Wataalamu Dadavueni nyie mie kichwa gongana

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
484
541
Viwango vya juu vya tozo ya Serikali vimepunguzwa kutoka sh. 7,000/- hadi 4,000/-(kwa wanaotuma zaidi ya sh. 3,000,000/-). Viwango vya chini vimepunguzwa kutoka sh. 100/- hadi shilingi 10/- (wanaotuma kati ya sh. 100/- hadi 2,999/-)

UFAFANUZI WA KINA UTATOLEWA NA WIZARA YA FEDHA
 
Waambie Watanzania hawataki Tozo kwasababu kabla hawajafikiria kupunguza,wakumbushe kuwa haikuwepo kwahiyo iondolewe na sio kupunguzwa,nipo hapa njiani naelekea Burundi kama wanavyotaka.
 
Siyo pekee yako, tuko wengi, mwezi huu katikati nilitamani kufunga kabisa na account yenyewe. Nilitumiwa hela ya kimarekani, kutoa ndiyo ngoma. Panga kwa kwenda mbele, hata malipo niliyotakiwa kufanya niliahirisha kwa siku mbili nikitafuta namna ya kuongezea
 
Acheni kuwaza too wakuu kuleni maisha why mjipe stress na maisha yenyewe mafupi haya.
 
Viwango vya juu vya tozo ya Serikali vimepunguzwa kutoka sh. 7,000/- hadi 4,000/-(kwa wanaotuma zaidi ya sh. 3,000,000/-). Viwango vya chini vimepunguzwa kutoka sh. 100/- hadi shilingi 10/- (wanaotuma kati ya sh. 100/- hadi 2,999/-)

UFAFANUZI WA KINA UTATOLEWA NA WIZARA YA FEDHA
Kwa mkanganyiko huu, inaonesha wazi hakuna sheria maalum ya kiwango au asilimia za makato kwasababu NI WIZI!

Huu ni wizi kwasababu tatizo sio kiwango, ila tatizo ni KWANINI WAKATE TOZO ZAIDI YA MARA MOJA KWA KIPATO HICHOHICHO KIMOJA?
Pesa tayari imekatwa kodi (PAYE) Kwa wafanyabiashara tayari wamelipa kwa kupitia ushuru, na bado ukiweka benk ma kutoa unakatwa fedha hiyo hiyo. Jamani huu ni wizi.

Kupunguza au kuongeza haisaidii chochote. Watoe maelezo ya kwanini wakate tozo na kodi zaidi ya mara moja?
Na isitoshe hayo makato wanayotoa kwenye taarifa zao sio sahihi. Ukweli ni kwamba wanakata zaidi ya hapo kwa kushirikiana na bank au taasisis ya fedha husika. Kwa sasa ukiacha benk hata tsh elfu 5, baada ya muda huikuti, wanakata service charge-sijui!
 
Back
Top Bottom