Watangazaji wa mwanzo Radio One na mbwembwe zao

FM stereo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2011
Posts
206
Reaction score
123
Charles Hillary a.k.a Jitu

Julius Nyaisanga a.k.a a Anko J

Flora Nducha

John Dilinga

Sebastian Maganga

Sostenes Ambakisye

DJ Fast Eddy

Misanya Bingi

Asia Mohamed

Hivi hawa watangazaji wako wapi siku hizi, wakati Radio One iko hot hawa jamaa ndio walio ifanya ing'are sana wakati ule...
mwenye kukumbuka mbwembwe na utashi wao katika vipindi walivokuwa wakitangaza Radio One atutupie hapa..
 
Attachments

  • Kikosi Kazi cha KWANZA RADIO One,,mwaka 1993..kutoka kushoto waliosimama..H.,Deo Mshigeni.,Mike .jpg
    Kikosi Kazi cha KWANZA RADIO One,,mwaka 1993..kutoka kushoto waliosimama..H.,Deo Mshigeni.,Mike .jpg
    61.4 KB · Views: 823
unimekumbusha mbali mkuu, wakati huo Radio One ilikuwa ndo kama radio ya taifa.

Charles Hilary 'mzee wa macharanga' a.k.a Nkwanga yuko BBC
Anko J alikwenda Radio Aboud sijui yuko wapi hivi sasa
Flora Nducha yupo Radio ya umoja wa mataifa
Misanya Bingi ni mhadhiri UDSM
John Dilinga na DJ Fast Eddy wanaendelea na udj
Sebastian Maganga yupo Clouds FM
Sostnes Ambakisye anapiga dili zake.
Asia Mohamed alipotoka Radio One alikwenda Radio Uhuru sijui kama bado yupo uko.
 
pia kuna Abubakari Liongo alikuwa anatangaza sports leoooo
jamaa alikuwa anatangaza vizuri sana.

DJ JD na Sostnes Ambakisye walitamba kwenye kipindi cha "The Heat"
DJ Ommy kwenye DJ Show
Mike Mhagama
 
charles hilary mzee wa kipusa duh kipindi chake cha chemsha bongo nilikuwa nacheka sana
 
Chemsha bongo na Abdala Majura pia alikuwa anaiweza sana,,,,kitenge naye pia amekaa sna radio one pale...

Kuna abuubakari liongo,,,huyu na majura walikuwa wakitangaza spot leo hata kama sio mpenzi wa mpira utafurahi tu,,, maana walikuwa wanawabana sana na maswali viongozi wa FAT Ndolanga na Rage....

Mara kibao tu Ndolangaa na Rage walikuwa wanachafukwa kweli na maswali ya Majura au Liongo wakati ule.....

"Sioo unaongea tuuu praaaa praaa praaa kama bata liloharisha, wewe hujui mpira babko hajui mpira mamako hajui mpira..."
 
unimekumbusha mbali mkuu, wakati huo Radio One ilikuwa ndo kama radio ya taifa.

Charles Hilary 'mzee wa macharanga' a.k.a Nkwanga yuko BBC
Anko J alikwenda Radio Aboud sijui yuko wapi hivi sasa
Flora Nducha yupo Radio ya umoja wa mataifa
Misanya Bingi ni mhadhiri UDSM
John Dilinga na DJ Fast Eddy wanaendelea na udj
Sebastian Maganga yupo Clouds FM
Sostnes Ambakisye anapiga dili zake.
Asia Mohamed alipotoka Radio One alikwenda Radio Uhuru sijui kama bado yupo uko.

Umewasahau Abdallah Majura na Anko Masoud Masoud, Abdallah Hussein, Sunday Shomari, Mike Mhagama na Rose Chitalah.
 
Nimewatambua wawili tu, wa kwanza kushoto (waliokaa) ni Charles Hillary Nkwanga na wa kwanza kulia (waliokaa) ni Julius Nyaisanga aka Anko J.

Waliokaa: Charles Hilary (kushoto), Mikidadi Mahmoud (wa pili kushoto) na Julius Nyaisanga (kulia).
Waliosimama kutoka kushoto ukiondoa huyo dada wa kushoto kabisa na mwingine aliyevaa nguo ya draft ni Sebastian Maganga, Mike Mhagama, Monica Mfumia, Flora Nducha, Vicky Msina, Aboubakar Liongo, Sunday Shomari na Taji Liundi. Hii kama sikosei ilikuwa ni 1995.
 
Timu ta radio one wakati uleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....

Nani mjanja anayeweza kuwatambua walioko hapaView attachment 101905

Waliokaa: Charles Hilary (kushoto), Mikidadi Mahmoud (wa pili kushoto) na Julius Nyaisanga (kulia).
Waliosimama kutoka kushoto ukiondoa huyo dada wa kushoto kabisa na mwingine aliyevaa nguo ya draft ni Sebastian Maganga, Mike Mhagama, Monica Mfumia, Flora Nducha, Vicky Msina, Aboubakar Liongo, Sunday Shomari na Taji Liundi. Hii kama sikosei ilikuwa ni 1995.
 
Chemsha bongo na Abdala Majura pia alikuwa anaiweza sana,,,,kitenge naye pia amekaa sna radio one pale...

Kuna abuubakari liongo,,,huyu na majura walikuwa wakitangaza spot leo hata kama sio mpenzi wa mpira utafurahi tu,,, maana walikuwa wanawabana sana na maswali viongozi wa FAT Ndolanga na Rage....

Mara kibao tu Ndolangaa na Rage walikuwa wanachafukwa kweli na maswali ya Majura au Liongo wakati ule.....

"Sioo unaongea tuuu praaaa praaa praaa kama bata liloharisha, wewe hujui mpira babko hajui mpira mamako hajui mpira..."
Mkuu umenikumbusha mbali sana na nimecheka kwelikweli.
 
Pia walikuwepo Blandina Munghezi (Anti Ndina) na DJ Rankim Ramadhani.
 
kitenge utangazaji wake kamuiga Aboubakar Liongo.Dj rankim ramadhani jamaa alikuwa kiboko. Misanya bingi aka def defao, redio one wamepita watu wengi sana akina sunday shomari, reggae time ilikua ilikuwa inachagizwa na ule wimbo wa steel pulse Rally round the flag aisee nilikuwa sikosi kusikiliza! Kulikuwa na kipindi usiku kuanzia saa nne mpaka saa saba watu wanaelezea masahibu yao ya kimapenzi baadae wasanii wakaingia ikawa uongo mwingi
 
Chemsha bongo na Abdala Majura pia alikuwa anaiweza sana,,,,kitenge naye pia amekaa sna radio one pale...

Kuna abuubakari liongo,,,huyu na majura walikuwa wakitangaza spot leo hata kama sio mpenzi wa mpira utafurahi tu,,, maana walikuwa wanawabana sana na maswali viongozi wa FAT Ndolanga na Rage....

Mara kibao tu Ndolangaa na Rage walikuwa wanachafukwa kweli na maswali ya Majura au Liongo wakati ule.....

"Sioo unaongea tuuu praaaa praaa praaa kama bata liloharisha, wewe hujui mpira babko hajui mpira mamako hajui mpira..."
maneno haya ni ya mzee Ndolanga aka DOO LANGU
 
kitenge utangazaji wake kamuiga Aboubakar Liongo.Dj rankim ramadhani jamaa alikuwa kiboko. Misanya bingi aka def defao, redio one wamepita watu wengi sana akina sunday shomari, reggae time ilikua ilikuwa inachagizwa na ule wimbo wa steel pulse Rally round the flag aisee nilikuwa sikosi kusikiliza! Kulikuwa na kipindi usiku kuanzia saa nne mpaka saa saba watu wanaelezea masahibu yao ya kimapenzi baadae wasanii wakaingia ikawa uongo mwingi

pia kuna someone kisengo,alikua mtangaza mzuri sana wa taarifa ya habar,kuna AMINA MOLLEL-TBC,KUNA MIKIDAD MAHAMOUD-REDIO UHURU,MOSES JUSTINE AKAK PAPA MO,MZEE WA MTAA WA MANGOMA,
 
Wakat huo ilikua si tu inaitwa radio one ila ilikua inaitwa RADIO ONE STEREO
>>radio oneeeeeeeeee,stereooooooooooooo,
na ilikua yasikika mikoa mitano tu na zenji,
dar,mwanza,mbeya,dodoma,zenj na kilimanjaro masafa ya medium wave
 
Back
Top Bottom