Watanzania ni Watu wanaopenda habari za Uzushi, Conspiracy theories na udaku

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Kwema Wakuu!

Jadili Chozi la CDF Mstaafu Mabeyo litolee ufafanuzi kana kwamba unajua alichokuwa anafikiri. Fafanua na elezea tabasamu na kila cheki lake na maana iliyojificha. Kwa kina onyesha jinsi body language yake inavyokinzana na anachozungumzia, hakikisha unaeleza uongo mtamumtamu unaopatana na akili za Watanzania kuhusu habari zilizofichwa ambazo watanzania wengi hata kabla hawajaambiwa huwa na hizo habari akilini.

Watanzania wanapenda assumption, imagination, fiction stories, ndio maana ukiwa mbobevu kwenye hayo mambo kwa hapa Tanzania lazima utoboe. Wachungaji wa kileo wengi washasoma saikolojia ya Watanzania, wanasiasa, waganga, biashara ya michezo ya kubahatisha itazidi kustawi na kushamiri kutokana fikra za Watanzania.

Ukishakuwa Star Tanzania ni rahisi kuwaendesha Watanzania vile unavyotaka. Unaweza ukawapa cha kuzungumza wakakizungumza mwezi mzima.

Mange Kimambi, Kigogo kigogo, ni miongoni mwa Watu walioweza kutumia fikra za Watanzania.

Tanzania unaweza ukavaa tuu nguo yenye fuvu la kichwa au pete yenye fuvu la kichwa na ukishakuwa na pesa ya kubadilisha mboga utatungiwa stori za uzushi mara wewe Freemasonry mara sijui kitu gani. Watanzania hawapendi Ukweli. Na ukiwa umesimama mbele ya mtu unayemjua ni Mtanzania hata kama una ukweli wa jambo usimwambie kwa sababu hatakuamini. Mtanzania ni rahisi kuamini uzushi na udaku kuliko kuamini UKWELI.

Hata hivyo haishangazi kwa sababu ukweli mara nyingi(sio zote) Hauna Faida, na Pia ukweli kikawaida unakatili sana. Ukweli ni uhalisia. Na mwanadamu hasa Mtanzania hapendi Uhalisia (ukweli).

Mimi nimemaliza.
 
na hizo ndizo hulka za wabongo maofisini,serikalini,michezoni,siasa mpaka kwenye familia.

kiukweli nilienda nchi flani nikakuta wabongo wanakataana huko,sababu za kukataana wanajuana kwa tabia mbovu upo uwezekano wa kuharibiana maisha huko ughaibuni.
 
'ahh' in SSH voice.

...ndio Dunia ilivyo.

Watanzania ni sehemu ya Dunia hii hii ya Conspiracies na hayo makorokoro mengine.

Ukweli ni Ukweli tu.
 
Interview ya CDF sio ya bahati mbaya. Ni ishara kuwa ukweli utakuwa wazi, utakuja vipande vipande ila naamini mwisho wa siku ABCs zote za kifo cha jiwe na zile siku 3 kabla ya kuapishwa SSH zitakuwa wazi.

Ukweli upi ambao utakuwa Wazi?
Kwa nini unahisi kuna ukweli umefichwa?
 
Interview ya CDF sio ya bahati mbaya. Ni ishara kuwa ukweli utakuwa wazi, utakuja vipande vipande ila naamini mwisho wa siku ABCs zote za kifo cha jiwe na zile siku 3 kabla ya kuapishwa SSH zitakuwa wazi.
yaleyale ya habari za kizushi unayaendeleza
 
Tunapenda sana uzushi uzushi na umbea yani utakuta mtu msomi tena wakiume ila bingwa wa umbea umbea, kina mange na kigogo lazima watoboe nchi hii hata shigongo si alipiyia humo humo hadi akatoboa, kuna watu wanapenda kusikia habari za watu wengine kuliko maisha yao.
 
Kwa hiyo hutaki watanzania watumie bongo zao kufikiri, unataka wawe wazembe tu wanaosubiri kuletewa kila taarifa kama ilivyo?

Hakuna sehemu nimesema sitaki na zitakuja kuwazuia Watu kutumia akili yao.
Ninachoeleza ni jinsi wanavyopenda habari za utunzi, kubuni, utopia, uzushi na udaku.
 
Tunapenda sana uzushi uzushi na umbea yani utakuta mtu msomi tena wakiume ila bingwa wa umbea umbea , kina mange na kigogo lazima watoboe nchi hii hata shigongo si alipiyia humo humo hadi akatoboa, kuna watu wanapenda kusikia habari za watu wengine kuliko maisha yao

Kiini cha habari hizo zijazwe ulaghai na uzushi(chumvi nyingi) ili stori iuze.
 
na hizo ndizo hulka za wabongo maofisini,serikalini,michezoni,siasa mpaka kwenye familia.

kiukweli nilienda nchi flani nikakuta wabongo wanakataana huko,sababu za kukataana wanajuana kwa tabia mbovu upo uwezekano wa kuharibiana maisha huko ughaibuni.

Bongo kuzushiwa stori negative la uongo ni jambo rahisi mno. Huitwa Fitna
 
Back
Top Bottom