Watanzania tunanyanyasika malawi!

rudini home, mnafanya nini kwenye kinchi masikini huko,
Jamaa kasema wanafanya biashara. Na biashara haina mipaka. Mbona kuna Wamalawi chungu nzima Bongo na sijawahi kusikia wananyanyaswa? Kuanzia enzi za uhuru Bongo tumekuwa na Wamalawi na wengine wengi tu wameshika nafasi za juu katika serikali zetu. Uwongo?
 
Asanteni sana! Nyumbani tunapenda kuja ila maisha ndo yametuleta huku hata sisi tunapenda tuwe tunaishi nyumbani kwanza me naona kama wanatupa changamoto ili tusijisahau kurudi kwetu, kuna jamaa yetu msukuma wamemkamata na familia yake yote kuanzia mke hadi wototo wamegoma hata kuwaachia watoto!
 
......Poleni sana, kama manyanyasaso yamezidi bora mrudi nyumbani.
 
hiyo hali sio malawi tu, hata ukifika Bot, Swaz, Leso, Nam, RSA wanakuwaga na kampeni maalumu kwa foreignerz, na nchi hizo lazima karatasi zako ziwe sawsawa,
ni hapa bongo tu unakuta mzawa na foreigner wanagombea kazi ambayo hata mzawa anaiweza vizuri
poleni sana waangaikaji, si siasa yetu ndio inayowatesa,
 
Edgartz, poleni sana kwa masahibu hayo!!

Lakini naomba mkumbuke kwamba haya hayatolei malawi tu, bali ni karibu dunia nzima; pia naomba mjiulize swali la msingi!!! why you? are sure kwamba mnafuata taratibu zote za nchi wenyeji?

nina imani kuna wamalawi nao wanasema wananyanyaswa hapa tz lakini si wote! jichunguze upo kundi gani na aina yako ya biashara inakupa taswira ipi kwa wamalawi
 
poleni watanzania mnaonyanyasika huko Malawi. Labda ni wakati mzuri wa kufikiri kurudi nyumbani.
Just a suggestion.
 
Wote waliokamatwa paspot zao ziko vizuri ila wao hawaangalii paspot wakikukuta popote wanakuchukua mbaya zaidi wanawatumia askari wao wanawapiga watu kama majambazi je? Ni haki?
 
Wote waliokamatwa paspot zao ziko vizuri ila wao hawaangalii paspot wakikukuta popote wanakuchukua mbaya zaidi wanawatumia askari wao wanawapiga watu kama majambazi je? Ni haki?
acha kulialia wewe komaa,kama yamekushinda nauli toka malawi hadi tz 30000 haifiki,rudi kwenu.
 
sidhani kama biashara mnayofanya malawi haifanyiki TZ labda ni magendo ndo maana mnakamatwa. Halafu mkae mkijua nchi za watu siyo kama Tanzania wenzenu wana hasira kwa nini mpate mkiwa kwao?
 
Nauli sio tatazo mkuu tatizo jinsi wanavyotunyanyasa wangesema kuwa hawataki wageni basi
 
Hakuna ubalozi huko na nyie watanzania wa huko hamna umoja wenu huo umoja hauna msemaji ? au wewe ndio msemaji ?
 
sidhani kama biashara mnayofanya malawi haifanyiki TZ labda ni magendo ndo maana mnakamatwa. Halafu mkae mkijua nchi za watu siyo kama Tanzania wenzenu wana hasira kwa nini mpate mkiwa kwao?

Biashara tunayofanya ni halali mkuu ila sema hawataki wageni hapo ningekusoma!
 
Hakuna ubalozi huko na nyie watanzania wa huko hamna umoja wenu huo umoja hauna msemaji ? au wewe ndio msemaji ?

Kila sehemu kunakuwa na umoja wa watanzania mfano lilongwe, blantrye, mzuzu kote kuna umoja wa watanzania,
 
Poleni sana ngoja si Jumatatu halafu mwisho wa mwezi naenda Masaki wapo watu wa Malawi kibao!
 
sidhani kama biashara mnayofanya malawi haifanyiki TZ labda ni magendo ndo maana mnakamatwa. Halafu mkae mkijua nchi za watu siyo kama Tanzania wenzenu wana hasira kwa nini mpate mkiwa kwao?
Magezi ushawahi kuishi/kufika nchi nyingine yeyote zaidi ya Tz? kwanini unawahukumu wenzako?

Mimi nishawahi siku moja kunyanyaswa na askari Nairobi, nje ya hotel niliyofikia, nilikuwa ninapunga upepo. Ugenini kuna mambo, wape nguvu wenzio wanatafuta maisha bro!!
 
na nyinyi si mrudi nyumbani mpewe sehemu pale machinga complex mfanye hizo biashara au
 
Back
Top Bottom