Watanzania sisi Mungu ametubariki Upole

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,493
8,724
Watanzania ni wapole jamani asikuambie mtu, Mungu katujalia hilo na tumshukuru sana kwa hili.

Tuna upole ule wa kuvuka kiwango cha upole,

Nawaza maneno ya kejele kama ya Mwiguru Nchemba iwe ni nchi nyingine huo moto acha kabisa, sisi sio mara ya kwanza kukejeliwa na Viongozi na kuishia kulalamikia kwenye vijiwe vya kahawa tu.

Angalia hata Wafanya kazi hawajongezewa Mshahara miaka mitano ila wako kimya kabisa wanalalimikia Whatsapp, facebook au kwenye vijiwe vya kahawa,

Nakuhakikishia hata wasipo pewa nyongeza kwa kipindi chote cha utumishi wao hakuna wanacho weza kufanya zaidi ya kulalamikia chini ya kapeti.

Watanzania wanaweza panda basi sit za nyuma na basi ikifika kwenye mizani wanaambiwa njooni mchuchumae huku katikati na kweli wana tii na wamelipa nauli si kwamba ni lift, au wanashushwa kabisa watembee kwa miguu kuvuka mizani,

Au kondakita anaweza ona trafiki mbele kama abiria wamejaa kusimama anawaambia watu wakae wawili wa wili kwa kila sit na abiria hakuna anaye kataa, bali atakataa akiwa ameisha shuka.

Huu upole tulio nao sio wa kawaida jamani ni zaidi ya limbwata.

Haya ya Mwiguru watu wanaandamania Facebook, whatsapp, Insita na kwenye vijiwe vya kahawa,
 
Watanzania ni wapole jamani asikuambie mtu, Mungu katujalia hilo na tumshukuru sana kwa hili.

Tuna upole ule wa kuvuka kiwango cha upole...
Msaada wa bure,hakuna mtu mpole ila wapo wenye hekima,na pia wanavikomo vya uvumilivu,amini usiamini, kwa asili binadamu sio mkatili, ila ukatili hufunzwa na matendo na mambo yanayojiri kwenye jamii inayomzunguka.
 
huu ni ukweli tupu, wobongo tuna uzezeta sana, tunaweza tukanwa tukaishia kwenye utani, angalia ishu ya Miamala ya pesa watu utasikia mama anaupiga mwingi, yaani ujinga mtupu, watu wana dhurumiwa haki zao wako bise na utani,
 
Msaada wa bure,hakuna mtu mpole ila wapo wenye hekima,na pia wanavikomo vya uvumilivu,amini usiamini, kwa asili binadamu soon mkatili, ila ukatili hufunzwa na matendo na mambo yanayojiri kwenye jamii inayomzunguka.
Hahaaa Watanzania ni wapole sana huu ndo ukweli na hii ni faida kubwa mno kwa watawala
 
Populationa kubwa ta Tz iko vijijini, kumobilize watu wafanye physical maandamano ni ngumu sana.

Until urbanization imefikia atleast 60% ya population nzima ndipo upole utakapoisha.
Unforgetable
 
Back
Top Bottom