Watanzania bila kujali vyama vyetu tushikamane kumdhibiti Sizonje. Vinginevyo......

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Huku serikalini amekanyaga katiba kwa kiwango kikubwa, ameikanyaga mihimili mingine (bunge na mahakama) kwa kiasi cha kutisha. Amevunja sheria na taratibu za utumishi na watumishi kwa kiasi kisichoelezeka. Tumenyamaza tu. Wachache sana wamekuwa na uthubutu wa kumkosoa, mifano ya waliothubutu mnayo.


Yote haya yakitendeka niliamini kwamba chama chake ccm kina uwezo mkubwa wa kumdhibiti na kumuonya. Lkn kwa alichokifanya leo huko Dodoma !! Kinanitisha sana.

Ameikanyaga katiba ya chama chake.

Kivipi?
amewavua uanachama viongozi wa ccm, halafu ili kuogopa kuhojiwa amewazuia wajumbe wailiomo safarini kwa sasa kuelekea kwenye mkutano huo wa kikatiba wa ccm wasihudhurie mkutano huo. Makatibu wote wa mikoa na wilaya wasihudhurie mkutano huo.

Hii ndiyo kusema alichokiamua kimepita na mkutano wa kesho haupo. Maamuzi yote yamefanywa leo.

Siko hapa kuikosoa ccm, bali kutoa mwito kwa watanz wote tutafakari kwa pamoja mwenendo wa Sizonje. Nani atamdhibiti endapo bunge, mahakama na chama vyote vitakuwa mfukoni mwake?
 
Kiongozi wa nchi ni kama baba ndani ya familia.

Kiongozi lazima uwe na maamuzi magumu, hata kama kuna watu wataumia na kupoteza maisha, ni sawa tu; sababu ni heri wachache waumie ili wengi wapone.

Ukiwa kiongozi wa nchi yenye watu zaidi ya milioni 45, tena wenye vichwa vigumu kama Watanzania, ni lazima uwe na roho ngumu kupita ya Hitler, vinginevyo watakutia vidole machoni.

Hongera Rais Magufuli kwa kazi nzuri, tuko pamoja mpaka 2025!
 
Sikubaliani naye kuanza kufukua makaburi ya uchaguzi wa 2015. Katk chaguzi kila mwanachama anakuwa na mgombea anaye. muunga mkono. Sasa hiyo haki ya kidemokrasia isiminywe. Hapo maana yake anatuma ujumbe kwa wanaccm wengine kwamba wakimpinga watafukuzwa.

Lkn pia angeruhusu vikao halali vifanye maamuzi
 
Mlionywa ...hamkusikia
Sasa huko dodoma ni patashika ...kumbe mtu anataka kubadilisha katiba kila kitu na anataka kwa mabavu aungwe mkono kwamba apitishwe bila kupinga 2020 na nawaapia nyinyi watanzania ikikubalika hio ndan ya lichama lenu nawaambia huyu atatawala milele nchi hii mana itakua rahis sasa kubadilisha na katiba yenu ya nchi..ndo yaleeeee ya uganda/rwanda/burundi/congo...
 
Bado najiuliza kuwa kipindi chote ambacho sheria na taratibu zilikuwa zinafuatwa kama taifa....tulipata faida zaidi ya kukithiri kwa wizi na kila aian ya uozo kwenye idara za serikali.......

Mimi kwa mtazamo wangu....kama yanafanyika haya kwa ajili ya kuliokoa taifa sioni ubaya wowote kwani sheria nyingi na taratibu ziliwekwa na mabawanyenye kwa manufaa yao na vibaraka wao.......

Kwa pamoja tutaijenga tanzania.....
 
Bado najiuliza kuwa kipindi chote ambacho sheria na taratibu zilikuwa zinafuatwa kama taifa....tulipata faida zaidi ya kukithiri kwa wizi na kila aian ya uozo kwenye idara za serikali.......

Mimi kwa mtazamo wangu....kama yanafanyika haya kwa ajili ya kuliokoa taifa sioni ubaya wowote kwani sheria nyingi na taratibu ziliwekwa na mabawanyenye kwa manufaa yao na vibaraka wao.......

Kwa pamoja tutaijenga tanzania.....
A LIKE FOR YOUR COMMENT. MAY YOU MERRY FOR A NEW COUNTRY HAS BEEN BORN. DO YOU BELIEVE IN DEMOCRACY, WELFARE AND GOOD WILL.
 
Back
Top Bottom