Watangazaji na Vyombo Vya Habari Mnamuona Salim Kikeke Wa BBC Swahili

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,162
3,162
Wana JF, kama wewe ni mfuatiliaji wa kipindi cha BBC swahili cha Star tv kinachorushwa mida ya saa tatu kasoro usiku utakubali kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Utangazaji wa Salim Kikeke na watangazani wa Kitanzania. Pia utaona utofauti wa jinsi habari inavyopangiliwa.

Huyui jamaa na wenzanke kwanza wanatangaza wakiwa huru sana, yaani wanajiachia, wanatabasamu na ikibidi wanaleta jokes kidogo. Yaani kwa ujumla utatamani taarifa isiishe. Kwa upande wa kwetu hapa utaona watangazaji wanasoma taarifa wakiwa hawako huru kabisa, wanasoma taarifa kama vile wanatoa Tangazo kwenye mkutano, wanatangaza utafikiri wameambiwa mguu sawa kama jeshini. Nashauri vyombo vyetu vya habari wabadirike angalau waanze kuwa huru, waalike professionals mbalimbali ambao wanaweza kutoa ufafanuzi wa habari fulani angalau kuweka chachu katika habari.
 
Ushasema nje ya Tanzania nenda kasome kibongo bongo huku unacheka cheka kesho yake usipoamkia kwa pilato
 
Nnachoamin wanawaandalia mavazi na sura tu ili wawe na mimvuto lkn salim anaandaa mwenyewe na huisoma kabla(soma soma enjoy)ndio maana huwa huru sana.na anakimbizana na muda vizuri tu.
 
tatizo la tanzania ukitangaza na ukaleta utani pia ukijiachia sana unalimwa barua ya kufukuzwa kazi usiku huo huo.

watangazaji wa kenya kama ntv na citizen uwa wanajiachia na wako huru adi utapenda kuangalia habari.

lakin watangangazaji wa tanzania wamenuna sura mbuzi. ni kama watu wenye msongo wa mawazo tena fundi mitambo akichelewa kuweka tukio wanagandishwa wanakuwa kama sanamu la michelini adi wanatia huruma
 
Inasikitisha!!!
Kuongea ni kipaji lkn hawa wa kwetu mmmmh kuna watangazaji wengine mpaka ile natural voice yao wanabadilisha inakuwa kama comedian. again wa hapa kwetu
 
Wakwetu wanawaza bahasha tuu na hutoa habari za ikulu,serena hotel,ajali za moto,magari,ugomvi wa wakulima na wafugaji mvomero na kiteto,mauaji mara wamemaliza!kila siku habari ni hizo hizo
 
tatizo la tanzania ukitangaza na ukaleta utani pia ukijiachia sana unalimwa barua ya kufukuzwa kazi usiku huo huo.

watangazaji wa kenya kama ntv na citizen uwa wanajiachia na wako huru adi utapenda kuangalia habari.

lakin watangangazaji wa tanzania wamenuna sura mbuzi. ni kama watu wenye msongo wa mawazo tena fundi mitambo akichelewa kuweka tukio wanagandishwa wanakuwa kama sanamu la michelini adi wanatia huruma

Natumia operamin haina like
 
Wana JF, kama wewe ni mfuatiliaji wa kipindi cha BBC swahili cha Star tv kinachorushwa mida ya saa tatu kasoro usiku utakubali kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Utangazaji wa Salim Kikeke na watangazani wa Kitanzania. Pia utaona utofauti wa jinsi habari inavyopangiliwa.

Huyui jamaa na wenzanke kwanza wanatangaza wakiwa huru sana, yaani wanajiachia, wanatabasamu na ikibidi wanaleta jokes kidogo. Yaani kwa ujumla utatamani taarifa isiishe. Kwa upande wa kwetu hapa utaona watangazaji wanasoma taarifa wakiwa hawako huru kabisa, wanasoma taarifa kama vile wanatoa Tangazo kwenye mkutano, wanatangaza utafikiri wameambiwa mguu sawa kama jeshini. Nashauri vyombo vyetu vya habari wabadirike angalau waanze kuwa huru, waalike professionals mbalimbali ambao wanaweza kutoa ufafanuzi wa habari fulani angalau kuweka chachu katika habari.

Jamaa alianzia magic FM wakamtosa, amesota sana mpaka kufikia hapo alipo.
 
Tatizo watangazaji wetu wengi wazo hili mtu mshahara unakuta ajadaka miezi 2 kujiachia itakuwa tabu
 
Jamaa alianzia magic FM wakamtosa, amesota sana mpaka kufikia hapo alipo.

Nakumbuka enzi zile za Magic fm. Namkubali sana Salim Kikeke katika tasnia yake ya utangazaji wa habari. Big up dude
 
mimi ni joooooooji maratuuuu wa aaaaiiiiiii tiiiiiiiiiiiiiiiii viiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

Ni kweli Maratu yuko juu. Na kuna mtangazaji mmoja wa TBCCM huwa anajifanya kuingiza manjonjo ila hayamkubali na umemjaa udini huyo. Sijui ni nani lakini ni mwanababa. Na yule wa ITV anayepamba habari kwa sauti tamu ndo anaitwaje?Utasiki, "mwalimu huyooooo ametaka wazaziiiii kumpa ushirikianooo ili awe-ze kufundisha vemaaaaa"
 
Wana JF, kama wewe ni mfuatiliaji wa kipindi cha BBC swahili cha Star tv kinachorushwa mida ya saa tatu kasoro usiku utakubali kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Utangazaji wa Salim Kikeke na watangazani wa Kitanzania...

La kujivunia Kikeke.....Salim Kikeke ni mtanzania pia

Big up Kikeke.........Salim Kikeke!!!
 
Back
Top Bottom