Watangazaji wa TV mjifunze jinsi ya kuvaa

TBC wanatia huruma sanaa maana kipindi hiki nilitegemea wangepigwa tafu lakini maajabu yake "Viongozi" wakuu wanaipa promo Clouds! Inasikitisha sana. Sijui nani alituroga.
 
Moja kati ya maeneo ambayo mwandishi wa Habari hasa msoma habari anatakiwa awe kamili ni muonekano. Nimekua nikiliona hili kwenye vyombo kadhaa vya habari hapa ndani na kimataifa ninapo fuatilia vipindi.

Tatizo nilililo liona kwa Television ya Taifa chini ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ni uvaaji mbovu wa watangazaji wake. Ninaposemea mavazi sio lazima iwe nguo za gharama namaanisha hata ule mpangangilio tu wa mavazi Kama rangi, namna ya kumechisha mavazi na kadhalika, nini cha kuvaa nini sio cha kuvaa nk.

Leo asubuhi nlikua nikifuatilia kipindi walicho kiita kuelekea Brazil 2014 alikuwepo kijana anaitwa Mbozi Katala kwa jinsi alivyovyaa to be honest hii ni aibu kwa shirika na nchi. TBC inaonekana kwenye ving'amuzi vya DSTV ambavyo ni World Wide sasa uvaaji wa hivi ni sawa na kuwatangaza wanaprofesheni ya habari Tanzania kuwa ndivyo walivyo. Sio huyu tu nimekua nikifuatilia kwa mda sasa wanahabari wa TBC ni aibu kwenye mavazi. Yupo dada mmoja anasomaga michezo ingawa ki ukweli uwezo wake ni mdgo kwenye ufaham wa michezo ila kwnye mavazi ndio hakuna kbsa. Hapa sijagusia ile confidence na uwezo wa kusoma habar kwa uhuru na vzur kama akina Salim Kikeke na wengneo hilo nalo ni tatizo kila ninapo mwangalia Gabriel Zakaria.

Wengine wanawezaje nyinyi TBC mshindwe..?? Watendaji mko wapi au na nyinyi hamuoni au hamjui umuhimu wa mavazi kwa wanahabari..?? Mwandishi muhimu uwe smart tofauti na watangazaji wengi wa TBC nnavyo waona. Mnalitia aibu taifa. Pale BBC kuna dada mmoja anaitwa Nagga Munchetty huyu binti anavaaga simple sana lakini mavazi yamepangiliwa kuanzia rangi mpka muonekano.

Sio unakuta mtu kavaa shati nyekundu, suti ya kijani na tai nyeupe halafu Suti yenyewe bega la kushoto limeegemea mbele la kulia kubwa zaid too bad eti anakukaribisha uskilize habar huku anasmile.. Hii ni aibu kwa nchi. Nyie TBC badilikeni!
Hawa TBC Wana matatizo mengi Sana! Hata Vichwa vya magazeti vinasomwa kwa kugeuzwa ni sheeda bin taabu
 
he hivi TBC bado ipo me nilijua serikali wameshaifunga maana wote rais,wazir na mkuu wa mkoa wake wamekimbia clouds sikuhizi...
 
Hv lengo ni habari au mavazi? Hiv kumbe wengine huwa hamna shida ya kuangalia habari ila munaangalia mavazi eeh??
Ukijua maana ya kifungashio au packaging huwezi kuuliza swali kama hilo lako. Soma tu comment za wengine upite kuna watangazaji hii nchi wanavaa mpk skin jeans kauonyesha makalio tu na kucheka Cheka Mbele ya camera.
Hata appetite ya kuangalia TV za home inapotea.
Mavazi mabovu, lugha kiswanglish, picha zenyewe hazing'ai studio haina hata mpangilio mbayaaaaaaaaaaaaaà
 
Back
Top Bottom