Watanzania tu wavivu mno!

Tena ni wavivu hata wa kufikiri. Mtu anakuambia mungu yupo. Bila ya kuhoji na kuuliza sababu, unaanza kutangaza uwepo wake

nikiambiwa mungu yupo sina haja yakuuliza kwa ninj niuliza wakati unajiona wewe mwenyewe unajua umeumbwa na mungu unaona mvua zinanyesha nani analeta unaona jua linakwenda kwa wakati wake nani ana fanya hakuona haja ya kuhoji au kuuliza. subiri ukiugua utamjua mungu
 
MTANZANIA MASAA 24 KUZUNGUMZIA MIPIRA YA NJE NA AKIMALIZA HAPO KUZUNGUMZIA MIZIKI YA BONGOFLEVA UDAKU
 
Watanzania ni wavivu kupitiliza na dunia inajua. Fikiria mtu anatoka india anakuja kuanzisha biashara ya urojo na mishkaki anapiga hela sisi tunaishia kucheza pool table na kuiba power window
Wengi wa Wafanyabiashara wa korosho = wageni (si wazawa) kwa miaka watanzania tumebaki kulia lia.
 
We mwenyewe mvivu wa kuandika

Nawaza tu.
 
kuna ulazima wa kuanzisha mafunzo kwa mujibu wa sheria kwa vijana wte wasio na kazi kwenda JKT
Kungewekwa mfumo wa mafunzo ya kijeshi 40% na ujasiriamali kwa vitendo kwa 60%

Yani kila kambi ya mafunzo wa specialise kwenye ujasiriamali fulani mbali na mafunzo ya kijeshi
Mfano ufugaji wa kuku, samaki, ng'ombe
Ushonaji,
Ufundi magari
Kilimo biashara nk
Na haya yafanyike kwa VITENDO wakihusisha chuo cha kilimo SUA
Na wakitoka huko wapatiwe MITAJI kwa vikundi ili wafanye kazi na kufundisha wengine mtaani...hapo ningeona logic

Lakini hii ya sasa unafundishwa kwata na silaha tuuuu... ukirudi mtaani inakusaidia nini?

Yani hakuna uhusiano kati ya unachofundishwa kule na maisha halisi mtaani. Uvumilivu pekee unakusaidia nini kama huna mtaji wala ujuzi na huna pa kuanzia. Unawezaje kusema vijana ni wavivu kwa staili hii?
 
Watanzania ni wavivu kupitiliza na dunia inajua. Fikiria mtu anatoka india anakuja kuanzisha biashara ya urojo na mishkaki anapiga hela sisi tunaishia kucheza pool table na kuiba power window
ila wewe jamaa ni mjinga sana unapojumhisha uvivu wako kuwa sawa na watanzania wengine. Wenzako tuna hustle tunapata pesa, wewe unaleta story za uvivu wa ukoo wako hapa. Siku zingine usijumhishe watanzania wote.
 
Iweje waajiri walazimike kuajiri wageni wakat kazi hizo zinaweza kufanywa na Watanzania?
 
Mvivu Nini mbona povu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…