, Mbowe na wenzake hawana cha kupoteza

ila magufuli na kina membe, nyarandu ,kikwete wanavyo vya kupoteza.
 
Rejea mkataba tata wa Nhc na Mbowe hotels waziri wa ardhi akiwa mtetezi wako , Ndio vitu vya kupinga na sio kushadadia, kwani hivyo vitu ndivyo vina dhofisha elimu afya na kuendelea
 
Leo nimeona niwaambie ukweli na niwape uhalisia ndugu zangu Watanganyika na wazanzibar,Kuhusu oparesheni UKUTA ya sept mosi.
Mbowe,Lowasa,Lissu,Dtk Mashinji,Pro Safari,Maalim Seif,Sumaye na viongozi wa juu wa CHADEMA na UKAWA hapana cha kupoteza hata wasipoandamana.
Sumaye amekuwa waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa miaka kumi,kama Mali nyingi alizipata kipindi hicho,Sumaye asipoandamana hana cha kupoteza,analipwa asilimia 80 ya mshahara aliokuwa akiupata alipokuwa waziri Mkuu,analindwa na mlinzi wa serikali,ana gari,ana nyumba kama ana watoto basi wapo ulaya

Freeman Mbowe,mbali ya kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, ni mfanyabiashara mwenye mafanikio yake,anamiliki hoteli,ana biashara zake nyingi halali,ana pesa ya kumtosha yeye na familia yake, ruzuku ya CHADEMA ikikatwa Mbowe hafi njaa,CHADEMA ikifa Mbowe hafi njaa,Kabla baba zetu hawajapata hata mia babake Mbowe alikuwa mtu mkubwa mwenye mafanikio nchi hii.

Edward Lowasa amekuwa serikali karibu miaka 30,anamiliki Ng'ombe wa kutosha,ana shule kubwa za kimataifa,ana his a kampuni kubwa,ameshakuwa waziri Mkuu,kama ana watoto basi watakuwa wanashinda ulaya,ana mlinzi wa serikali,analipwa asilimia 80 ya mshahara,ruzuku ya CHADEMA ikikatwa hafi njaa,CHADEMA ikifa hana shida.

Tundu Lisu,prof safari,Dkt Mashinji,Peter Msigwa,Lema,Sugu wote ni watu wenye mafanikio,wana pesa washajijenga,Ruzuku ya CHADEMA ikikatwa hawafi,CHADEMA ikifa hawafi njaa,Magufuli asipoleta elimu bora watoto wao hawaathiriki,huduma za afya zikiwa mbovu hawateseki wataenda Agha Khan watakuta dawa,wakikamatwa wataweka mawakili watashinda kesi.

Pamoja na yote hayo,mtu anatoka huko anasema maandamano ya UKUTA viongozi, wa CHADEMA watangulie mbele,seriously?? Wasipoandamana wana nini cha kupoteza??

Watu ambao wana maisha yao,siasa ni kwaajili ya kuweka historia tu za maisha yao,ruzuku ya chama ni kwaajili ya kukuza harakati tu,Lowasa anataka urais ili awepo kwenye kitabu cha historia ya nchi,kuwa ashawahi ifanyia kitu nchi yake,Mbowe anapambana kujenga legacy tu CHADEMA siyo kitu kinachofanya aishi,ila yeye anasaidia kufanya CHADEMA iishi.

From no where anatoka mwanaccm mmoja anasema tuache mbowe na lowasa waandamane sababu ndo wafaidi ruzuku ya CHADEMA, mtu huyo alivyo mjinga anadhani CHADEMA ikifa mbowe atakufa njaa.

Watanzania tusiwe wajinga Mbowe hata asipotangulia mbele sept mosi haimuathiri yeye,sisi tunaoathirika na hali ngumu ya maisha,afya mbovu,elimu mbovu,barabara mbovu,mishahara mibovu,kilimo duni,magari hatuna ndo tuna sababu kubwa ya kuandamana,tuna kila sababu ya kumtaka rais afuate katiba, tuna kila sababu ya kutangulia mbele,Tuna kila sababu ya kudai ajira zetu na ndugu zetu,tuna kila sababu ya kumwambia rais hapa unakosea hapa siyo sahihi,hapa rekebisha hapa acha hapa ndiyo.

Mbowe,Lowasa na wenzao hata wakifa leo wametimiza wajibu wakuwaamsha watanzania kudai haki zao na kujitambua,wamefanya kilichowaleta duniani,wameacha legacy.

Mwalimu Nyerere, akiwa mwalimu Pugu Alikuwa akilipwa mshahara,alikuwa na uwezo wa kujimudu maisha yake,lakini wazee wa TANU walipomuomba asimame aungane kutetea watanganyika dhidi ya manyanyaso na Maovu ya mwingereza Nyerere aliwafikiria watanganyika wenzie,unadhani Nyerere angekuwa mbinafsi angekubali kupoteza kazi,kuhatarisha maisha yake wakati anaweza kuepuka..

Wanaharakati kina Durbois,Martin Luther, Mandela hawakua na cha kupoteza,wakoloni walikuwa tayari kuongea nao na kuwapa Mali na vyeo,lakini walisema no na kuendelea na harakati.

Unayejiona unahitaji UKUTA, kwaajili yako,elimu yako,afya yako,mshahara wako,biashara yako na uongozi unaotii na kuheshimu katiba,HAUNA HAJA YA KUMSUBIRI MBOWE,LOWASA,LISU,SUMAYE WATANGULIE KWENYE UKUTA.IT BEGINS WITH YOU
KAMA UNAHISI MBOWE ANAANDAMANA ILI APATE KITU UNAJIDANDANYA MBOWE HANA CHA KUPOTEZA,HATA ASIPOKUWA CHADEMA,ASIPOKUWA MWENYEKITI WA CHAMA,ASIPOGOMBEA UBUNGE,WALA ASIPOTANGUALIA MBELE HANA CHA KUPOTEZA.

MBOWE NA CHADEMA WAMETIMIZA WAJIBU WAO,WAKIFA LEO WAMETIMIZA KILICHOWALETA DUNIANI.WAMETUAMSHA WATANZANIA.

TUACHANE NA PROPAGANDA ZA KUAMBIWA WATANGULIE MBELE,HATA NCHI IKICHAFUKA LEO, WANAOWAAMBIA KINA MBOWE WATANGULIE MBELE,WATAKUWA WA KWANZA KUFICHA FAMILIA ZAO ULAYA

SISI NDIYO TUNAJUKUMU LA KUWALINDA VIONGOZI WETU,TUNAJUKUMU LA KUHAKIKISHA WAPO SALAMA,TUNATAKIWA KUWAJENGEA UKUTA DHIDI YA WATU WANAOWAWINDA,TUNAJUKUMU LA KUWATETEA SIO KUWATUKANA .
THEY STAND FOR US.TUSIMAME NAO


......UKUTA NI UKOMBOZI....
.......UKUTA NI MUHIMU ZAIDI KWA KIPINDI HIKI.....
TUNAHITAJI UKUTA,HATA KAMA SIO WA KINA MBOWE.TUNAHITAJI UKUTA WA KUDAI MASLAHI YETU NA KIZAZI CHETU
.............NIMEMALIZA
UWONGO katika ubora wake. ..utavuna mnayo yapanda. ..mwacheni MWENYE ENZI MUNGU asimame afanye kazi yake!
 
Rejea mkataba tata wa Nhc na Mbowe hotels waziri wa ardhi akiwa mtetezi wako , Ndio vitu vya kupinga na sio kushadadia, kwani hivyo vitu ndivyo vina dhofisha elimu afya na kuendelea
Well said
 
ila magufuli na kina membe, nyarandu ,kikwete wanavyo vya kupoteza.
Wangekuwa na vya kupoteza wasingetunyanyasa,hawana cha kupoteza ndo maana wanafanya wanavyotaka,Wakiamua kukiwasha ulaya kwao ni hapo tu
 
Na hata Mbowe na Lowasa wasipoumia maisha yao hayaharibiki kitu,wewe gamba ndo utaumia kwa ugumu wa maisha, elimu mbovu, afya mbovu,wenzako wana account Dubai, wanasomesha shule bora,wanatibiwa ulaya,kupigwa kwao,kukamatwa,kutukanwa,na wewe kuwadhihaki yote haya ni kutamani na babu yako kijijini aishi kama malaika,sio shetani kama rais wenu anavyosema

Kwa hyo ukiandamana ndio UTAPATA GARI?
Akili ndogo sana hii unayotmia ili unishawishi
 
Ninyi ni watu wa namna gani? Kwa hakika ni watu wa ajabu kabisa. Ufisadi uliokuwa umekithiri miaka ya huko nyuma hamkuona haja ya kuandamana wa kuleta fujo za aina yoyote ile. Leo hii ufisadi umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa ninyi ndiyo mnatoka mafichoni kuwaaminisha watanzania kuwa ninyi ndiyo wazuri. Mliwaaminisha watanzania kuwa EL ni fisadi, alipokuja tu kwenu ghafla mkabadilisha mashairi kuwa huyo si fisadi. Ndiyo maana tunajiuliza kuwa ninyi ni watu wa namna gani?


Hawana Misimamo, ndio maana wana taabika
 
NAFSI yako itakusuta. ...have a nice day my friend
Mimi siyo rafiki yako,sijawahi na sitawahi kuwa na rafiki wa ccm,nachukia ccm kwa moyo mmoja,Natamani nkimuona mwanaccm nimchape hata risasi
 
Kwa hiyo post nzima umeona neno gari tu?? Kweli ukiwa ccm lazima ujitoe akili
Sina chama, na s mfuata mkumbo. Ila najua kusoma , kuandika na kutafakari. Ulitaka nicopy vyote ulvyovsema?

Nmekpa hako ka mfano ka GARI coz mawazo yako unataka UTAFUNIWE na UPEWE.
 
Mimi siyo rafiki yako,sijawahi na sitawahi kuwa na rafiki wa ccm,nachukia ccm kwa moyo mmoja,Natamani nkimuona mwanaccm nimchape hata risasi
Nawaonea huruma family yako.....ubongo mataptap matupu
 
Mwandishi mleta uzi,mbona maelezo "contradictions" sana, msimamo wako ni upi? Mfano wa Nyerere unalinganishaje na genge la wachumia tumbo?
Nilitegemea utashawishi umma kuwapuuza hao uliowataja kwa kuwa wao hawatapoteza chochote hata wewe ukiuwawa kwasababu ya vurugu walizochochea wao, itakula kwako,sababu wao wapo ki maslahi zaidi. Labda kwa mbaaali,ingeleta maana
 
Mimi siyo rafiki yako,sijawahi na sitawahi kuwa na rafiki wa ccm,nachukia ccm kwa moyo mmoja,Natamani nkimuona mwanaccm nimchape hata risasi
hapo ndio unapokosea kila mwanadamu nisawa bila kujali chama kabila jinsia rangi wala hali yake haya mawazo ya vyam yasitufikishe huko watz na wala silazima kuipenda chadema wala ccm wa act nimamuzi ya mtu binafsi
 
Back
Top Bottom