Wasomi wetu na kigugumizi cha "academic papers publication"

Kipilipili

JF-Expert Member
May 25, 2010
2,272
1,882
Habari wana ukumbi!
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiliona tatizo/changamoto hii ya upungufu wa "academic papers" katika "international journals" mbalimbali kwa upande wa wasomi wa Tanzania. Kwa kifupi ni kwamba wasomi wetu wengi hawa"publish" academic papers zao. mfano,mtu anasoma degree ya kwanza/ masters/PhD mpaka anamaliza hajawahi ku"publish" paper yeyote na pengine hata hajui ni kitu gani. matokeo yake thesis/desertation zinabakia vyuoni zikipigwa na vyumbi maktaba.Hali hii huwapa ugumu sana wanafunzi wengine wa ndani na nje ya nchi wanapotaka kuandika kazi zao kwa sababu wanakosa "literature reviews" za kutosha kuhusu kada husika kwa upande wa Tanzania.
Katika baadhi ya nchi huwezi kumaliza undergraduate au postgraduate bila kufanya "publication" yaani hiyo huwa ni sehemu ya mahitaji ili uweze kuhitimu. Kwa Tanzania hili halipo katika vyuo vingi. Publication ni njia ya kumfanya mwanafunzi kuwa mahiri katika kada yake ya taaluma na pia ni njia ya kukifanya chuo anachosoma kukuza hadhi yake ya kitaaluma.
Je kigugumizi hiki cha wasomi wetu kinasababishwa na nini? TUJADILINI kwa maslahi ya taifa na hasa kukuza professionalism na kuviongezea hadhi vyuo vyetu kwa sababu moja ya kigezo kinachotumika ku"rank" vyuo duniani ni IDADI ya publications ambazo ama wanafunzi au walimu kutoka vyuo hivyo wamefanya kwa mwaka husika.
Asanteni.....
NB:Kama hii"haikuhusu" basi naomba upite kimya
 
Academic writing haipewi emphasis ya kutosha katika vyuo vyetu...ni kweli unachosema..hata usomaji wa new articles bado watu wako busy wanasoma vitabu most of which vya zamani...cha muhimu ni kuweka conditions tu every masters dissertation lazima iwe published au inapublication potential...phd minimum 3 publications....
 
Publication ni muhimu sana, sio tu inainua hadhi ya chuo husika bali pia inamfanya mtu ajione kweli yeye ni msomi na anapotential.
 
Back
Top Bottom