Watanzania hawakuwa miongoni mwa Walinda Amani wa UN waliouawa katika helikopta nchini DRC? Serikali tutoeni hofu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Kuna Ndege (Helicopter) ya MONUSCO (Askari wa Kulinda Amani huko Congo DR) Jana imedunguliwa ikiwa na Askari Nane ( 8 ) wa Kulinda Amani na Wote wamefariki dunia.

Natambua kuwa Tanzania ina Askari wake wengi pia huko ambao 'batch' ya mwisho iliondoka Wiki Mbili au Tatu tu zilizopita baada ya wale waliokuwepo huko kwa Miezi 13 Kurejea nchini hivyo so vibaya sana kama Serikali itatoa Tamko lake kama katika hao Askari Nane waliokuwepo na wamewafiriki hakuna wa kutoka Tanzania ili tutoe Hofu.

Taarifa ya 'Kudunguliwa' kwa 'Chopper' hii iliripotiwa Jana Jioni na BBC Dira ya Dunia kupitia Redio One ambapo Watangazaji wa Zamu walikuwa ni Wadada Regina Mziwanda na Scola Kisanga.
 
Wanajeshi wa Tanzania sio exceptional, sema jeshi lina taratibu zake za kutoa taarifa….. utaambiwa kile jeshi litaona kinafaa.
 
Kwani lazima kuingilia mambo ya nchi za watu akati huku dar kwenyewe amani hamna tu panya road tunasumbua!
 
Ni utapiamlo wa akili kuamini kuwa Serikali ya Mapaka kama hii inaweza kusema ukweli🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom