‘Watanzania changamkieni biashara Sudani Kusini’

‘Watanzania changamkieni biashara Sudani Kusini’

hiyo fursa tuambiane wote jamani has aupande wa kupeleka mbogamboga huko au nafaka
 
Duuuh mi nasubiri kwa ham na Kama vp tukishapata nondo tujiorganize ki group twende direct tuje kuwafahamisha wenzetu mi nadhan ukitaka kuwahi nenda peke yako lakn ukitaka kufika umbali mrefu nenda na wenzako
 
fursa za sudani kusini ni nyingi hasa ukizingatia ile ni nchi iliyokumbwa na vita muda mrefu na hivyo kukosa uzalishaji wa kitu chochote kuanzia bidhaa za kilimo hadi viwandani na ukumbuke hawana viwanda.
 
kwa mgeni ni rahisi kufanya biashara juba maana ni mjini japo kuna miji midogo pia ambayo imechangamka kibiashara.
 
mo dewij ni moja kati ya watanzania wanaonufaika na soko la wasudani na hasa anapeleka mchele na unga wa mahindi.
 
pesa ya sudani kusini ni pound ambayo thamani yake ilikua kubwa karibu na dollar ya marekani, sudani kusini ni eneo ambalo kwanza nafaka, mbuzi, kuku, mchele, kwa ufupi bidhaa za vyakula zinasoko sana.
 
bidhaa au vifaa vya ujenzi pia ni mali sana hasa ukizingatia ndio kwanza nchi ilikua inajengwa na ni changa vitu kama nondo, cement, chokaa na matofali vinauzika sana hivyo wafanyabiashara kutoka kenya na uganda waliofungua maduka ya hardware walitengeneza pesa nyingi sana.
 
kwa wanunuzi wa dhahabu pia wanadhahabu nzuri ambayo ina asilimia 98 hadi 99 nadhani wafanyabiashara wa dhahabu mtanielewa hapo nina maana gani.
 
migahawa, internet cafe, stationaries, ni moja ya eneo ambalo watu hufanya biashara pia.
 
makampuni ya usafi pia ni biashara inayolipa kwani kuna makampuni na maofisi yanayohitaji huduma ya usafi ukipata pia yale mashirika ya umoja wa mataifa hulipa vizuri.
 
kama maada inavyojieleza naulizia fursa ya biashala sudani kusini kwa yule anayejua au mwenye connection
 
usalama mhhh, juzijuzi mkenya kapigwa risasi kule tena mwalimu wa nursery school maskini eti sijui hakusimama wakati bendera inapandishwa, mie nilikuwa interested saana sana lakini usalama kwanza!
High risk more money.Sifieni amani tu huku mkiwa mnakufa kwa njaa na ufukara
 
Pesa kwanza Mengine baadaye,sawa na kusema Machangudoa wafe na njaa ndani sababu ya kuogopa Ukimwi,Na mwanaume ufe na njaa sababu ya kuogopa vita
 
Back
Top Bottom