Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,913
- 6,516
Ubalozi wa Tanzania Nchini Afrika Kusini umethibitisha kukamatwa kwa zaidi ya raia 90 wa Tanzania na kuwekwa katika Kituo cha Lindela kufuatia msako wa Wahamiaji Haramu unaoendelea Nchini humo.
Akizungumza kwa njia ya simu na AyoTv_ Balozi wa Tanzania Nchini humo James Bwana amethibitisha kuwapo kwa Watanzania waliokamatwa kutokana na vuguvugu linaloendelea dhidi ya Raia wa Kigeni.
Soma Pia: Balozi Bwana: Video inayosambaa mitandaoni haihusiani na matukio ya vurugu dhidi ya Waafrika Kusini na raia wa kigeni, Watanzania wapo salama
"Hawa 60 wanatoka maeneo ya kwetu huko Nchini Tanzania ikiwemo Mbagala, Ilala, Tandika,Kilwa, Magomeni, Temeke, Kariakoo, Mbezi Juu, Manzese, Mwananyamala, Kiwalani, Keko, Mbezi, Kimara, Tabata, Zingiziwa na mmoja ni Tanga kwahiyo ukiangalia hapo kwa tathmini ya haraka asilimia 99 ya hawa Watu wanatoka mkoa wa Dar es salaam”—— Bwana.