BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 5,292
- 11,820
Hapa narejea nukuu ya Mwalimu Nyerere kwamba ujinga ni kipaji kama ufupi na urefu. Ni kama aina fulani ya unyumbu wa kurithi.
Sijaona mashekhe wakiandamana kupinga ripoti ya CAG iliyosheheni ufisadi na ujambazi wa kutisha.
Sijaona makongamano ya mapadri na watawa wenye vilemba wakikemea ufisadi kwa mbwembwe na madaha kama wanavyofanya kwenye kufokea usagaji.
Sijaona mitandao ikifurika kwa mapovu na jazba dhidi ya majizi yanayokwapua pesa ya nchi na kuzitumbua watakavyo.
Humu mitandaoni pamejaa hadithi za kula matunda ya kimaskhara pamoja na mbinu za kutafuna wake za watu bila kukamatwa.
Huwezi kukutana na critical analysis ya taarifa ya CAG. Ni hadithi za papuchi tu na kutafunana.
Watu kama hawa waliojichokea kwenye ujinga na unyumbu, ni haki yao kuibiwa. Sheria ya mwituni lazima itawale ili maandiko yatimie kwamba nyumbu ni halali ya simba.
Magoigoi lazima wadhibitiwe na wenye nguvu. Ni sheria ya asili.