FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,776
Nipo katika mazingira ambayo huwa naona kazi za hawa vijana wa chuo kikuu cha DSM mara kwa mara. Kiukweli misingi yao ya kielimu ni mibovu. Assinment wanazopewa huwa wanapata shida sana kuzijibu kiufasaha, hasa kiingereza kinapohusika. Kiingereza chao ni kibovu mno. Aghalabu sisi wabongo huwa tunajua zaidi kingereza cha kuandika kuiko cha kuongea, lakini kwa hawa vijana wetu ni tabu tupu. Huwa najiuliza hao walimu wao wanaposoma kazi zao huwa wanakuwa katika hali gani.
NB: Nami pia ni alumni wa UDSM
Mara kwa mara mimi huuliza, hizo shule walienda kusomea ujinga? huwa sipati jibu, lakini naona wewe at least umekuja na jibu linaloyakinisha nnachokiuliza siku zote humu JF.