WaTanzania hii ni AIBU

WaTanzania hii ni AIBU

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,673
Reaction score
14,052
Mara kwa mara toka kale tumekuwa tukijinasibu kwamba sisi hatuna ukabila wala chuki kwa kujilinganisha na majirani zetu wa Kenya,

Lakini cha ajabu waTanzania tumekuwa na mambo ya kutia aibu sana hasa ninyi ma Diaspora mambo ya kuchomana chuk, wivu, fitna,uchawi na ushirikina,

Wenzetu wa KE tunawasema wana chuki na ukabila lakini tafiti zinaonyesha wana umoja wenye nguvu sana biashara za maana ambazo watanzania ndio tumekuwa cheap labour kwao,(kwa kifupi waTZ ni watumwa kwa wa KE)

Kwa upande wa nyumbani wa KE wamewekeza.... DATA zipo waweza ku google....kila mwaka mabilioni yanaingia nchini mwao,,,siye watanzania aaahhh twakwea minazi tu.

Pamoja na vurugu zote za Trump lakini waKE wamefanikiwa ku ''lobby'' kwa raia wao wasio na makaratasi kupata msaada wa green card hasa wenye record safi na wale wanao fanya kazi halali kwenye sekta ya afya,,,siye mabalozi wetu na mawaziri aaah hawana khabari yakhee..

Wenzetu wanawekeza nchini mwao kuna viwanda vya ma Diaspora kuna Mahoteli ya Diaspora kuna mashamba na mifugo ya Diaspora....sisi waTanzania kama tukianzisha ka umoja fulani ghafla yanaibuka maneno umbeya fitna majungu kuharibiana n,k, ndugu zangu hii ni AIBU,

NIPO TAYARI KUKOSOLEWA KAMA HUU NI UONGO.
 
1773749172378.jpg
 
Sasahivi Tanzania ukitaka kuonekana msomi, anza kuitukana Tanzania bila sababu za msingi. Bure kabisa 🚮🚮
 
Kama wewe hujawah kuitwa diaspora basi haya uliyoandika ni chuki binafsi na hisia zako tu...
Ukiwa diaspora ndio utajua ukweli wa hiki uliandika
Nipo tayari kukosolewa kama huu ni uwongo.
 
Ni diaspora Gani atakuwa Tyr kuwekeza kwenye nchi ambayo mihimili yake inaendeshwa kwa
utashi wa kisiasa?
Nchi ambayo mwanasiasa akiamua ulale rumande inawezekana
Nchi ambayo mwanasiasa akiamua ufilisiwe inawezekana
Nchi ambayo watekaji wanakupigia simu na kukwambia kuwa watakuteka na hakuna watakachofanywa
 
Ni diaspora Gani atakuwa Tyr kuwekeza kwenye nchi ambayo mihimili yake inaendeshwa kwa
utashi wa kisiasa?
Nchi ambayo mwanasiasa akiamua ulale rumande inawezekana
Nchi ambayo mwanasiasa akiamua ufilisiwe inawezekana
Nchi ambayo watekaji wanakupigia simu na kukwambia kuwa watakuteka na hakuna watakachofanywa

spot on, mtu akikuchukia kwa sababu yoyote ile siku akipata cheo au power yoyote ile basi ukatafute pa kuishi vinginevyo utaozea jela, na hakuna kitu utafanya, uonevu kuanzia chini mpaka juu mwenye nguvu anakanyaga wa chini hata wana msemo wanaita ''kanyaga twende'' hata raisi mstaafu alisikika akimwambia mwigulu wm mpya kwamba kanyaga twende, evil system ...
 
Back
Top Bottom