Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
TANGA KWETU
Ni ukweli usiopingika kuwa wazungumzaji wazuri wa lugha ya kiswahili ni watu wa pwani, jambo hili limechangiwa na sababu kadha wa kadha lakini kubwa ni sababu za kihistoria na maingiliano ya watu wa pwani na jamii za kale za waarabu waliofika na kufanya makazi katika ukanda huu miaka mingi iliopita, maingiliano hayo ndio chanzo cha kuzawa lugha hii ya kiswahili.
Neno swahili linatokana na neno la kiarabu ساحل "saahil" lenye maana ya Pwani au mwambao au ufukwe, hivyo waswahili "سواحليون"(sawahiliyun) nii wakaazi wa wa ukanda wa pwani. Kama ilivyo katika lugha nyingine mzungumzaji mmoja anaweza kutafautiana na mwingine, mtindo huu wa kuzungumza wenye utafauti hujumuisha matumizi ya maneno tafauti na matamshi tafauti (lafudhi), utafauti huu baina ya wazungumzaji wa lugha moja huitwa " lahaja" na lugha moja huweza kuwa na lahaja mbalimbali.
Mji wa tanga na mwambao wake ni katika wazungumzaji wazuri wa kiswahili kinachovutia kukiskiza. Lahaja hizi za kiswahili cha mji wa tanga huitwa kimtang'ata (kiswahili cha Tanga) na kimrima (kiswahili cha mwambao wa Tanga).
sifa kubwa ya lahaja hizi ni uzungumzaji wake wa kasi ya wastani usio wa haraka kama lahaja ya kipemba, na usio wa taratibu sana kama lahaja ya kiamu (kiswahili cha Lamu). Lakini pia wazungumzaji wake hupenda sana kufupisha vitenzi wakati wa kuvitamka, Kama kusema naja badala ya ninakuja, napika, nachoka, naenda.
Mfano wa utumiaji wa maneno yanayoweza kumtambulisha haraka mswahili wa Tanga ni kama odo" mama mdogo"
ngogwe "nyanya chungu" uono. Kimrima nacho ni lahaja ya kiswahili cha mwambao wa Tanga. Kiswahili hiki khaswa huzungumzwa maeneo ya digo kama vile Moa, Vanga, Pangani, Mwarongo, Tongoni, Kwale, Vyeru, Monga na Kichalikani, baadhi hukiita kiswahili cha kidigo kutokana na wazungumzaji wake kuzungumza kwa madaha ya kidigo.
lahaja nyengine za kiswahili za mwambao ni kama kiamu, Kisiu, kipate kingozi, kibajuni, Kibarawa na kimvita, kiunguja na kipemba.
Baraza ya kiswahili la tanzania limechagua lahaja ya kiunguja kuwa ndio lahaja ya kiswahili sanifu(fasaha).