ERTUGRUL BEY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 11,529
- 21,530
Nimesoma habar ya kujeruhiwa kwa kiongozi mmoja wa dini akiwa anapata kiraji canteen
Na polisi wamedai wamemkata mtuhumiwa tayar ,ina maana uchunguzi unaendelea na bilashaka tutapata majibu hivi karibuni
Kinacho nisikitisha zaidi ni tabia yetu ya kukurupuka na kutoa lawama ambazo hata hazina msingi,ni watu wa kudandia mambo na kwenda nayo kadri ya vile tunavyojisikia
Na ndio maana ni rahisi mno kwa watu kutubadilishia muelekeo kutoka kwenye mambo ya msingi na kutupeleka kujadili jambo ambalo litaletwa mbele yetu maadamu tu tunajua kukurupuka basi hao tunajaa kwenye mfumo
Pamoja na mapungufu ya jeshi la Polisi lakini si sawa kila jambo linalotokea basi lawama wapewe wao tu,je mnamaanisha jeshi la polisi ndio limepanga kujeruhiwa kwa huyo kiongozi wa dini?
Wengine mnaenda mbali zaidi mnampa lawama mama Samia kuwa sijui hafai kuongoza nchi,sasa kwahiyo kwa kila tatizo linalo tokea Raisi anatakiwa kulizuia?
Kwa kila shida inayotolea mama Samia anatakiwa aitabiri mapema na kuizuia isitokee? Jamani mama Samia kama kiongozi mwingine yeyote yule ana mazuri yake na mabaya yake,kwani hakuna mtu aliyekamilika,ila sio sawa na sio haki kila jambo basi apewe yeye lawama
Tijifunze kuwa watulivu na wenye subira tukisubiri mamlaka husika kufanya uchunguzi na kisha kupitia ripoti yao ndio tuweze kujadili na kuchambua habari hiyo
Tabia hii ya kukurupuka sio nzuri kabisa,haina tija wala faida yoyote ile sana sana inaleta chuki na kuondoa umoja kama taifa
Tulaumu pale inapo paswa kulaumu na tupongeze pale inapo paswa kupongeza na kuhoji pale inapopaswa kuhojiwa
Ni hayo tu!