Umejifunza nini kuhusu Mungu?

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Kwahiyo umejifunza nini kuhusu Mungu?


Mungu ni zaidi ya sisi tunavyomfikiria, huenda mtazamo wetu juu yake haufiki hata theluthi ya uwezo wake halisia.

Powered by #tangaselftour
........................................................................

Ni mara ngapi umepiga goti kwa Mungu, kuomba maombi mengi ambayo mwisho wa siku ulihisi ni kama unanswered cries. Ukimya ulitawala na ukakata tamaa ukahisi hakuna tegemeo tena.

Lakini baadae, mambo yakaenda kama ulivyokuwa umeomba. Ukabaki unashangaa kuona maisha ya ndoto zako yamekuwa uhalisia.

"Mpango ya Mungu ni sahihi sana kuliko mategemeo yetu."

Kuna muda kuchelewa kujibiwa maombi yetu ni faida kwetu, sababu tunapata hamu na kuthamini kile tulichokiomba siku tukikipata.

Anaandika M.J.Ryan kwenye kitabu chake cha Patience. Anasema

"Uvumilivu ni tiba, ni kama kupika chakula tu. Kadri chakula kinavyochelewa kuiva ndio kadri ambavyo njaa inazidi kuuma mwisho wa siku kikiiva unakila kwa adabu na heshima".

Katika maombi yetu tunayoyaomba kwa Mungu, lazima tuweke nafasi kubwa ya uvumilivu. Ni lazima tujitoe mhanga kuwa na subira, na kwenye maisha kama huna uvumilivu wala subira basi huwezi piga hata hatua moja mbele.

Hebu niulize kwanin?

Kwasababu kila kitu kwenye maisha kinahitaji process. Hakuna linalotokea ghafla.

Hata katika uzazi, huwezi kulala na wanawake tisa ndani ya usiku mmoja ili upate mtoto, bali utalala na mwanamke mmoja ndani ya miezi tisa ndio utapata mtoto.

Kila kitu kinahitaji process, sasa wewe binafsi ni lazima ujifunze kuwa na subira ili uendane na process. Hakuna tunda linalokomaa na kuiva ndani ya siku moja. Be, patient

Mungu angekuwa anajibu maombi yetu pale pale tunapomuomba tusingethamini uwezo wake.

Ila kwa vile tunasubiri basi lipo tumaini. Uwezo wake ni mkubwa sana zaidi ya tunavyodhani. Usife moyo, fanya sehemu yako na Mungu nae atatimiza sehemu yake.

"Mkulima humwagilia mti wake kila siku ila matunda huota msimu hadi msimu. Mkulima anafanya sehemu yake, then Mungu nae anatimiza sehemu yake."

Mi nimemaliza ila nakukumbusha tu kuwa Mungu hajaishiwa mbinu juu ya matatizo yako ni kuwa na imani na subira tu.

Na subira ndio kitu kigumu sana kukaa kuki handle sababu siku zote sisi binadamu tumeumbiwa pupa.

Zingatia:
"Jinsi tunavyomfahamu Mungu haifiki hata theluthi ya ukweli wake halisia."

Become a better you, by Joel Osteen

Wako katika kalamu Amani bin Dimile

#amanidimile #misemoyahekima #tusomevitabu #mtotowafundimota #fikrazadimile #becomeabetteryou #tungomaridadi #tangaselftour
6770118-XXZNKWDX-7.jpg
 
Waislam wanasema Allah anajibu maombi yao lkn nao wakristo wanasema Yesu anajibu maombi yao. Mungu wa kweli wapo wangapi?

Na kama ni mmoja, mbona watu wanaabudu Miungu tofauti lakini wanapata matokeo sawa? Anayeabudu Mungu wa uongo anapata matokeo sawa na anayeabudu Mungu wa kweli,hii imekaaje?

Au maombi ni dhana tu lkn hakuna kitu kama hicho?
 
Back
Top Bottom