‘Watanzania changamkieni biashara Sudani Kusini’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Watanzania changamkieni biashara Sudani Kusini’

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jun 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  USHAURI umetolewa kwa Tanzania na Watanzania kuamka na kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara ambazo zimejitokeza nchini Sudani ya Kusini.

  Ushauri huo ulitolewa Siku ya Jumatano na Meja Jenerali Wynjones Kisamba ambaye ni Naibu Kamanda wa vikosi vya kulinda amani katika jimbo la Darfur maarufu kama UNAMID, wakati alipokutana na kubadilishana mawazo na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York.

  Meja Jenerali Kisamba yuko hapa Umoja wa Mataifa, kwa ziara ya kikazi na mafunzo ya maOfisa wa ngazi za juu katika misheni za Umoja wa Mataifa, mafunzo ambayo yameandaliwa na Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa (DPKO).

  “ Tanzania tuna kila sababu ya kuwekeza nchini Sudani ya Kusini, zipo fursa nyingi mno kuanzia upelekaji wa chakula hadi ujenzi. Nilikuwa nyumbani hivi karibuni, nimekutana na viongozi mbalimbali na kuwaelezea juu ya fursa hizi”, alisema.

  Alisema ana wasiwasi kwani Watanzania wanachelewa kwani majirani wa Tanzania wamekwisha zichangamkia fursa hizo na wako mbali na kwamba ni kama wameishaingia mpaka jikoni.

  Aidha katika mazungumzo yake na maofisa wa ubalozi, Naibu Kamanda wa vikozi vya UNAMID alibainisha kwamba kama kweli Serikali, kwa kushirikiana na sekta za umma na binafsi zikiamua kuingia kibiashara Sudani ya Kusini hakuna tutakachopoteza.

  “Sudani ya Kusini ndio kwanza wanaanza kuijenga nchi yao, wanachangamoto nyingi, sisi tunaweza kuwasaidia kwa maana ya kuwekeza na kwa kufanya biashara. Kwa mfano wale wanakula sana chapati, hawana ngano, tunaweza kuwauzia ngano, wanahitaji mafuta ya kupikia tunayo alizeti, wanahitaji vifaa vya ujenzi, tuna viwanda vya saruji na nondo pia, kwa kweli fursa zipo tunachotakiwa ni kujipanga.
  ‘Watanzania changamkieni biashara Sudani Kusini’

   
 2. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hili
  wameshaambiwa sio mara moja
  mfano kwa sasa kuna zaidi ya Wakenya zaidi ya elfu ishirini na tautu wanafanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato KUSINI MWA SUDANI
  badala ya serekali kuwekeza kwa kuajiri vijana wanaoweza kutambua fursa mablimbali zilizopo katika nchi mbalimbali WATAWALA wanajitahidi kuwekeza kuwaua wanaowaona wanawapinga na wanaopigania haki
  tumeshashauri kwakuwa hatuna platform hizi fursa lakini hata ukiwaandikiwa hawajibu, ukitum mail wala hawajibu

  kinachoniumiza kuna WATANGANYIKA wengi wamepata pesa kariakoo badala ya kujenga vihoteli vidogo kariakoo
  tumeshauri kwanini wasizijenge JUBA?au GOMA na kwingineko

  Natamani tena saan WAINGEREZA wasingetupa UHURU tungekuwa na maendeleo zaidi
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda sana hiyo picha ya Ben Curson. Huyo bwana ni one of the best neuro surguries in the world. But he built his fortune and career by hard working. He learned the importance of leading bookd earlier in his life to the extent that he became so knowledgable. Jamani wale wafanya biashara wa kariakoo wachache sana wanaweza kuvuka mpaka na kufanya biashara. hatuna maarifa sisi...na kibaya tu wazito sana kuyatafuta hayo maarifa. Ila sudan kusini is the place to be...
   
 4. m

  mamasuma Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usalama mhhh, juzijuzi mkenya kapigwa risasi kule tena mwalimu wa nursery school maskini eti sijui hakusimama wakati bendera inapandishwa, mie nilikuwa interested saana sana lakini usalama kwanza!
   
 5. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hakuna asiye penda maendeleo/ mabadiliko ya biashara yake, lakini kama usemavyo usalama wa wangu na mali yangu unalindwa vipi?
   
 6. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwenye business venture kuna kuwa na changamoto...na bigger the risk, the BIGGER the Cake!!
   
 7. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu Tanzania Bado sana, Na Tatizo kubwa linalo kabiri wafanya biashara wa Tanzania ni kupenda kufanya Biashara kiujanjaujanja sana, sasa sehemu ambazo hazina njia za mikato wanapata shida sana, that is wahy

  MFANO:
  1. Chukulia Ujenzi holela wa magorofa yasiyo fuata utaratibu kule kariakoo- Nchi nyingine hawana njia za mikato ni lazima sheria zifuatwe,

  2. Cheki sheri za mafuta zinavyo jengwa bila kufuata sheria

  KWA NCHI AMBAZO ZINAFUTA SHERIA ZOTE NA HAKUNA RUSHWA HATA KIDOGO WABONGO TUNAPATA SHIDA SANA


  Swala Jingine ni Watanzania kuto penda kabisa kufanya Network, tunasubiri serikali ndo ituambie twende SUDANI, wakati wakenya wao wameenda wenyewe na wala hawajasubiri kuambiwa, kwenye bara la africa kuna Maonyesho kibao ya biashara lakini sijui kama Watanzania huwa wanahudhuria,

  Angalia hata Maonyesho ya Sabasaba, Wakati Wafanya biashara wa Nchi zingine wamekuja kutafuta masoko na kutafuta watu wa kufanya nao BIASHARA Watanzania tuko bise kuuza, na ukipita Banda la wabongo usipo nunua wananuna, Wakati wachina wako bise kuchukua contact na kuuliza kama mnaweza fanya biashara,

  Nakumbuka kuna kipindi fulani kule Arusha wakati Jumuia ya Africa mashariki ndo inaanza, Kulifanyika MAONYESHO YA WAFANYA BIASHARA WA NCHI TATU KWENYE UWANJA WA MPIRA WA ARUSHA, na yalikuwa maalunu kwa ajiri ya wafanyabaisha wa Tanzania , kenya na Uganda kufahamiana, Cha kushangaza WAFANYA BIASHARA WA TANZANIA WAKATI WANAITWA KUJITAMBULISHA WAO WALIENDA NA BENDI YA TOT kipindi hicho ikipiga Bilingo, na hawakuwa na cha kuonyesha, Wakati wenzao wa Kenya na Uganda walikuja full na Business card na kazalika, Wabongo hata Business card waliona haina haja, KWA KIFUPI NDO HIVYO,

  Maonyesho ya SABASABA ni PICHA tosha kwamba hatuwezi hata kwenda Burundi Achilia mbali huko SUDANI KUSINI, maonyesho yametawaliwa na Promosheni za pombe, full miziki, na full kuchuuza bidhaa za kichina, NA KINACHO UMA ZAIDI NI KWAMBA UCHUUZI UNAOFANYWA NA WATANZANIA PALE NI WA KUCHUUZA BIDHAA ZA CHINA BORA HATA ZINGEKUWA ZA TANZANIA, hivi kwa stail hii tunaweza enda SUDANI?

  Mkuu kwa kifupi ni vigumu sana na Mifano ni mingi sana hata humu JANVINI KUNA MIFANO TOSHA,

   
 8. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Prodigy son my brother, umefika mbali. Usifanye hasira za mkisi, furaha ya mvuvi., Nadhani tunahitaji kuelimisha watu na wafanyi biashara wetu. Haya yanaweza kurekebishika. Tufundishe Standard financial literacy and some basic economic theories, kwa kutumia lugha ya kawaida ambayo mwanaichi wa kawaida wataielewa. Na jinsi ya kutafsiri economic data. Pia tuwafundishe English.

  Great posting. Lakini kumbuka kua hawa wenzetu wemekua kutoka kwenye siasa za ubepari (let's call for what it is) toka mkoloni. Sisi tumeanza hivi karibuni tu. Kwanza nawapa kredit kubwa sana Wafanya biashara wetu kwa sababu sidhani kama serikali yetu ilijiyarisha na how to manage a free enterprises system. Hata regulations mpaka leo bado wanazifanyia kazi kitu ambacho kinaongeza rushwa na pia kinamrudisha mfanya biashara nyuma. Kuna mambo flani kama hayo nilioandika hapo juu yakifanyika mfanya biashara wa Tanzania atakua very competative. Wewe naona ni muandishi mzuri, anza kufikiria na kuandika kuhusu solutions.

  Kuna WAJASIRIMALI wengi hapa Tanzania, wakipata information kama hii wanaweza kwenda. Najua vijana wengi wenye moyo wa kutaka maendeleo na wanaweza kupima kiwango cha faida na hatari zake. I am from the street and I 've done some tradings. There is an Entrepreneurial spirit out there. These are naturally talented and tenacious. something our neighbors have never seen. Just teach 'em english, since it's boils down to communication.
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ukiwa na sifa zote za Ujasiriamali huhitaji Serikali ikuwezeshe au ikujengee mazingira ya kwenda SUDANI, mfano Je kuna tatizo la kupata VISA?

  Mkuu kuhusu kwamba tulikuwa na mfumo wa Kijamaa, hiyo sio hoja sana make kuna Nchi nyingi sana zilizo kuwa zinapractise Ujamaa lakini leo hii ziko Mbali sana, HATA CHINA TUNAYO IONA LEO ILIKUWA INA PRACTISE UJAMAA TENA ULE UJAMAA WA HALI YA JUU(UCOMONIST)

  Tuna matatizo mengi sana sisi kama watanzania, tumeisha rizika na biashara za huku Tanzania, NA UNGEENDA SABASABA NDO UNGEAMINI KWAMBA TUNAMATATIZO MAKUBWA SANA INGAWA HATA VIONGOZI HAWAYAONI HAYA NA KUBAKIA KUSIFIA TU MAONYESHO,

  Kwa staili ile ya SABABSABA ni vigumu sana kufanya biashara hata BURUNDI, Jarubu kwenda pale SABASABA WAHAJO WAFANYA BIASHARA WETU USIKIE, oo maonyesho yamekuwa magumu sana hatujauuza kabisa, watu hawana pesa na kazalika, NA JARIBU KUWAHOJI WALE WACHINA, Utasikia yes tumeweza kupata patiners kadhaa, au tumeshindwa kabisa kupata patiners au supplya wa kusaply bidhaa zetu,

  Lakini kwa WABAONGO huwezi wasikia pale wakisema wamepata PATINERS AU WAMEPATA SOKO wao wanazungumzia kuuza tu, KWA STAIL HII HATUWEZI KABISA,

  NA kabla hatujataka kwenda SUDANI ni lazima tufanye vizuri Ndani ya NCHI YETU, swali, JE WAFANYA BIASHARA WATANZANIA WANAFANYA IPASAVYO KWENYE SOKO LA NDANI? Kama ni yes wanaweza kwenda lakini kama ni NO hawawezi kwenda SUDANI,

  Na Internatinal Trade Unaanza kwanza na DOMESTIC market ikisha jaa ndo unazungumzia kwenda Nje ya Nchi, Leo hii unakuta tunaanza kuzalisha ASALI NA KUTAKA KUUZA MAREKANI WAKATI SOKO LA NDANI LENYEWE HATUJALIKAMATA,
   
 10. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2012
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mkuu, naandika kwa ajili ya paragraph yako ya kwanza na ya pili hapo juu. Malalamiko kuhusu SabaSaba 2012, nadhani ni muhumu tume ya maandalizi Uwanja wa sabasaba na wafanya biashara wa TZ, wajirudie na kuchuja hali yote na kujirekebisha. Ni aibu na inatuma meseji mbaya kwa wageni wetu. Kwenye trade shows biashara husaidiana kuhakikisha tafrija inaleta biashara. Na pia wasikose business card, lengo kuu la trade show ni networking na kujitambulisha kwa wateja.

  Kuhusu paragraph ya kwanza
  Wanaojifanya magwiji wa biashara ndio zao, Hata hivi juzi Europian Union imekubali kuzisaidia benki zilizopoteza hela. Ingawa hii bail out sio ya kawaida lakini misaada kutengenezewa mazingira mazuri ya biashara hufanyika mara kwa mara. Wanadai, Katika Free Enterprises system, kazi ya serikali ni kusaidia private sector na kutengeneza mazingira yakuhamasisha biashara (kuregulate). Tena nchi za ulaya, Japani na marekani ndio wanafanya sana hii kitu. Kampuni nyingi za China zinasaidiwa na serikali yao, hadi mikopo.

  Kuhusu Paragraph ya pili.
  Pointi nzuri, lakini China ilijiandaaa sana. Kwa mfano, kuna wakati USC (University of Southern California) ilipata kutaniwa na kuitwa University of Sino California. Kwa kua wachina walikua wengi yani majority. Na hio ni shule moja tu. Halafu ukipata nafasi soma kuhusu sheria walizowekewa wawekezaji huko China.
   
 11. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,403
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Suala la msingi ktk kufanya biashara huko south sudan tokea watengane ni kuwa ar u tough?unaweza kumtisha mtu ama kumkomalia mpaka akupatie malipo yako?nna jamaa zangu wa uganda walikuwa wakifanya bznes huko sasa wamekuja kufanya tz wakisema watz ni wakarimu,xo kama unaenda kufanya ujijue kuwa ur tough enough n fearless
   
 12. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,316
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Usalama ni jambo muhimu sana kibiashara wakati umefika kwa sudani-kusini kujizatiti katika hili kwanza alafu mambo mengine yatafuata likiwemo lile swala la kujiunga na eac.
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kama kuna mwenye websire mbalimbali za taarifa za Sudan ya Kusini tafadhali weka hapa. Asante...
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mtanzania tabia yake kukaa kwenye comfort zone siku zote. Ndio maana hata hii jumuia ya Afrika mashariki sisi haitatunufaisha sana kwa kuanzia labda hapo baadae tufaidi kwa kuchangamshwa na wakenya kutokana na zile mishe mishe zao. Kwa haraka haraka sioni mtanzania ambaye anaweza kwenda kwenye mazingira mapya kama huko akaanzisha mradi. Labda Bakhresa tu akafungue KIwanda cha unga.
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu Bakhresa naye si mtanzania?
  Mkuu, na mitaji ya kuungaunga si rahisi kulianzisha katika nchi ambayo hata serikali yaek imegundua kuwa haiwezi kuanza kushughulikia maendeleo mpaka pale swala la amani litakapokuwa stable.
  Sasa hivi ninaoweza kuwashauri kulianzisha kisouth Sudan ni watu wanaotaka kufanya kazi za UN etc...
   
Loading...