Watanzania tuache kuishi kwa mazoea!

Watanzania tuache kuishi kwa mazoea!

Hii nchi tunavyoishi ni kama vile hakuna mabadiriko!, hata kama yapo basi yanaenda kama kobe kitu ambacho si halali!.

Pesa serikalini zinapigwa lakini bado kuna watu mnaishangilia serikali, badilikeni acheni mazoea hizo ni nguvu zenu zinatumika na wachache!.
Miaka 60 ya uhuru lkn bado wanafunzi wanakaa chini na bado mnaichekea serikali tena mnapiga mapambio na wimbo wenu wa mitano tena!.
Mpaka leo bado watu tunalia umeme na maji haya ni mazoea mabovu sana!, tunavyozidi kuchekea ndio matatizo yanaongezeka!. yani nchi ya kwetu wote lakini tunavyoishi kana kwamba kila mtu atajujua kivyake!.. kuna vitu vya mtu kivyake na kuna vitu vya kijamii sasa vitu vya kijamii havitakiwi kuchekewa hovyo!.

we need to be serious guys!
Mataifa ya wengine wanajiangalia wao kwanza ndo wanaangalia mataifa mengine!. Haiwezekani kila siku tukae tunaishi kwa kutegemea mpaka aje kiongozi mmoja mkali ndo ayakemee haya madudu!, huyo kiongozi mkali hata akija ni ngumu kupambana na majizi yaliyomzunguka yatafanya chochote yampoteze!.

Muhimu ni sisi wenyewe kutokukubali upuuzi,ulaghai, kutochekea mambo ya hovyo, kuhoji nakufatilia kodi zetu hii ni haki yetu maana hatukai bure sisi sio wakimbizi kwenye nchi yetu tuna kila haki, uhuru.. shida tunawaachia wachache.

Kama viongozi na serikali hawataki kubadirika ili kutuletea tija ktk nchi basi kwa pamoja tuwabadirishe wao!, hatuwezi tukakaa tu tunavumilia madudu yanayotuuma kila mahali!..
nchi hii gharama za kila kitu huwa zinapanda hazijawahi kushuka haijalishi uzalishaji umeongezeka ama lah!, huu ni ukiritimba!.

Uhuru tulioupata mwaka 1961, Ulikuwa ni kutukwamua dhidi ya wakoloni ili tujiletee maendeleo yetu binafsi!, sasa uhuru huo kama upo halafu maendeleo hakuna hiyo ni sawa na kuunajisi uhuru huo!.
acheni kubabaika na visukari na chumvi na hizo hamsini, ukipambana vyema ngazi ya uongozi ikakaa katika haki unaweza kuingiza pesa nzuri tu ukaachana na hivyo vikanga vyakupewa kila baada ya miaka mitano!.

Tusiwe mazwazwa yakuchekea vitu vya hovyo, semi za hovyo iwe ni chama chochote cha siasa kikishafikia dola kinatakiwa kiwe serious na matakwa ya nchi na wananchi ni sisi ndo tunaamua kudekeza ama kutodekeza tubadilike!.
Kila mtanzania anawaza na kuwazua jinsi gani atapata Gepu apige pesa lundo aishi maisha ya ndoto zake.

Kila anayepata nafasi ya uwakilishi katika kutenda kazi kwaajili ya watz wengine, anasahau majukumu yake ya msingi yaliyomuweka katika position iyo nae anaanza kutafuta magepu ajinufaishe yeye binafsi.
 
Jana, Lissu alipokamatwa, niliwaeleza vijana wenzangu hali halisi ya jinsi ambavyo wanaofaidika na dhulma wanazuia haki kupatikana.

Wakaniambia wameridhika na haya maisha, bora waishi hivi kuliko wahatarishe maisha yao kupambania haki.

Nadhani watanzania wengi tunawaza hivyo.
 
Na kuna ule ujinga, eti kiongozi anakuja kutembelea eneo lenu na huwa mnapata shida ya usafiri kwa sababu ya barabara mbovu, inaibuka mijitu mijinga kuanza kufukia mashimo ili eti apite pazuri, angetaka kupita pazuri si angetengeneza, tunendekeza ujinga
kwanza kiongozi ndo anatakiwa apitie tafrani ili ajue ana kazi yakufanya!
 
Kwanza jana Mbinga ilibidi wananchi wakatae Lissu kubebwa..yaani napata hasira mimi..hakuna damu za mabadiliko kabisa hii nchi ..kutwa kudanganyana Tz kisiwa cha amani..mbafu
Tz ina safari ndefu sana, kwanza ukitaka umtawale mtu mjinga miaka yake yote, usimpe Elimu iliyo bora. Ndicho kilichofanyika hii nchi. Wengi hawajui kusoma na kuandika. Ubongo wa huyu mtu hauwazi ya maana zaidi ya kula, kuzaliana.

Tunahitaji watu wa kuhoji na kutaka mabafiliko kwenye jamii. Baada ya miaka 62. Leo 2025 bado tunachangishana kujenga matundu ya choo. Ni V8 ngapi hadi Manaibu Waziri wanazo, zinazurura mjini tena Dar wala si Dodoma. Ambazo fedha zake zingejenga hayo?

Hatuna umoja, ila toka mwanzo walivyofanya huo umoja hautakuwepo, wanajua nini kitakachotokea. Mimi nachukia kuona mtu anatumika pakubwa, halafu anaishi maisha hata mbwa ana maisha mazuri. Hakuna ubinadamu kwa viongozi, wao wanajali wao na familia zao basi.
 
Pole mdogo wangu... Bandiko lako ni zuri lakini vijana halisi wa Tanzania itachukua miaka mingi kuelewa wajibu wao katika Taifa.
Wao waambie wajadili na wapambanie
1. Simba na yanga
2.usioe single maza
Usihonge usihudumie
3. Usihangaike kumridhisha mwanamke kitandani kojoa wewe yeye atajijua na kopo lake.
4. Usivumilie mwanamke kama umeoa akizingua mpe taraka watoto lea mwenyewe.
5. Usioe mwanamke maskini na ambae anatokea ukoo maskini.
6. Kataa ndoa ni utapeli
7. Mishangazi inafaa na iliwe pesa zao.
8. Mbinu za kukimbia mizinga
9. Jinsi ya kupata mwanamke au mishangazi mwenye pesa.
10. Ulishawahi kuhongwa na mwanamke nifanyaje niweze kuhongwa!!!

Hayo baba wanayafanyia kazi na wanayapambania mitandaoni na taratibu hizo heka heka wanazileta kwenye maisha halisi.

Sie wanawake tuna vichinjio vyetu tayari kwa kupiga kura,,, tukikutana kwenye malkia wa nguvu, sijui kitcheni party gala, sijui mwanamke chuma kwenye vikao vya mtaa , makanisani, vikao vya shule huko tumejazana wanawake na kampeni zilishaanza kupiga wapiga kura wenye sifa ndio sisi yaani hapo lazima mjae kwenye mfumo wa mitano Tena.

Mabadiliko na uwajibikaji mtausikia kwa traoure.
 
Hayo simba yanga kwangu mimi ni starehe tu sijui wengine wananini mpk wanachukulia serious kiasi chakuteka akili zao!.

Hii nchi inahitaji mabadiliko haswa!
 
wengi walamba hapa hakuna kutegemea celebrity hapa ni sisi wananchi maana ma celebrity wakipewa vitita tu wanaufyata ama wakionywa!, lakini sauti ya wananchi ni kiboko hakuna asieogopa!
Twende kazi tunaanzaje? kenya last yr walianzaje? Walianza kuhamasishana kwa magroups....hii ianze jamani..am In
 
Hayo simba yanga kwangu mimi ni starehe tu sijui wengine wananini mpk wanachukulia serious kiasi chakuteka akili zao!.

Hii nchi inahitaji mabadiliko haswa!
Kwako burudani kwa wengine ni Mila na desturi zisizo takiwa kuvunjwa.
Muhimu elimu kwa umma na kuanzia mtoto akiwa mdogo aelewe nini maana ya uwajibikaji...
Mabadiliko yatakuja lakini si kwa kizazi hiki.
 
Na kuna ule ujinga, eti kiongozi anakuja kutembelea eneo lenu na huwa mnapata shida ya usafiri kwa sababu ya barabara mbovu, inaibuka mijitu mijinga kuanza kufukia mashimo ili eti apite pazuri, angetaka kupita pazuri si angetengeneza, tunendekeza ujinga
Kweli tupu!!👿 wananchi tunadanganywa kwa vitu vidogo inasikitisha sana!!
 
Back
Top Bottom