Itakugomea endapo tu eneo sio ekari moja ya kupima kwa futi au kwa gps, njoo na maelezo zaidi
Mkuu nadhani kanuni uliyotoa namna ya kukokotoa idadi ya miche kwenye eneo husika inajieleza vizuri sana. Maelezo yangu ya ziada ni haya. Kwanza nimetoa mfano wa eneo husika kwa kutumia alama na herufi(rejea chini), pili nimetoa ufafanuzi wa herufi na alama, tatu nimeonyesha namna ya kukokotoa eneo lote na spacing, nne nimetumia kanuni yako kukokotoa idadi ya miche kwenye eneo la mfano na mwisho nimeonyesha ni namna gani idadi ya miche kwenye iliyopatikana kwa kutumia kanuni inatofautiana na idadi ya miche iliyoko kwenye mfano.
Karibu ufuatilie maelezo yangu kwa kina.
-------
o -o -o - o
I - I - I - I
o - o- o - o
I - I - I - I
o -o -o -o
=====
Rejea umbo la mstatiri wa herufi 'I', 'o', na alama '-' hapo juu. Alama '-' inawakilisha 2 m kati ya mche na mche, na 'I' inawakilisha 2.5 m kati ya stari wa miche na mstari mwingine wakati 'o' inawakilisha shimo la mche (mmoja).
Ukijumlisha idadi ya alama '-' kwenye mstari wa kwanza tu unapata alama 3 ambazo zinawakilisha upana wa mstatiri wa 6 m wakati ukijumlisha 'I' kwenye nguzo(column in an above rectangle) ya mstatiri huo hapo juu unapata 2 ambazo zinawakilisha urefu wa mstatiri ambao ni 5 m.
Kwa kanuni zetu za eneo, mstatiri huo una eneo la (upana X urefu)= 5 x 6 = 30 sq-m
Spacing (eneo linalotenga mche na mstari) ni sawa na [nafasi kati ya mche na mche (2 m) X nafasi kati ya mstari na mstari(2.5 m)] = 5 sq-m.
Tumeambiwa shimo lina mche mmoja (1)
Kanuni yako inatuelekeza kuwa Idadi ya miche =(Eneo lote /spacing) x idadi ya miche kwenye shimo.....eqn(i)
Nikiweka takwimu zangu hapo juu kwenye kanuni yako hapo kwenye eqn(i) ninapata kifuatacho:
Idadi ya miche = (30 sq-m / 5 sq-m) X 1 = 6. Napata miche 6. Lakini ukiangalia mstatiri wetu hapo juu utakuta idadi ya miche ni 12.
Kwa maelezo yangu hapo juu, nimekwama namna ya kutumia kanuni yako. Ebu, Mkuu, fafanua zaidi.