Watakaokwiba fedha za mapato ya gesi miaka 30 jela, kufilisiwa

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
gas.jpg

VIONGOZI na watumishi wa umma watakaoiba ama kutumia vibaya mapato yanayotokana na gesi na mafuta watafungwa miaka 30 jela pamoja na kufilisiwa.

Hayo yamefafanuliwa katika Sehemu ya VII ya Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Gesi ya mwaka 2015, Ibara ya 21 (1) na (2) ambayo inabainisha pia kwamba ofisa huyo atatozwa faini ya kiwango sawa na fedha alizozifisidi ama atakabiliwa na faini pamoja na kifungo kwa pamoja.

Soma zaidi hapa=> Watakaokwiba fedha za mapato ya gesi miaka 30 jela, kufilisiwa | Fikra Pevu
 
Mwanzo mzuri kuweka nidhamu kwa watumishi wa uma sheria hii isiishie kwenye gesi na mafuta tu bali iende kwenye sekta nyingine pia.

kika atakayeajiriwa ajulishwe kuhusu sheria hiyo. ikiwezekana waiimbe kama wimbo wa taifa kila wanapowasili kazini asubuhi.
 
Kuwafunga viongozi mafisadi 30 years? No...hiyo ni hadaa tu. Angalia sheria inatoa nafasi aliyeiba arudishe alichoiba. Hapo mafisadi watatumia mwanya huo wakijua watalipa walichoiba. See? Vipi sheria ya wahalifu illicit drugs? Cocaine, heroine, black tar, meth? Nao si 30 years au faini au vyote? Swali nani amefungwa 30 years kwa makosa haya? Well, mtu anaweza argue.....we have new government and JPM won't tolerate criminals lazima wafungwe. Siamini hivyo...serikali inatengeneza "hali ya woga" tu kujaribu kupambana na tatizo sugu la wizi/ufisadi.
 
Uvujaji mkubwa wa pato upo kwenye mikataba mibovu. Kipaumbele ilikuwa ni kupitia upya mikataba sekta ya gesi.

Na mikataba hiyo inakuwa ya muda mrefu mno, sidhani kama wanaweka muda wa ku review. Mkataba ukiisha wameshachimba gesi yote.

Kilichonishangaza zaidi matangazo kuwa gesi ya Helium imegundulika Tanzania yalitangaziwa wanahabari Japan, na katika mahojiano afisa wa Tanzania aliyehojiwa alisema hakuweza kuelezea chochote kwa wakati ule kwa sababu hakuwa na habari kamili. Nimebaki najiuliza gesi imepatikana Tanzania iweje hao wataalamu wasitangazie dunia wakiwa hapa Tanzania wakaenda kutangazia japan? Na waliwezaje kutangaza kabla wahusika sisi watanzania hatujajua kinachoendelea?

http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/06/160628_helium_gas_find_Tanzania

"Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia."
 
Gesi tu....

Dah shikamoo lugumi... Naibu sipika naagiza!!

Mungu wangu hii tz sijawahi ona..
 
JPM mbona alisha tweet hii kitu mkuu.
 
Kuwafunga viongozi mafisadi 30 years? No...hiyo ni hadaa tu. Angalia sheria inatoa nafasi aliyeiba arudishe alichoiba. Hapo mafisadi watatumia mwanya huo wakijua watalipa walichoiba. See? Vipi sheria ya wahalifu illicit drugs? Cocaine, heroine, black tar, meth? Nao si 30 years au faini au vyote? Swali nani amefungwa 30 years kwa makosa haya? Well, mtu anaweza argue.....we have new government and JPM won't tolerate criminals lazima wafungwe. Siamini hivyo...serikali inatengeneza "hali ya woga" tu kujaribu kupambana na tatizo sugu la wizi/ufisadi.
Hata Mtogo aliyehukumiwa na Mahakama Kuu Moshi mwezi uliopita hukuisikia?
 
JPM mbona alisha tweet hii kitu mkuu.

Gesi inayowindwa na dunia nzima inatangaziwa Japan na Raisi wa Jamuhuri ya Tanzania ana tweet! hiyo tweet mimi sijaiona. Alitakiwa kusema tena akijiamini Helium imeapatikana Tanzania na ni ya watanzania, Kama yeye hakuwa na nafasi hata waziri angefaa, itangazwe na mtanzania wakiwa hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom