Kwanini Radio One stereo inasikilizwa sana Arusha , kilimanjaro na Manyara?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,662
16,023
Nimefanya utafiti wangu binafsi na kote nilipopita nimebaini wakaazi weengi zaidi ya 90% wa mikoa ya kilimanjaro, arusha na manyara ni wapenzi wakubwa wa Station ya Radio one.

Mimi nilikua mpenzi enzi za kina Charles hillary , Rose chitallah , misanya bingi, abdallah majura na marehemu Julius nyaisanga.
 
Anhaa kumbe unipe mwaliko wa sikukuu za mwisho wa mwaka maana nyie mlivyo serious utadhani Yesu alikuwa mchaga😂😂
Mwaliko nakupa mda wote , ila ile ya kwenda wote moshi japo imefungamana na Christmas kiupande fulani, ila ile pia ipo kimila kwa wngne na wengne ni fuata mkumbo tu .
 
Nimefanya utafiti wangu binafsi na kote nilipopita nimebaini wakaazi weengi zaidi ya 90% wa mikoa ya kilimanjaro, arusha na manyara ni wapenzi wakubwa wa Station ya Radio one.

Mimi nilikua mpenzi enzi za kina Charles hillary , Rose chitallah , misanya bingi, abdallah majura na marehemu Julius nyaisanga.
Umewasahau watabe wengine wa Enzi hizo redio one kama Deogratius Rweyunga, Maulidi Kitenge,Izack Gamba. Hawa watatu kipindi cha michezo utakipenda wakitangaza enzi hizo.
Wengine ni Double G (Godwin Gondwe) sauti ya zege. Kuna mwamba alikuwa anaitwa Abubakari sadiki katika kipindi cha chaguo la msikilizaji na DJ's choice. Dah noma Sana.
Mimi ni Mtu wa Kilimanjaro na ni kweli kabisa redio one mikoa hiyo uliyoitaja imebamba Sana.
 
Back
Top Bottom