Waswahili tunatawaliwa na waarabu ?

rreporter2010

Member
Nov 7, 2010
34
1
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.
 
Usiogope haitatokea.
Kama wangeomba wasingepata.

Na Kiswahili si lugha ya pekee iliyoazima sehemu kubwa ya msamiati wake kutoka wengine. Kiingereza ni vile (mchanganyiko Kijerumani / Kifaransa).
Wahsiapania na Waitalia n.k. waliazima lugha yooote kutoka Waroma na Kilatini.
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

SWALI NI LA AJABU KIDOGO!

  1. hakuna hatimiliki katika utamkaji wa maneno.
  2. Kila lugha duniani ina maneno yenye asili ya sehemu nyingine. Kwa hiyo hata Kiarabu kina maneno yenye asili ya lugha zingine.
  3. Maneno mengi kati ya "theluthi moja" uliyoitaja hapo juu, sio Kiarabu "per se" bali ni yenye "ASILI YA KIARABU"
  4. Si kweli kuwa kwa kutumia maneno ya "yenye asili ya kiarabu" basi tunatawaliwa na waarabu. Hakuna anayetulazimisha, na wala Kiswahili hakikutengenezwa na waarabu kama njia ya kututawala. Tungekuwa tunatumia kiarabu halisi basi labda kungekuwa na ukweli fulani. Inawezekana wanatutawala kwa kwa njia nyingine lakini si lugha
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Hiatatokea waarabu wakasema tusitumie lugha yao maana hata wao kwenye lugha yao kuna maneno wameyatohoa kutoka kwenye lugha nyingine. Pia Duka sio neno la asili ya kiarabu ni neno la Kigujarat cha nchini India.
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.
Hivi unazungumzia wanaweza wakatukataza kutumia maneno au maana ya maneno.......??? Nionavyo spelling za maneno uliyoyalinganisha ni tofauti though maana ni moja................daftar - daftari, asbuh-asubuhi............
 
Kuna vyombo vingi kama (TUKI,BAKITA,BAKIZA,CHAKITA,BAKAMA) vinavyo husika na maendeleo ya kiswahili .visikae na kupunguza baadhi ya maneno ya lugha nyingine kwenye lugha yetu.kama tulivyo fanikiwa kupata msamiati ya baadhi ya maneno kama Television ,computer,Information Technology,Internet n.k .Hivyo hivo tunaweza kupunguza maneno ya kiarabu kwa kuyatafutia misamiati ya kiswahili.
 
Sikazi rahisi Rahisi kupunguza maneno ya kiarabu kwenye kiswahili kwa sababu maneno ni mengi sana kiasi kwamba unaweza ukapewa PHD ya heshima endapo utafanikiwa kufanya hivyo.
Ngoja niwaongezee maneno mengine 11 ambayo kila mmoja wetu anayatumia kila siku,Haya maneno tumeyachukua kama yalivyo
1.Tajiri 2.Sukari 3.ghali 4.Rahisi 5.mhandisi 6.robo 7.Nusu 8. kaskazini 9.Kusini 10.Mashariki 11.Maghalibi.

Samahani - lakini jwa nini wapunguze maneno yenye asili ya Kiarabu? Bila maneno haya hakuna Kiswahili chenyewe.
 
Sikazi rahisi Rahisi kupunguza maneno ya kiarabu kwenye kiswahili kwa

sababu maneno ni mengi sana kiasi kwamba unaweza ukapewa PHD ya heshima endapo utafanikiwa kufanya

hivyo.
Ngoja niwaongezee maneno mengine 11 ambayo kila mmoja wetu anayatumia kila siku,Haya maneno

tumeyachukua kama yalivyo
1.Tajiri 2.Sukari 3.ghali 4.Rahisi 5.mhandisi 6.robo 7.Nusu 8. kaskazini 9.Kusini 10.Mashariki

11.Maghalibi.

Sahihisho hapo kidogo, neno Kusini kwa kiarabu ni al-Janūb (الجنوب), na Kaskazini ni ash-Shamal (الشمال), kama kuna makosa wataalam wanaweza kusahihisha...!

Na neno Magalibi, linaandikwa Hivi: Magharibi.

Ila ni kweli maneno mengi sana yanatokana na lugha ya kiarabu...! yakiwemo...

Saa, Nia, Kanuni, Katili, Kismati, Kauli, Kiyama, Razi, Salamu, Sababu, Salama, Asubuhi, Taaruki, Taarifa, Jamhuri, Siasa, Dar ES salaam, Alhamisi, Ijumaa, Sifuri, Sita, Saba, Tisa, Arobaini, Hamsini, Sitini, Saba, Sabibi, Themanini, tisini, mia, Alfu, Maji, Bin Adam, binamu, Chemia, Darasa, Chuo, Kanisa, Askofu, Bahari, Amir, adobe, algebra, algorithm, algorism, Alkali, Kahawa, Gitaa, hashish, Jaa, Jasimini, jinn, Safari, Tafsiri, sofa, Spinachi, Sukari, Askari, Sultani Swahili, Mahari, Kitabu, Maktaba, Zahanati, Tarehe, Takriban, Takrima, Umri, Walidi, Wakili, Watani, Yatima, Zalimu, Zani, Zikiri, Ziara, Zulumu, Samaki, Tuna (aina ya samaki), Riwaya, tamthilia, haramia, Jasusi, Sauti, zamani, Dunia, Hatari, Mahali, Msumari, Kata, Habari, Huru, Dhamiri au Dhamira, Kamusi, Baridi, Samahani, rafiki, tafadhali, Furahi, asubuhi, dakika, Mauti, wakati, Alfajiri, alasir, Karne, Tausi, Saidia, Jadi, Kabila, Karatasi, Waziri, Rais, Fedha, Mhasibu, Hesabu, Haki, Dini, Swali, Suhala, Ahsante, shukrani, Thabiti, zaituni, shughuli, Mtihani, Mahakama, Muktasari, thibiti, Ardhi, Adabu, akili, Ashiki, Ajabu, Asiri, Azabu, Awali, Badala, Balaa, Bila, Dawa, Dawati, Dua, Faida, Fakiri, maskini, Tajiri, Fahamu, Faraki, Fikiri, Fitina, Fursa, Ghairi, Hakimu, Halali, Haja, Hakika, Haramu, Hawa, Hawala, Hekima, Himaya, Hukumu, Tabasamu, Hisani, Elimu, Mwalimu, Jahazi, Jeneza, Jawabu, Majununi, Kafiri, katibu, Kalamu, Karimu, Khalisi, Kufuru, Laa, Lazima, Mahiri, Mahaba, Marehemu, Malkia, Msafiri, Mushkeri, Nafsi, Nasibu, Safi, Sharti, Binti, Aghini, Birika, Aibu, Anwani, Afiki, Arusi, Bei, Budi, Deni, Dai, Enzi, Faharasa, Ghasia, Hadi, Ibilisi, Jasho, Kaidi, Madini, Miliki, Naam, radi, Zaidi.

Na mengine mengi ambayo sikuweza kuyakumbuka...

Lakini si Kiswahili tu, ambacho kimetohoa maneno ya kiarabu, hata baadhi ya Lugha kama vile kiingereza, Kispania, Kifaransa, Kireno, na hata Kilatini, pia zimekopa baadhi ya maneno kutoka kwenye Kiarabu, na hii wala si ajabu kwa sababu, lugha kuu karibia zote zimeazimana baadhi ya maneno ambayo kwenye lugha yao hayapo...!
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Mkuu,

Kitu gani hasa kilichokujengea hofu hii?

Au uliota ndoto ulipolala, waarabu walikujia wakakwambia usitumie maneno yenye asili ya kiarabu unapozungumza kiswahili chako?

Je umeshawahi kufanya uchunguzi ukagundua jambo kama hili limeshawahi kutokea kwa lugha nyengine?

Je una lugha nyengine mawazoni mwako ambayo tunaweza kukopa huko na tusiwe na wasiwasi kuwa itatokea siku wenyewe watatuambia kuwa tusitumie maneno yao?

Kuna mwanaJF mmoja, Jerusalem ,yeye alisema wazi "I hate Kiswahili.It is arabic, the language of islam" Kitu kama hicho. watu wengine bwana!!

Umenifanya nijiulize masuali mengi sana, mkuu!

Muulize Mtu wa pwani, member hapa JF, suali hili, Kiswahili ni lugha ya nani?
Utafurahi majibu yake. Kama wewe si mswahili basi lugha si yako, waachie wenyewe!!

Pia nenda TUKI uone juhudi wanayoifanya katika kutohoa maneno kutoka lugha za kibantu kuyaingiza katika Kiswahili.

Pia Zungmza na Prof. Batibo ,UDSM,juu ya chimbuko na ukuaji wa lugha.
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza.
waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........
maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa.
NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.

Theluthi ukimaanisha one third? 1/3, ndio? kama ni hivyo basi umekosea, Kiarabu kina zaidi ya asilimia hamsini 50% ya maneno ya kiarabu kama si sitini.
 
Si zaidi ya 25% ya Kiswahili ni Kiarabu.
INGEKUA 60% YA KISWAHILI NI KIARABU KAMA BAADHI WANAVYODAI BASI WAARABU WASINGEKUA NA HAJA YA KUWA WAKALIMANI KUELEWA KISWAHILI. NA WATANZANIA WASINGEKUA NA HAJA YA MKALIMANI AU KUJIFUNZA KIARABU MAANA WANGEELEWA BILA SHIDA.

NILIWAHI KWENDA UARABUNI, NIKAWA SISIKII CHOCHOTE PUNDE WANAPOANZA KUZUNGUMZA KIARABU. NDIO UNAWEZA BAHATISHA NENO MOJA KATIKA SENTENSI NZIMA LAKINI HII HAIKUWEZESHI KUELEWA SENTENSI ILIKUA INA MAANA GANI.
 
Mwenye data sahihi atuwekee,
1. idadi ya maneno ya kiswahili yote
2. yenya kie asili ya kibantu
3. yenye asili ya kiarabu
4. yenye asili ya kingereza
5. yenye asili ya kihindi
6. yenye asili ya kiajemi
7. yenye aili ya kireno
8. yenye asili ya kijerumani
9. yenye asili ya ...................n.k
then wataalamu wa mahesabu watajua asilimia ya maneno ya kiarabu kwenye kiswahili. kama hamna data hamna uhalali wa kuongea, msije kuleta falacies.
kuhusu kutawaliwa na waarabu kwa kuwa tunatumia lugha yao hizi ni ndoto, na hawawezi kusema tuache kutumia maneno yaliyo katika lugha yao hata siku moja, kwani ni waarabu wangapi wako huku kwetu na hawajui hicho kiarabu, wanazungumza kiswahili tu!.
 
Makadirio niliyoona ni asilimia 40 hivi kwa jumla. Nikisoma maandishi juu ya habari za kidini inaweza kuwa juu zaidi, katika mada nyingine itakuwa chini yake.

Ningependa pia kuona takwimu halisi lakini sijaona.

Lakini hata nusu ya maneno ya asili ya kiarabu (au 60, 70 %) haimaanishi ya kwamba wasemaji wa lugha hizi wanaweza kusikilizana.
a) sarufi si kiarabu; kwa hiyo sentensi na muundo wake ni tofauti kabisa.
b) maneno yanabadilika maana mara nyingi baada ya muda katika mazingira tofauti.
c) matamshi ya sauti nyingi za Kiarabu hayapo kwa Kiswahili kwa hiyo mara nyingi si rahisi kutambua kama neno lina asili ya kiarabu hadi uione kimaandishi (ukijua Kiarabu).
 
Mwenye data sahihi atuwekee,
1. idadi ya maneno ya kiswahili yote
2. yenya kie asili ya kibantu
3. yenye asili ya kiarabu
4. yenye asili ya kingereza
5. yenye asili ya kihindi
6. yenye asili ya kiajemi
7. yenye aili ya kireno
8. yenye asili ya kijerumani
9. yenye asili ya ...................n.k
then wataalamu wa mahesabu watajua asilimia ya maneno ya kiarabu kwenye kiswahili. kama hamna data hamna uhalali wa kuongea, msije kuleta falacies.
kuhusu kutawaliwa na waarabu kwa kuwa tunatumia lugha yao hizi ni ndoto, na hawawezi kusema tuache kutumia maneno yaliyo katika lugha yao hata siku moja, kwani ni waarabu wangapi wako huku kwetu na hawajui hicho kiarabu, wanazungumza kiswahili tu!.

Hoja ni zuri lakini nisipokosei hakuna aliyekamilisha kazi hii. Sidhani hatua 1) tayari, na bila hii takwimu haiwezekani.

Katika post hii nimetia rangi maneno yote yenye asili ya kiarabu , na pia za asili ya Kiingereza (isipokuwa kiingereza yenyewe ni lugha yenye asili ya mchanganyiko: "data" kutoka Kilatini, falacy Kifaransa nisipokosei. "Kiingereza" ni kutoka Kireno "ingles")
Sijui kama nimepata maneno yote? Kuhusu "hoja" sina uhakika, nilikuwa mvivu kufungua kamusi.
 
Sikazi rahisi Rahisi kupunguza maneno ya kiarabu kwenye kiswahili kwa sababu maneno ni mengi sana kiasi kwamba unaweza ukapewa PHD ya heshima endapo utafanikiwa kufanya hivyo.
Ngoja niwaongezee maneno mengine 11 ambayo kila mmoja wetu anayatumia kila siku,Haya maneno tumeyachukua kama yalivyo
1.Tajiri 2.Sukari 3.ghali 4.Rahisi 5.mhandisi 6.robo 7.Nusu 8. kaskazini 9.Kusini 10.Mashariki 11.Maghalibi.

Hizo redi mwana jamvi zina furahisha maana zingine umechanganya zaidi. Mfano Nusu hakuna kwenye kiarab neno hili ila kuna Nisfu.
Tajiri ukifuatilia kwa umakini utaona waswahil wanapotosha maana ya Tajiri ni mfanyabiashara. Tafaut na maana ya waswahil wachache yaani mwenye uwezo wa mali.
Pia kaskazini hilo neno hakuna kwenye kiarabu.
Wengine watusaidie!
 
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu , zenye kubeba maana na zilizokubalika na jamii zitumike ili kuwasiliana.

haya tuzidi kuogelea kenya bahri hiyo
 
mmm reporter umenifurahisha sana endapo wenyewe watataka tusitumie maneno yao maana siyo lugha ukisema lugha una kosea kwani kiswahili kina maneno mengine mengi kotoka lugha nyingine za kibantu na hata hivyo isikupe hofu kwani moja ya sifa za lugha ni kukua sasa itakuwaje kama haijajiongezea misamiati kutoka lugha nyingine hivyo usiofu haiwezi tokea kwani hata wa CHINA wamekopa lugha kutoka kwa majirani zao wajapani na wa korea
 
Lugha itumike kuwaunganisha watu na si kutenganisha. Tatizo kuna baadhi ya watu wanachuki sana na waarabu hapa. Maneno ya kiarabu yame tajirisha lugha ya kiswahili. mashairi unayosikia redioni ni fanisi za kiarabu, Mziki wa taarabu pia una asili ya kiarabu. Popote pale duniani watu wa mataifa tofauti wanapojumuika hutajirisha lugha, utamaduni na mila zao na huwa wana jivunia hilo. Kibantu pekee hakina lolote la kufanya lugha ya maana.
 
Lugha ya kiswahili ilianza takriban miaka 800-1000 iliyopita,Kiswahili ni sarufi na msamiati wa Kibantu pamoja na maneno mengi ya Kiarabu. zaidi ya theluthi moja ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu.kuna maneno machache ya kiajemi,kihindi ,kireno na kingereza. waswahili bado tumetawaliwa na Waarabu kupitia kwenye lugha.Tanzania ,Kiswahili ni lugha ya Taifa.mfano wa maneno ya kiarabu tunayoyatumia ni suku-soko,dukan-dukani,shai-chai,bahri-bahari,samaku-samaki,rejea-rejea,daftar-daftari,asbuh-asubuhi,........ maneno ni mengi siwezi kuyataja yote hapa. NINI KITATOKEA ENDAPO WAARABU WATAKAA NA KUTUOMBA TUSITUMIE MANENO YAO ?,KISWAHILI KITAKUFA?.
Hebu tuomdolee upupu wako hapa. Kwani hujui kuwa hata lugha ya mama yako pia ina maneno yenye asili ya lugha zingine. Hata Kiingereza kina maneno yenye asili ya Ufaransa, ujerumani, poland na kwingineko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom