Wataalamu kuacha kazi zao kukimbilia ubunge, tumeyataka wenyewe

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Kupanga ni kuchagua. Wote ni tumeshuhudia wateule, watumishi mbalimbali, wafanyabiashara viongozi was dini na hata wastaafu wakikimbilia fomu za kuwania ubunge. Hatujiulizi ni vipi mtu uache ukuu wa mkoa eti uka- beti ubunge?

Kuna mahala tumefanya kosa
Kazi ya ubunge, ya kuwatumikia wananchi wanyonge ilipaswa kuwa kazi ya kujitolea zaidi, kazi ya wito kazi ya kutetea maslahi ya wana wa nchi. Ubunge ulitakiwa kuwa ule ambao mtu akiambiwa toka nje ya bunge au umevuliwa ubunge muhusika ajisikie kutua mzugo mkubwa badala ya hali ilivyo sasa ambapo aliyevuliwa ubunge anasononeka kwa kupoteza mshahara, posho na kiinua mgongo.

Makosa makubwa tuliyoyafanya ni pale ambapo ubunge umekuwa chanzo cha mapato, njia ya kupata mitaji, njia ya kujinasua katika umasikini na kumuingiza mtu katika uchumi wa kati.

Wabunge hawako tayari kupoteza maslahi yao eti nini? Kisa anatetea waliomtuma. Mbunge ataambiwa chagua kutetea hao watu wako upoteze mtaji au upige kura ya NDIYOOO! upewe posho zaidi!

Wewe katika uchaguzi huo unahitaji tume huru? Jibu ni wazi. Kwa umasikini huu ulio tuzunguka hata ingekuja tume gani, kwa mashariti hayo, kura za NDIYOOO Zitatawala.

Chondechonde viongozi wetu, hasa wa chama kilichoshika utamu, tambua kuwa wakati ukuta! Leo mna nafasi ya kubadili upepo was watu kutulia katika nafasi zao katika vipindi vya uchaguzi. Wabunge wastaafu wapongezwe kwa madholuba waliyokumbana nayo katika harakati za kuwatetea wananchi wao, ikiwezekana kuwapa tuzo walioibua hoja za kitaifa za msingi. Usiwe wakati wa mavuno, wakati wa kufungua biashara, au wakati wa wateule wa Rais kutupilia mbali nafasi zao kanakwamba walijishikiza tu huku wakisubiri kugombea kazi inayolipa zaidi, yenye mshiko, yenye maslahi binafsi.

Watu tuone kuwa kazi ya ubunge ni ya kujitolea
Bwana Polepole, Bwana Kabudi, Bwana Bashiru na hata viongozi wetu was kitaifa Mh. Rais, Makamu wako, Waziri Mkuu hili halionekani Kama tatizo? Achilia mbali kuwa baadhi ni wafaidika wa maslahi hayo, lakini si unaweka uzalendo mbele? Si unafanya kinachowezekana wakati upo kwenye nafasi kuliko kuwa Kama Membe kulalamikia tume huru baada ya kutoka kwenye uringo?

Membe alipogombea u Rais kwa tiketi ya CCM hakukuwa na shida ya tume huru. Kagombea Kama mpinzani ndio miwani ya mbao anaivua na kuona kuwa loh! kumbe tume sio huru.

Tujifunze kwa makosa ya wenzetu.
 
Ubunge ni ajira ya wanyonge 🤣🤣🤣 halafu fomu yenyewe laki tu! Wacha watu wauwane kuwania kinyang'anyiro cha mkopo wa VX V8
 
Hili ni Tatizo kubwa kwa Taifa letu, lakini bwana yule halioni, Wanataaluma, Wanajeshi na Polisi kwenda kwenye Siasa. Madikteta Mara kwa Mara wanapenda kuwa karibu na wajeshi kwa hofu ya kupinduliwa.
 
Ni kupitia sanduku huru tu la kura ndipo haya yote yatarekebika. La sivyo, bunge litabaki kuwa chanzo cha kipato na mitaji. Nani hataki utajiri?
 
Back
Top Bottom