Watanzania Tuacheni Unafiki!

Omera Yawa

JF-Expert Member
May 5, 2016
882
1,000
Habari zenu wakuu, bila kupoteza muda niende kwenye mada kuna ile dhana ya kuwa marehemu hasemwi vibaya, ila kusemwa vibaya huko hakujafafanuliwa ni kivipi?, kama ni kupakaziwa basi ni sawa ila kama ni ukweli hilo ndio fundisho na litakuwa funzo kwa wengine wenye tabia za kishenzi kama hizo.

Hata tukija kwenye dini tunaona mifano ya kina yuda na farao wote tunawazungumzia kwa matendo yao ili iwe fundisho sio tunawasema bali ndio ukweli, hata tukija kwenye zama hizi za wakina Mobutu, Iddi Amini tunaongelea mabaya yao ili tujifunze.

Hatuhukumu hiyo sio kazi yetu, ila kuuzungumza ukweli hii ni dhahiri haiwezekani kuna watu wamepotezewa ndoto zao, wamebaniwa promo kisa kukataa malipo duni yasiyostahili kutoka kwa beberu mmoja mwenye connection kila kona anayeweza kukuzima kwa ujumbe mmoja tu wa sms, ila leo hii tunamtukuza kwa sifa na mapambio kana kwamba yaliyolalamikiwa miaka na miaka hatujayasikia, alaa!

Yote yawekwe wazi ila busara ni kuzingatia usia thabiti kama ule aliotuachia Baba wa Taifa ambae alitoa mfano akigusia yale yaliyofanyika katika awamu yake kuwa ni mema au ya kijinga, yale ya kijinga hatuna budi kuyakacha na kushika yale mema, vivyo hivyo mfano huu tuuakisi katika maisha ya kawaida,
mema tuyashike na mabaya tuyaache ila kuyazungumzia ni muhimu ili tujue tumeteleza wapi.
Wasalaam
 
dafity

JF-Expert Member
Aug 16, 2008
1,771
2,000
Marehemu MPYA ndio hasemwi vibaya hasa akiwa hajazikwa lakini siku zinavyoenda haiwi shida kuyasema makosa yake ili kujifunza kama mifano uliyotoa ya akina Yuda, Farao, Kaini, Amoni nk.
Habari zenu wakuu, bila kupoteza muda niende kwenye mada kuna ile dhana ya kuwa marehemu hasemwi vibaya, ila kusemwa vibaya huko hakujafafanuliwa ni kivipi?, kama ni kupakaziwa basi ni sawa ila kama ni ukweli hilo ndio fundisho na litakuwa funzo kwa wengine wenye tabia za kishenzi kama hizo.

Hata tukija kwenye dini tunaona mifano ya kina yuda na farao wote tunawazungumzia kwa matendo yao ili iwe fundisho sio tunawasema bali ndio ukweli, hata tukija kwenye zama hizi za wakina Mobutu, Iddi Amini tunaongelea mabaya yao ili tujifunze.

Hatuhukumu hiyo sio kazi yetu, ila kuuzungumza ukweli hii ni dhahiri haiwezekani kuna watu wamepotezewa ndoto zao, wamebaniwa promo kisa kukataa malipo duni yasiyostahili kutoka kwa beberu mmoja mwenye connection kila kona anayeweza kukuzima kwa ujumbe mmoja tu wa sms, ila leo hii tunamtukuza kwa sifa na mapambio kana kwamba yaliyolalamikiwa miaka na miaka hatujayasikia, alaa!

Yote yawekwe wazi ila busara ni kuzingatia usia thabiti kama ule aliotuachia Baba wa Taifa ambae alitoa mfano akigusia yale yaliyofanyika katika awamu yake kuwa ni mema au ya kijinga, yale ya kijinga hatuna budi kuyakacha na kushika yale mema, vivyo hivyo mfano huu tuuakisi katika maisha ya kawaida,
mema tuyashike na mabaya tuyaache ila kuyazungumzia ni muhimu ili tujue tumeteleza wapi.
Wasalaam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Born 2 Be Wild

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,081
2,000
Kama hujui chuki ndo humsogeza mtu kutoka hatua moja mbele, yaani ni kama unaishi msituni halafu hakuna miti, maadui ni wa muhimu katika maisha ndo hutupa challenge ya kupambana na kufikia malengo yetu, adui ni sawa tu na konda wa basi analipeleka gari stendi Dereva anakuja kulichukua.
 
alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
400
500
Habari zenu wakuu, bila kupoteza muda niende kwenye mada kuna ile dhana ya kuwa marehemu hasemwi vibaya, ila kusemwa vibaya huko hakujafafanuliwa ni kivipi?, kama ni kupakaziwa basi ni sawa ila kama ni ukweli hilo ndio fundisho na litakuwa funzo kwa wengine wenye tabia za kishenzi kama hizo.

Hata tukija kwenye dini tunaona mifano ya kina yuda na farao wote tunawazungumzia kwa matendo yao ili iwe fundisho sio tunawasema bali ndio ukweli, hata tukija kwenye zama hizi za wakina Mobutu, Iddi Amini tunaongelea mabaya yao ili tujifunze.

Hatuhukumu hiyo sio kazi yetu, ila kuuzungumza ukweli hii ni dhahiri haiwezekani kuna watu wamepotezewa ndoto zao, wamebaniwa promo kisa kukataa malipo duni yasiyostahili kutoka kwa beberu mmoja mwenye connection kila kona anayeweza kukuzima kwa ujumbe mmoja tu wa sms, ila leo hii tunamtukuza kwa sifa na mapambio kana kwamba yaliyolalamikiwa miaka na miaka hatujayasikia, alaa!

Yote yawekwe wazi ila busara ni kuzingatia usia thabiti kama ule aliotuachia Baba wa Taifa ambae alitoa mfano akigusia yale yaliyofanyika katika awamu yake kuwa ni mema au ya kijinga, yale ya kijinga hatuna budi kuyakacha na kushika yale mema, vivyo hivyo mfano huu tuuakisi katika maisha ya kawaida,
mema tuyashike na mabaya tuyaache ila kuyazungumzia ni muhimu ili tujue tumeteleza wapi.
Wasalaam
Una uhakika na mabaya yasemwayo kuhusu marehemu au ni kupokea tu na kuangalia upande mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom