Watanzania tunaumwa akili?

Mantz

Member
Aug 6, 2009
97
30
Alianza Babu Loliondo, akafuatia kijana kule Tarakea, kisha mwingine tena Mbeya na sasa kuna mama huko Tabora. Wote hawa wanadai wameoteshwa kutibu magonjwa sugu na zaidi gharama zao (500) na njia yao ya kutibu (kikombe) zinafanana. Sehemu zote hizo watu wanajaa na wanadiriki kutoa ushuhuda kuwa wamepona.

SWALI: Walikuwa wanaumwa nini?

JIBU: .........................................


Mimi nahisi Watanzania tunaumwa akili. Ikitokea mtu yoyote alie eneo la karibu na wewe akasema ameoteshwa kama hao niliowataja hapo juu utakwenda kupata tiba? Unaumwa nini?

Ni hayo tu...
 
ww hujui maradhi ya watanzania??????

zahanati za vijiji hazina dawa

hospitali za wilaya mpaka uwe na rushwa!!!

hizo za rufaaa ndio mpaka umjue dr.
 
Mhh.. Sielwi,

Babu naye; Alisema kuwa anatibu magonjwa sugu matano.

Wateja wakaanza kushuhudia kuwa nguvu zao za kiume zimeboreka.

Babu akasema tena kuwa hata wenye upungufu wa nguvu za kiume nao wanaponeshwa na dawa yake. (Sio wenye upungufu kutokana na kisukari na magonjwa mengine)

Babuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...
 
Wanachoniudhi mimi ni kujifanya ni watu 'spesho'waliotumwa na Mungu badala ya kujitangaza kuwa ni waganga wa kienyeji kama walivyo waganga wengine tuu.
 
itafikia kila mtz ataoteshwa ,watanzania tunashida bwana ,njaa, magonjwa vyote vyetu.
 
Title haiendani na context!

Niseme inatosha kusema/kushauri kwamba watz wawe waangalifu ktk swala hili ya kikombe na matibabu ya magonjwa sugu. Kusema watz tunaumwa akili utakuwa umeenda mbali sana. Kumbuka kwenda kupata kikombe ni personal decisions zianzokuwa influenced na belief (labda ujifunze kuwa maswala ya imani hayaendani na reasoning);and two people are not equal hasa ikizingatiwa kuwa circustances ni tofauti. Ni kutokana na hilo kwako inakuwa aingii akilini kabisa wakati kwa mwingine ni tofauti.

Nimalizie kwa kusema if you think hao watu waonakwenda kwa Babu si viumbe rational kama wewe, think twice.
 
Magonjwa yote hasa hayo yanayosemwa ni sugu lazima yapelekee taztizo la urijari, na mtu ukinywa hiyo dawa na kupata nafuu ni wazi pia eneo hilo litapata ahueni.Hivyo huenda babu alisahau au amejichanganya au vp sijui?.Ngumu kweli kunyoosha mstari wa hii kitu.Vinginevyo mambo haya ni utata mtupu.Oooops......!
 
ww hujui maradhi ya watanzania??????

zahanati za vijiji hazina dawa

hospitali za wilaya mpaka uwe na rushwa!!!

hizo za rufaaa ndio mpaka umjue dr.

ooh yeah!!
ni shida aisee
 
Back
Top Bottom