Sheria za miswada ya hati ya dharula bungeni ni tatizo sana,hii nchi inasheria za hovyo sana kama hujui,kunawatu wamenasa mahabusu miaka mitano sasa kwa amri ya hayati hawapelekwi mahakamani kwakuwa wanajuwa wakipelekwa mahakamani watashinda kesi.Sheria ndio inasema hivyo ?
Swali mtajuaje jibu lake ni kupima.Na ndio maana hata kwa Covid watu wakiingia wanapimwa kwanza au angalau kupiga marufuku wasiingie na hata wakiingia kwa njia za panya wakikamatwa hawauwawi hao watu watakamatwa watapimwa kwa lazima kwa gharama zao kisha wanafungwa.Sidhani kama umefikiria kuhusiana na Afya ya watanzania ambayo iko hatarini??
Tutajuaje kama hao wanyama wanafaa kwa matumizi ya binadamu wakati hawajaingizwa kwa kufuata taratibu.
Si umeona Kenya walivyo ban mahindi yetu kwa kigezo cha afya za wananchi wake??
Badala ya kufanyia siasa kila jambo, tumia akili pia.
chukulia ni mtoto wako anachomwa moto utasema mambo ya kizungu? najua utasema mtoto wako ni binadamu ila kumbuka tu hata kifaranga ni kiumbe hai kama mwanao.Najua utasema mbona tunachinja kuku na ngombe jibu ni kwamba mungu alihalalisha tuwatawale lakini sio kuwatesa kwa kuwachoma moto.Huo muda wa kutetea vifaranga nitautoa wap niache kupambana na maisha yangu mzee, maisha yalivyo magumu hivi hizo tabia za kizungu sina maisha yamenipa moyo wa kibedui
Wawapime na kama hawana magonjwa wapige mnada kama mwenye mali hana hela ya Kodi, tuache kutumia nguvu kila siku wakati tunahitaji pesa. Hii hata tukiwachoma haitusaidii kitu. Halafu najiuliza kuna nini Kenya mbona watu wanapenda mbegu ya vifaranga vya huko?
Kuna mahali nilifanya kazi kampuni flani hivi boss wetu alikuwa mzungu sasa mlinzi wake siku moja aliingia nyoka boss akiwa hayupo getini kwake yule mlinzi akamuua.Kwa misifa yake akamchukua hakumzika akaona ili apate misifa ngoja amuweke boss akija amuonyeshe huenda atapewa sifa.Hata km vina magonjwa vinapaswa kukabidhiwa kwa madaktari wa mifugo ili vitibiwe.
Mtu akiugua anauliwa? Inasikitisha sana. Afrika mpaka ifike hatua ya maendeleo itachukumia miaka mingi sana. Njia rahisi wanaona ni kuchoma moto.
Ningekuwa kiongozi mkubwa, huyo jamaa ningemfuta kazi maana hana mchango wwte kwenye jamii.
Tumia akili ya kuzaliwa, sheria siyo amri za MunguKwani Sheria inasemaje kuhusu Hilo ,kwann hawataki kufuata Sheria ?
Unataka tupate mafua ya ndege.....Leo katika taarifa ya habari ya ITV saa 08:00pm wametoa taarifa ya mfanya biashara huko Morogoro kukamatwa na mabox 200 yenye vifaranga vyenye thamani ya TZS 40M vilivyoingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya.
Mwandishi amemhoji mtaalam husika wa serikali Ni nini kitafuata baada ya ukamataji huu, mtaalam akawa na jibu moja tu "Tutaviteketeza kwa mujibu wa sheria"
Ningekuwa mimi ndio nmeulizwa hilo swali ningejibu "Tutachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuvipima kuangalia Kama vimebeba vimelea vya magonjwa then mamlaka husika itaona Ni hatua gani zaidi zichukuliwe baada ya kushauriana.
Hii ni kwa sababu, endapo vitachomwa na ikaja kutthibitika havina magonjwa, kwanza ni kukiuka haki ya ya kuishi kwa viumbe hai, pili kupotezea nchi mapato ambayo yangeweza kupatikana endapo muingizaji angetozwa faini, tatu kupoteza Kodi ya mapato kutoka kwa muingizaji na mwisho wa siku kuua uchumi wa wafanyabiashara.
Kuliko vichomwe Kama itathibitika havina ugonjwa bora vigawiwe bure hata kwenye majeshi yetu kuongeza tija.
Kwa sababu tajwa hapo juu, nawaomba wana jf wote na watanzania kwa ujumla tuungane kwa pamoja kupinga kitendo hichi kisitekelezwa kwa Hawa viumbe hai wenye Tina kubwa kiuchumi.
Roho inaniuma Sana kwa kweli!