WATAALAM TU: Kwa hoja za kitaalam, kwa nini nyumba hii iwekewe umeme?

Avatar

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
11,127
11,908
Naomba hoja zitumike kujibu swali la msingi.

Karibuni.
IMG-20190330-WA0014.jpeg

Sent by anonymous user
 
Hii hapa chini ni moja kati ya sehemu ya hotel kubwa tu na ina umeme sasa sijui tatizo ni nn hapo. View attachment 1057938

Ndio maana tumeambiwa tujadili kitaalam. Ukiangalia uimara na aina ya kuta za hiyo hoteli na ile nyumba havifanani kabisa, nyumba ukuta wake ni mbavu za mbwa (fito zilizofunikwa kwa tope) ukita ni mwembamba sana na mvua huendelea kumomonyoa udongo hadi ukuta kubaki wa fito tupu.

Ukuta wa hoteli ni wa matofali ya udongo lakini ni mnene na uko imara. Paa ni la nyasi lakini ndani umeona walivyotengeneza? Hiyo vyumba ya makazi haina dari.

Kwa hayo maelezo machache, miundo mbinu kama waya, swichi, plag na vishikio vya taa na vifaa vingine havitakua na sehem imara ya kushikiliwa kwenye ukuta duni. Hata vikikaa kwa muda, vitachomoka tu na kusababisha majanga.

Bora wangeambiwa zipigwe lipu imara ya udongo ndani na ziwekewe mbao au miti imara juu kutengeneza dari la kuweka nyaya vizuri kwa usalama.

Sio lazima nyumba ziwe za block, hata za udongo imara zinaaeza wekewa umeme.
 
Ukiona nyumba imeezekwa kwa "kuhomakela" ni ushahidi wakati wa mvua ni mtindo wa kuhamisha vitanda.

Kwa elimu yangu ya darasa la 7, niliambiwa maji na umeme hayapatani..

Tumerithishwa usiasa usiasa, hata mtoto mdogo sikuizi wamejaa siasa,, sijuui hii ni tabia ya ki genetic
Wanajibu kisiasa....
Lakini tukija kitaalamu haikuwa sahihi.
Lifetime ya hiyo nyumba ni ndogo sana hapo tutasikia majanga ya umeme tuu huko

Sent by anonymous user
 
Ukiona nyumba imeezekwa kwa "kuhomakela" ni ushahidi wakati wa mvua ni mtindo wa kuhamisha vitanda.

Kwa elimu yangu ya darasa la 7, niliambiwa maji na umeme hayapatani..

Tumerithishwa usiasa usiasa, hata mtoto mdogo sikuizi wamejaa siasa,, sijuui hii ni tabia ya ki genetic

Sent by anonymous user
Inategemea vimekutana wapi... Huku kijijini kwetu vinapataka vizuri tuu yani huwezi kuamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu swali kwa jibu sio kwa swali. Kama sio mtaalamu tafuta sredi nyingine

Ndio ninaweza kukujibu, na baadhi ya majibu yapo comment za juu
Na wewe unaweza kutuambia kitaalamu kwanini hii nyumba haipaswi kuwekewa umeme ?

Sent by anonymous user
 
Mkuu tatizo la huyo bwana kavamia tu, hakuchukua hata dk 1 kutafakari swali.

Kwa maelezo yako maridadi, nitamwomba huyo bwana arudi tena sasa.. Hatoweza kutoka kapa hapa.

Unaanzaje kulinganisha hoteli ya nyota ngapi huko kwa hako kajumba...!

Ndio maana tumeambiwa tujadili kitaalam. Ukiangalia uimara na aina ya kuta za hiyo hoteli na ile nyumba havifanani kabisa, nyumba ukuta wake ni mbavu za mbwa (fito zilizofunikwa kwa tope) ukita ni mwembamba sana na mvua huendelea kumomonyoa udongo hadi ukuta kubaki wa fito tupu.

Ukuta wa hoteli ni wa matofali ya udongo lakini ni mnene na uko imara. Paa ni la nyasi lakini ndani umeona walivyotengeneza? Hiyo vyumba ya makazi haina dari.

Kwa hayo maelezo machache, miundo mbinu kama waya, swichi, plag na vishikio vya taa na vifaa vingine havitakua na sehem imara ya kushikiliwa kwenye ukuta duni. Hata vikikaa kwa muda, vitachomoka tu na kusababisha majanga.

Bora wangeambiwa zipigwe lipu imara ya udongo ndani na ziwekewe mbao au miti imara juu kutengeneza dari la kuweka nyaya vizuri kwa usalama.

Sio lazima nyumba ziwe za block, hata za udongo imara zinaaeza wekewa umeme.

Sent by anonymous user
 
Hakuna tatizo mkuu umeme wa REA tunafunga hadi kwenye mashimo wewe tuelekeze tu shimo lako lilipo tunafika hii ndio serikali ya wanyonge umeme sio anasa tena,matajiri wataishi kama mashetani wanyonge wanafutwa machozi na kupunguziwa ukali wa maisha.
 
Mkuu niliamini kwa kuandika kwa herufi kubwa japo maudhui ya uzi yataeleweka..! Hali imekuua tofauti kwako
Hakuna tatizo mkuu umeme wa REA tunafunga hadi kwenye mashimo wewe tuelekeze tu shimo lako lilipo tunafika hii ndio serikali ya wanyonge umeme sio anasa tena,matajiri wataishi kama mashetani wanyonge wanafutwa machozi na kupunguziwa ukali wa maisha.

Sent by anonymous user
 
Huu umeme bhana Kuna kipindi inafika kijijini nilifuatilia kweli niweke kwa bimkubwa ila nilishindwa na nyumba iko vizuri!
Sijui kutakua na awamu nyingine?
 
Back
Top Bottom