Watanzania tumestaarabika au Elimu haijatukomboa?

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,274
21,441
Kuna suali najiuliza kila siku kwa wasomi wetu kwanini tukipata Raisi muumini wa Dini nyingine, upizani wa bila hoja unaanzishwa tena na watu wasomi? Na kiongozi wajuu kupewa majina yanao ishiria ubaguzi wa dini, wakati hi nchi haina udini ukabila ubaguzi wa aina yoyote, muasisi wa nchi hi alipambana sana kukomesha vitendo kama hivyo ila wasomi wetu naona paka sasa hawajaelimika. Ntatoa mifuano michache kuonyeshe jambo nalo ongelea.

1. Zitto kabwe kiongozi wa ACT-Wazalendo, alivo tamka na kuangiza wanachama wake ku support miradi ya serikale yenye manifaa kwa wananchi, ameitwa kila aina ya majina kwamba ni Mdini, ni mnafiki ni CCM B, wakati wa Raisi alio pita watu wengi waliunga mukono jihudi za serikali watu hawakuwasema hivo.

2. Watu wanakuza mfumko wa bei bila hata kuleta takwimu ya vitu mwaka juzi na mwaka hu kwa mfano sukali mwaka juzi ilikua 2700 na bei ndo hiyo hiyo paka leo, ila utasikia maisha magumu ila hao sanaa wakati hao hao ndo walisema vyuma vemekaza kipindi kile na kutulia tu.

3. Utakuta kwenye mitandao ya kijamii hata na watu wenye elimu yao humiita Raisi wetu bibi ushungi jambo linalo ishiria ubaguzi wa Dini, kwanini humiita raisi kwa vazi lake ni kukosa ustarabu.

4. Hoja nyingi za siasa zimebadilika zimekua uzazibari na ubara sio tena ccm na chadema lakini kwanini watu hatujifunzi kwamba hayo mambo ya taturudisha nyuma Raisi tumkosowe kwa hoja sio kwa mihemuko yetu.
 
^Two-tar-6-harabikaje^ :) na kuelimikaje, wakati hata lugha ya taifa tu tunaiguyuguza kama parachichi kwenye blenda? Hapo kweli elimu ^imetukombowa^?
 
Back
Top Bottom