Watanzania tubadilike

Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
630
1,000
Habari Zenu Bandugu,

Naomba niende moja kwa moja kwenye maada.... Vijana wengi au kundi kubwa la vijana hua hatunaamuzi yetu binafsi hasa pale tunapofikisha umri kuanzia miaka 18 na kuendelea maana yangu ni nini?

Yaani unakuta kijana amezaliwa anakuta baba/ mama yeye ni shabiki wa Simba/ yanga nae atakua ivo ivo anashabikia mzazi anaposhabikia.

Baba askari nae mtoto atataka kua askari/ baba mfanyabiashara mtoto nae atataka kufanya biashara mara chache Sana kukuta moto ameenda kinyume na wazazi wanachokifanya labda kwenye Mambo ya taaluma/kusomea.

Sasa ukija kwenye Mambo ya Siasa unakuta baba ni mwana ccm tangu enzi za Tanu mtoto nae atakua ccm bila kujali Wala kitaka kujua ccm imetutoa na kutufikisha wapi.

Ama kakuta baba yake mpinzani basi nae atakua mpinzani milele daima Bila kuhoji au kuona Mambo ambayo yamefanywa chama tawala hata Mambo mazuri yeye atapinga tu mladi upinzani.

Nitoe Rai hasa katika wakati huu wa uchaguzi Mkuu, Wananchi tunatakiwa kusikiliza sera za wagombe wabunge,madiwani na Uraisi Bila kujali Wazazi wako ni Chama gani/pasipo kufata Uchama Ili tusifanye makosa 28oktoba kuchagua viongozi ambao wanataka madaraka ili kujinufaisha wenyewe na watu wao wa karibu.

Tujitahidi 28 octoba kwenda kupiga kura Sio ushabiki wa vyama kumbe upande mwingine huna hata kitambulisho Cha mpiga kura, Jamani Watanzania Tubadilike.

Asanteni.
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,596
2,000
Career development theories hazijatofautiana na watanzania wanavyofanya.Baadhi ya theory zinaeleza kuwa career hurithiwa kitoka wazazi,utamaduni,mazingira nk.

Hivi unafikiri mimi mtoto wa mvuvi ni rahisi kuwa rubani wakati nacheza na nyavu tangu utoto wangu.Kumbuka mungu kagawa karama kwa kila ukoo.

Usolazimushe kuwa daktari wakati asili yenu ni kufuga ng"ombe au ufundi .Kila ukoi una talanta yake ila mfumo was kisakyula unevuruga hizo Atlanta na kulazimisha shule/walimu wakuchagulie talanta ndio maana tunakwenda ili mradi nchi haisongi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom