Watanzania ni balaa.

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,637
4,521
Kuna jamaa(watanzania) wafanyabiashara ya madawa ya kulevya katika nchi moja ya ulaya,walikuwa wamepokea mzigo wa kutosha wa madawa hayo katika nyumba ya kiongozi wao.Basi wakawa wamekutana kama wanaume wanane na wanawake sita ili kila mmoja achukue mzigo wa kumtosha aende akauze katika mji anaoishi,wakati wakiendelea na moja moto moja baridi kabla ya makabidhiano,polisi wakawa na taarifa zao na wakapanga mtego ili wakawakamate.
Kwa bahati kijana mmoja akawa amewaona polisi kupitia dirishani,akawaambia wenzake tumekwisha lakini mmoja wao akasema nyie anzeni kulia kila mmoja kwa staili yake kisha mimi nitaongea na polisi.Wale polisi walipofika mahojiano yalikuwa hivi
Polisi: Mbona mnalia?
Jamaa :Tumepokea taarifa ya msiba kutoka kwetu ndio maana tumekusanyika hapa kuomboleza.
Polisi :Lakini mnajua utaratibu wetu kuwa haturuhusu mtu yeyote amsumbue jirani yake kwa kelele.
Jamaa :Sawa tutajitahidi kuomboleza kimyakimya.
Polisi :poleni sana kwa msiba,sisi tunaindoka ila msiwasumbue jirani zenu.
Jamaa :Sawa afande hatutarudia tena.
Basi polisi walipoondoka kilifuatia kicheko na kutawanyika.

This is a true story.
 
mmmhhhhhhh mbona ipo simple hivyo.........polisi wa nnchi gani hao?

maana wale wa kwa ELIZA hawana mchezo....

hata kama mnalia lazima watimize azima yao
 
Kuna jamaa(watanzania) wafanyabiashara ya madawa ya kulevya katika nchi moja ya ulaya,walikuwa wamepokea mzigo wa kutosha wa madawa hayo katika nyumba ya kiongozi wao.Basi wakawa wamekutana kama wanaume wanane na wanawake sita ili kila mmoja achukue mzigo wa kumtosha aende akauze katika mji anaoishi,wakati wakiendelea na moja moto moja baridi kabla ya makabidhiano,polisi wakawa na taarifa zao na wakapanga mtego ili wakawakamate.
Kwa bahati kijana mmoja akawa amewaona polisi kupitia dirishani,akawaambia wenzake tumekwisha lakini mmoja wao akasema nyie anzeni kulia kila mmoja kwa staili yake kisha mimi nitaongea na polisi.Wale polisi walipofika mahojiano yalikuwa hivi
Polisi: Mbona mnalia?
Jamaa :Tumepokea taarifa ya msiba kutoka kwetu ndio maana tumekusanyika hapa kuomboleza.
Polisi :Lakini mnajua utaratibu wetu kuwa haturuhusu mtu yeyote amsumbue jirani yake kwa kelele.
Jamaa :Sawa tutajitahidi kuomboleza kimyakimya.
Polisi :poleni sana kwa msiba,sisi tunaindoka ila msiwasumbue jirani zenu.
Jamaa :Sawa afande hatutarudia tena.
Basi polisi walipoondoka kilifuatia kicheko na kutawanyika.

This is a true story.
Hao ndio wa TZ original,

Ukiendesha bus sehemu haina kibali ukawaambia abiria mapolisi hao anzeni kulia wanalia tena kingoni na kamasi juu!
 
Back
Top Bottom