Wasomi wetu na tabia za kuiga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi wetu na tabia za kuiga

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Godwine, Apr 11, 2010.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kwanini watu walioelimika wasionyeshe mfano mwema katika tabia wao ndio wamekuwa mstari wa mbele katika kuonyesha ni jinsi gani jamii inaweza kuishi katika uzinzi ulevi na kila aina ya machukizo, je hii inatupa picha gani kwa wasomi wetu? je kuna mapungufu gani kwa wasomi wetu katika kuishi maisha yaliyo safi?
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu as one of JF member nadhani inabidi ujumbe wako sijauelewa sana kwani hauna justification; kama ni machukizo na ulievi nadhani jamii ina watu wengi sana wa namna hiyo na wengine hawajasoma... na kama ni usomi basi naamini walio na usemayo hawafiki twenty percent

  can you please clarify your allegations kwa wasomi wetu ili tuwe fair?

  we dare talk openly so please dare to talk openly
   
 3. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Kunatofauti kati ya kusoma na kuelimika,hao wamesoma tuu na hawakuelimika!!
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kusoma si kuelewa, na kuelewa si kusoma,

  na kama ingekuwa hivyo? basi mpaka leo kusingekuwa

  na wafuasi wa qurani t'ukufu ambao ni wasomi maana

  mule namo ni matatizo matupu,

  samahani lakini kwa kutolea mfano huo

  lakini sina jinsi maana nimeona ni rahisi sana
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wasomi ni wale wenye kufungua makanisa na kujiita mitume na manabii kila kukicha, uku wakila lile fungu la kumi toka kwa wsomi wengine.
   
 6. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pia kuna wale wasomi wanaojiita mapadri ambao hawataki kuoa na kazi yao ni kunyemelea wake na watoto wa kike na wa kiume ili kuwafanya vibaya kwa kutumia nafasi zao ndani ya nyumba za ibada.
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kuiga ni lazima ndio maana kuna maendeleo,watu huga na kendeleza yale mazuri na mifano hipo kuanzina kina Einteinet al....hiyo ndiyo misingi ya maendeleo,sizungumzii kuinga "upuuzi"
   
 8. T

  Tall JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Una pokuwa shule,kuanzia dayone akili yako yote kwenye masomo,hadi unapata kadegree kako, sasa looooh unakuja shituka mambo mengi yamekupita, ngono/ulevi na mengine mengi, kwa ajili hiyo hawa jamaa huvamia hizi fani za watu na kuumbuka.Si unajua tena,hana uzoefu,konyagi mzinga mmoja hoi,haya kwenye ngono mara huyu mara yule,yaaani fujo tu.Hapa siyo wasomi wote ila wale ambao ndio kwanza wamegraduate ndio spidi yao kali maili 1000 kwa dakika.Tuwavumilie wakikua wataacha.
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  sema ujengele sema.
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ni wakristo Vs waislam tena??
   
 11. Katibukata

  Katibukata Senior Member

  #11
  Apr 12, 2010
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 183
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hata sioni hoja ya kujadili hapa. Mtu mmoja kabadili nia ya mtu aliyeanzisha thread hii... Makanisa Vs Misikit.!! Loh!!

  Binafsi naamini kwamba tabia chafu/mbaya ya mtu haina uhusiano na kabila lake, dini yake utaifa, elimu yake etc. Kama mtu ni mwizi , mchawi , mlevi au kahaba ni TABIA yake tu.
   
 12. T

  Tall JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  mmmmmmmmmmmh yamekuwa hayo,kwaherini,nahamia thread nyingine
   
 13. G

  Godwine JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  unafahamu jamii nyingi duniani wanategemea kupata mfano mwema kutoka kwa wasomi kwa mfano ukiangalia maisha ya wasomi katika nchi za swiss, china, na cuba
  unaona jinsi walivyojengeka kuishi vyema na jamii yao, lakini kwetu wasomi ndio walio katika mstari wa mbele katika uovu , hii sijui inatokana na wao kutopata elimu stahili au mfumo wa elimu yetu, kwa mfano ukiona takwimu zinazoonyesha kuhusu watu waathirika wa ukimwa unakuta wasomi ndio walio katika ngazi ya juu katika kupata ugonjwa huu, pia wasomi wetu wameshindwa kuwa mfano wa jamii yetu, nini tatizo la wasomi wetu?
   
Loading...